Tujadili kuhusu matuta barabarani

Kwa jinsi ya uendeshaji wa magari wa Tanzania ulivyo mimi naona hayo matuta yaliyopo hayatoshi kabisa.

Ingekuwa juu yangu ningeweka matuta kwenye barabara kila baada mita moja ili kutia watu akili.

Upo sahihi kabisa mkuu, lakini shida ni pale viwango vya hayo matuta vinavyotofautiana...

Kuna aina fulani za matuta ni kama zinaharibu magari tu, yaani yainuka ghafla na ni marefu kwa kimo...

Kwa watu wenye kutumia magari madogo basi huwa wanapata tabu na baadhi ya parts za chini hukwanguliwa...
 
aisee umepoteaje ? nasikia huko mo town kumegeuga uwanja wa tigo ...wachaga wanakula tigo balaa kwa mabeki 3 wao....hebu nirushie hiyo cd nione maana siamini mie

nipo my dear, na mie nimefanya kusikia sikia tu juu juu, weekend hii ntapata full picture, kaa mkao wa kunyumba.
 

mkuu Nyani Ngabu nashukuru kwa mchango wako hapa.....umeshayaona aina ya matuta wanayoweka lakini?

BAsi tufike mahali, tutembee tu kwa miguu.....
 
Last edited by a moderator:
Shikamoo shemeji.Siku hizi una maswali magumu kweli.Ni kwa vile serikali imeshindwa kusimamia taratibu na sheria ilizojiwekea ndio maana inaingia gharama zaidi kujaribu kutafuta usalama wa barabarani.Ni bora hayo matuta yaongezeke mpka hapo tutakapopata akili nzuri.
 
Lakini kwanini uvunje sheria?

sawa huwa navunja sheria coz nikiona hilo tuta hapo mbele yangu naona otee kabisa, lakini sijawahi kukamatwa kwa kuvunja sheria, nakamatwa na mambo yasiyoeleweka kabisa, ndio mana nikasema kuna wakati nagoma kuwapa chochote kabisa wataning'ang'ania, kuna siku wamenishindisha kituoni coz nilikataa/niligoma kuwapa kitu kidogo, kuna wanawake wawili wananichukia kabisaaa coz hao ndio niliowagomea kuwapa kitu kidogo so siku hizi nikikutana nao popote ni malumbano tu, watanitafutia sababu tu, siku nikiwa na haraka zangu inabidi niwape niendelee na safari, "nchi ya kitu kidogo"
 

mkuu I like your line of thinking kuhusu Highway...kumbe huku hakuna highway kabisa sio....
 

Asee Zion Daughter.....apo umeongea kwamba wote hatuna akili nzuri eee? duh

Yaani kimsingi ni kwmaba sheria na hali halisi vitu viwili tofauti!
 
Last edited by a moderator:
mkuu Nyani Ngabu nashukuru kwa mchango wako hapa.....umeshayaona aina ya matuta wanayoweka lakini?

BAsi tufike mahali, tutembee tu kwa miguu.....

Nimeshayaona ndiyo.

Na mimi binafsi ni mwoga sana wa kuendesha gari Dar. Ni kero na hatari tupu. Si bodaboda, si bajaji, si vipanya, si vi coaster, si mikokoteni...ni hatari mwanzo mwisho.

Nikiendeshaga gari Dar, tuseme natoka nyumbani kwenda mjini nikirudi nyumbani bila kupatwa na road rage ntashangaa sana.

Yaani huwa ni lazima nimpe mtu finger na lazima nitukanwe na lijitu jingine ambalo halijui kuendesha kwa usalama na kistaarabu.

Unakutana na jitu linaendesha wrong way halafu ukilipigia honi eti wewe ndo unaishia kutukanwa. Gademu it.
 
mkuu I like your line of thinking kuhusu Highway...kumbe huku hakuna highway kabisa sio....

kwa maoni yangu...this is a HIGHWAY....huwa haina na haiwekwi matuta.....hapo kwenye fensi ya mbao kuna access wamezuia pedestrian wasikatize ingawa sheria ipo kwazuia ila usipodhibiti wanakula short cut

 
hahaah Kipaji Halisi unamaanisha nje ya nchi? kama nje ya nchi sawa hawana hii makitu bana,,,kule ni sheria mtindo mmoja na watu wako conscious, huku majanga

kama ni hapa mitaa ya bongo utakuwa umeona hii
hivi anko@Kaizer unaweza kupita road zetu bila kukutana na matuta km si nje?...hii kitu uliyoweka ina wahusu KakaKiiza na Asprini...hahahahahahahahaha
 
Last edited by a moderator:
kwa maoni yangu...this is a HIGHWAY....huwa haina na haiwekwi matuta.....


Bongo hakuna highways za maana.

Kwa wenzetu kuna hadi mi freeways, expressways, interstates yenye lanes hadi kumi!



Halafu cheki hiyo concrete median. Kwa maoni yangu husaidia sana kupunguza head-on collisions.

 
hahahahaha..mkuu hii kitu huwa nashangaa sana..mfano uliotoa ni wa ukweli sana...unafika zebra dereva ndio kwanza anaongeza mwendo....halfu huyo derva kumbuka ana leseni ujue..
 
Bongo hakuna highways za maana.

Kwa wenzetu kuna hadi mi freeways, expressways, interstates yenye lanes hadi kumi!



Halafu cheki hiyo concrete median. Kwa maoni yangu husaidia sana kupunguza head-on collisions.


huku mbali sana kaka....hata DUAL CARRIAGEWAY ingetosha.....halafu ikipita around built up area inawekewa fence...strictly no pedestrian....sasa single lane track inapita katikati ya kijiji/shule bila matuta si mnataka wanakijiji/wanafunzi wateketee.
 
Achia mbali kuharibu magari...kutingishwa ndo usiseme hasa kwa kinamama!!

Yani wameweka matuta kama vile wote watumiao muundo mbinu huo wana cruza tu kumbe kuna na Vitz!!
Sioni umuhimu wa kuweka matuta kwenye highways,dereva akiona kibao cha mwendo kasi chini ya km 50 anaelewa kabisa anatakiwa apunguze mwendo na ndo mana dereva anatakiwa awe zimetimia kichwani.
 
Mi nafurahi kwamba TBS sasa wako mbioni kuja na stanfards za matuta..kwamba yawe aina gani hasa...tunacholalamika ni kwamba hakuna kabisa standards kwenye hii kitu

Haya mambo lazima yawepo kisheria haki na wajibu wa kila.mmoja vianishwe
Chocs naomba kutambua mchango wako
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…