Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Ngoja wake tuone ila tatizo linakuja wenye hio mitandao mikubwa wana moles ktk serikali hivyo wakiona hawa jamaa wanawatoa sokoni, wataingilia na TCRA watakuja na kale kamsemo ka ku-promote a level playing field to all competitors!

Mkuu hawa Halotel ni matapeli tuu hata siku moja haiwezkani wakaja bei chini kamavile wapo huko kwao Vietnam.

Hawa Halotel hatasiku moja hawatoweza kushindana na big3(voda,airtel,tigo).
ukizingatia mishaara yao ipo chini sababu ya cheap working force..

Msijipe matumaini hewa..
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

ndugu hawa watu sio wa kawaida..niko Kalambo mpaka wa zambia wana hadi ofisi..tumezoea mitandao mingine ikianza huanza ktk majiji na kusambaa polepole mikoan..ila hawa wanaanza huduma nchi nzima kwa pamoja hadi vijijin
 
Mkuu hawa Halotel ni matapeli tuu hata siku moja haiwezkani wakaja bei chini kamavile wapo huko kwao Vietnam.

Hawa Halotel hatasiku moja hawatoweza kushindana na big3(voda,airtel,tigo).
ukizingatia mishaara yao ipo chini sababu ya cheap working force..

Msijipe matumaini hewa..

usifanye hitimisho la kusema matapeli je wamekutapeli? Sioni utapeli wowote hapo coz currently natumia line yao na huduma zao zipo vizuri tu mkuu
 
Hata kama watauza lain yao laki nachukua tu maana nimechoshwa na haya mavoda kila kukicha manyanyaso yanazd hebu angalia 500/= 1mb,40sms,14min in24hrs ivi wanafkili tunakipato gan? Yaan nayatumia tu maan sna chakufanya na wasiliano kwangu ni ya mhim yaan haya ndo maccm tu hakuna tofauti
 
Mitambo ipo on kwaiyo ili kujua kama wapo fanya manual seach ya operators eneo ulilopo utawaona wanatumia jina Hit TZ.
View attachment 297332View attachment 297332
LAKN pia huko Zanzibar ulishaona wanachimba mitaro na kutandaza nyaya? Maana huku bara wametandaza nyaya karibu nchi nzima.

Mtandao wao una nyaya Inapita ardhini, huwezi ona minara mingi, wana minara michache alafu mirefu sana ile myembamba. Sehemu nyingine wamenyanyua juu nguzo kama za ttcl.

Hao ndio halotel wengine tushaanza watumia kama freelancer

wewe wanaotandaza nyaya sio huo mtandao wenu mpya WA halotel hao ni ttcl (mkongo WA taifa)
 
sifa kubwa ya huu mtandao ni 3g tz nzima safiri na gari toka dar mpaka mwanza ni full 3g. natumia mtandao wao leo wiki mbili ni full speed. movie ya mb 550 unashusha kwa chini ya dkk kumi. ni kqmpuni ya jeshi la vietnam.
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

Mkuu, hawa wavietinam wamejipanga hasa, minara na mitambo yao walishapeleka vijijini siku nyingi, tatizo lao ni kwenye mishahara ya wafanyakazi wao, ni shida yaani
 
kabla ya kusifia huo mtandao inakubidi ujiulize swali hili!

je, huo mtandao utaendeshwa kwa sheria na taratibu za nchi gani?
-maana kama na Tz Kampuni pekee inayoweza kutoa huduma kwa bei nafuu ni ile iliyo chini ya serikali (TTCL) haya mengine hawawezi kwani kufanya hivyo itakuwa hasara kwao.

Ila nilisikia nyepesi nyepesi kwamba hii kampuni inaendeshwa na jeshi la Vietnam, sijui ni kweli? Naomba mwenye kujua anijuze, manake kama kweli inaendeshwa na jeshi la Vietnam napata wasiwasi kidogo
 
Kuungia kwny competition ya biashara ya huduma za simu kwa sasa unabidi uje na unique product, unless ushindani ni mkubwq sana, yako wapi makampuni km Sasatel, Smart na hatq Zantel....hawa Vietel labda waje na huduma nzuri za internet zenye bei ndogo sana na zinazopatikana kila pembe ya nchi!

Unless hizi kampuni zilizopo huduma zao ni ghari sana...!
 
Wanatuua na minara yao isiyo na mpangilio, inatuletea cancer itakayotumaliza kwa kupenda rahisi##
 
Jamaa noma, jana nimetest line yao, nkatamani nivunje vunje line ya tigo, wako vizuri sana.. Hasa Internet full, Ukibonyeza hapo hapo kitu kinafungua
 
Cha muhimu uwe mtandao wa uhakika kama wanavyosema.

Hata wakiweka gharama kubwa na mtandao ni wa uhakika basi waje tu.

Ila wasiwasi wa TCRA kuwaachia hawa jamaa wafanye watakavyo.
 
Nime search by manual hakuna kitu kama hicho, huenda ni uzushi mtupu!
 
Back
Top Bottom