Nani ana unafuu kati ya msichana na mvulana wanapofikia balekhe?

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
686
1,360
Habari wanajamii,

Katika mazingira ya sasa ya malezi na makuzi huwa najiuliza sana hivi ni nani anapitia changamoto nyingi kati ya msichana na mvulana hasa wanapofika kipindi cha kubalehe hadi ukubwani kutokana na kuwepo na mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu hasa maeneo ya mijini?

Mimi ni mwanaume, japo nimezaliwa miaka ya 90's lakini wakati nakua hadi kujitambua ilikuwa nadra sana kuona sehemu za siri za mwanamke na mambo ya ushawishi. Watu walionizunguka hasa upande wa KE walikuwa watu wenye aibu na woga na kujiheshimu, hii ilinifanya kupotezea mambo mengi yanayohusu kujamiiana.

Sasa kwa wakati tulionao, kuzuka kwa mitandao ya kijamii pamoja na simu janja kumefanya watu kuhamisha maisha ya mitandaoni kuyaleta katika jamii, yaani kuvaa tight na t-shirt kama wa kwenye video za miziki, kujiuza hadharani kama watu wa majuu, kutomasana na kubusiana hadharani n.k kumekuwa kawaida sana.

Kwangu mimi nisiokulia katika mazingira haya nikilinganisha na nyuma naona ajabu sana na ni changamoto, naweza mtizama mwanamke alivyovaa nusu uchi si kwa kumtamani bali kwa kusikitika kwanini jamii imefika huku na nini cha kufanya, binafsi sipati majibu.

Lakini pia hali hii inaongeza ushawishi katika matamanio ya nafsi najikaza lakini kuna siku nateleza ni changamoto sana.

Sasa huwa najiuliza kwa wadada either wanaovaa hivyo au wasiovaa nusu uchi kwao changamoto hizi huwa hawazioni? Na je, kwa upande wao ni changamoto gani za kiushawishi wanaziona kwa wanaume au vijana ambazo zinawafanya wafanye ayo?

Na je kwa vijana wanaochipukia hii hali wanawezaje kuikabili ili waweze kuishi katika misingi ya maadili huku wanaowazunguka wapo kwenye dimbwi la mmomonyoko? Na nini kifanyike kwa wale tusiomudu mikikimikiki ya mmomonyoko huu?

Nawasilisha.
 
Kuna siku nimemkuta dogo anamsulubu mbwa jike🤔,

Nikawaza sasa huyu dogo hawezi pata magonjwa? Nimewaambia wazaz wake wakampime na kichapo juu.
 
Wanawake wanajiachia sana wanapoteza vijana wa kiume kwa mavazi yao
 
Back
Top Bottom