TUJADILI: Kati ya Baba na Mama nani ni muharibifu?

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,463
Habarani marafiki wote

Nimeleta mada hii hapa tujadili kwa pamoja na sio kujoke
Kati ya Baba na Mama nani ni muanzilishi wa kumharibu mtoto
kimaadili na kumfanya mtoto awe mento na kudata kupitiliza?

Nani ampaye vitu (simu, tablet n.k) hatarishi mtoto na kufanya akengeuke na
kuiacha njia sahihi ya maadili mema

Marafiki hebu tujadili kidogo hapa nini kifanyike ili mtoto aweze kurudi katika
nafasi yake kama mtoto kwani siku hizi maadili yameporoka na vijana wengi
wamekengeuka wazazi wanalia kila iitwapo leo. Toa ushauri mzuri nini kifanyike
hapa nchini kwetu na ulimwengu mzima.

Karibuni mabestitooo
 
Both,ila kila mmoja kwa namna yake,
muda mwingine unakuta baba anasema"mwacheni jembe langu,hasa kwa mtoto wa kiume"
mama nae mwacheni mrembo wangu nshamnunulia bunduki mijianaume inavyomtolea macho"
kwa ufupi kutengeneza njia nzuri ya mtoto inabidi kuwe na mawasiliano mazuri kwa wazazi wote wawili,
 
Cha msingi ni apatkane dikteta aseme hakuna kutumia internet yyte...mizki icyo n maadili ifungiwe..nnchi nzma madela n kanzu tu
 
Habarani marafiki wote

Nimeleta mada hii hapa tujadili kwa pamoja na sio kujoke
Kati ya Baba na Mama nani ni muanzilishi wa kumharibu mtoto
kimaadili na kumfanya mtoto awe mento na kudata kupitiliza?

Nani ampaye vitu (simu, tablet n.k) hatarishi mtoto na kufanya akengeuke na
kuiacha njia sahihi ya maadili mema

Marafiki hebu tujadili kidogo hapa nini kifanyike ili mtoto aweze kurudi katika
nafasi yake kama mtoto kwani siku hizi maadili yameporoka na vijana wengi
wamekengeuka wazazi wanalia kila iitwapo leo. Toa ushauri mzuri nini kifanyike
hapa nchini kwetu na ulimwengu mzima.

Karibuni mabestitooo

Jukumu la kwanza kabisa la mwanamke alilopewa ni kumpenda na kumweshimu mume wake, kukaa kwa maarifa na utakatifu na kutunza boma (Tito 2:4-5). Wanawake kwa maumbile jukumu lao ni kutunza kuliko wanaume kwa sababu wamepangiwa kuwa walinzi wa watoto wao.

Jadiliana nao ulimwengu unaowazunguka vile wanavyouona, na wafunze kuhusu utukufu wa Mungu kila siku. "Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee" (Methali 22:6).
 
Inategemea kwa kweli,kuna family mama akimkemea mtoto basi baba akijua ni shida!
Kuna ambazo mama akisema hata baba hapingi!!
Cha kufanya nadhani ni wazazi wote wawili kuwa na msimamo mmoja juu ya malezi ya watoto,wawe huru kiasi gani na kipi hawaruhusiwi kufanya. Mzazi yeyote awe huru kukemea mtoto anapokosea na mwenza am support au akae kimya na kama ana maoni tofauti basi amsubiri mwenzie chumbani wakaelekezane mbali na masikio ya watoto.Hii itafanya mtoto ajue akiharibu kwa mama basi baba akija atamuongezea adhabu.
Kitu kingine kinachopaswa kukemewa ni mtoto kunyenyekewa kisa tu amepewa jina la bibi/babu,mzazi anamuogopa mtoto wake kisa tu ni baba/mama/mkwe!!!
Mtoto apewe jina kama wazazi wataamua hivyo ila abaki kuwa mtoto bila kuogopa ukubwa wa jina lake!
 
hapo kwenye kupewa jina nakumbuka mamayangu alikuwa akisema msiwape watoto wenu jina langu maana najua mtakuwa mnanitukana kila siku.

lakini la muhimu ni hilo la wazazi kuwa na msimamo kwa pamoja
 
Habarani marafiki wote

Nimeleta mada hii hapa tujadili kwa pamoja na sio kujoke
Kati ya Baba na Mama nani ni muanzilishi wa kumharibu mtoto
kimaadili na kumfanya mtoto awe mento na kudata kupitiliza?

Nani ampaye vitu (simu, tablet n.k) hatarishi mtoto na kufanya akengeuke na
kuiacha njia sahihi ya maadili mema

Marafiki hebu tujadili kidogo hapa nini kifanyike ili mtoto aweze kurudi katika
nafasi yake kama mtoto kwani siku hizi maadili yameporoka na vijana wengi
wamekengeuka wazazi wanalia kila iitwapo leo. Toa ushauri mzuri nini kifanyike
hapa nchini kwetu na ulimwengu mzima.

Karibuni mabestitooo

% mia moja ni mama' 7bu zpo nying - mama anamda mwing xna na mtoto' pli mama bora ndio anatengeneza familia boraa
 
Inategemea ka mie babaangu alindekeza na alikua tayar kumpa bakora mama kisa mm...bt mamaang alikua mkali sanaa
 
ni kweli bila ya kuwa na mawasiliano mzuri kati ya wenza hawa yaani wazazi hakutakuwa na suluhu ya kumlea mtoto katika maadili mema
Both,ila kila mmoja kwa namna yake,
muda mwingine unakuta baba anasema"mwacheni jembe langu,hasa kwa mtoto wa kiume"
mama nae mwacheni mrembo wangu nshamnunulia bunduki mijianaume inavyomtolea macho"
kwa ufupi kutengeneza njia nzuri ya mtoto inabidi kuwe na mawasiliano mazuri kwa wazazi wote wawili,
 
Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana m.pumbavu ni mzigo wa mamaye.
 
Home kwetu baba na mama wote wana sauti moja, ukikosa wanakuchapa wote, wote wanaamua hakuna kuangalia TV.

Kila kitu ni "collective decision making"

Kwahyo kama kutuharibu au kutujenga wote wamechangia.

Kwa familia nyingine inategemea mtoto ameelemea upande gani, kuna watoto wa mama na watoto wa baba.
 
Washauri watani wa jadi wenzako waache ule mchezo wa kuona mtoto anakengeuka badala yakuchukua hatua mara moja kumrekebisha wanaishia kumwambia baba akirudi nitakushitaki.
 
Back
Top Bottom