Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Nchi itabaki salama kweli? Jeshi la nchi nyingine kuendesha kampuni ya mawasiliano ndani ya nchi nyingine

mkwere alitukuta tukiwa tumevaa nguo, leo anatuacha uchi.
 
hawa jamaa tatizo lao kubwa ni kuweka internet ya 2g vijijini hivyo czan kama watateka soko kwani kwa kuweka 2g netwek vjijin kutafanya watu wengi wasivutiwe mtandao huu

Kuna sehemu nimesoma wanasema hawa jamaa wameweka 3G nchi nzima.
 
Kwa mjini watateka soko km watakuwa na bei nzuri kulinganisha na makampuni mengine

Mijini masoko yameshakuwa saturated sana.

Hadi sasa watumiaji wa mitandao ya simu wapo mijini kuliko vijijini.

Kama airtel walivyopata wateja wengi vijijini.
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?
Awa jamaa minara yao wameijenga sana vijijin mm nilikua kiteto yana kule ambapo hakuna mawasiliano wao ndo wameweka minara yao
 
Wakizindua line zangu zote ntazitupa huko wameshatuibia sana.
Mwaka huu ni mwaka wa mabadliko
 
Kesho,nanunua line ya Halotel rasmi naachana na line zingine,
 
Dah!! Naona hizi kozi; persuasion, sales & marketing ulizifaulu vizuri sana!!!
Kama unayosema ni kweli, basi nitakuunga mkono!!!:A S angry::mad2::cheer2:
 
Naona mawakala mmejifungulia uzi wenu....
Sasa hv kukiwa na wateja wachache just enjoy to the fullest but after muda watarudi huku huku.
 
Dah juzi nilikuwa na rafiki wangu pande za Namtumbo tukaliona bango lao,tukawa tunajiuliza halotel ni kampuni gani?Kumbe ni kampuni ya simu,karibuni sana,ila mjue watu wanataka mabadiliko kwenye gharama za mitandao.
Haiwezekani ninunue kifurushi cha 1500 then nipewe 50-70Mb.
 
Last edited by a moderator:
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

wanatumia cable. Wamesambaza cable karibu nchi nzima - mijini na vijijini. Je bei za simu zao itakuwaje? Hata mimi nawasubiria
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

Mkuu huo mtandao si mchezo juzikat nilienda boda Rusumo kupitia Dodoma Singida Tabora Kahama Geita adi Kagera Ngara Rusomo halotel wapo. sehemu nyingine mapori ya hatari nakuta halotel wamefika wamesimamisha nguzo na minara yao hawa jamaa ni balaa. naskia wakipita sehem wakikuta network yao iko 3G tu wanawela kambi adi ifike 4G hawa jama hawataki mchezo.
 
Back
Top Bottom