Tujadili juu ya ubaguzi

Gelion Kayombo

Senior Member
Feb 17, 2018
149
193
Hebu tuzungumze leo juu ya ubaguzi. Mara nyingi huwa tunasikia na kuangalia kwenye vyombo vya habari juu ya ubaguzi dhidi ya watu wengine. Mara nyingi habari zinazosikika zaidi ni kwamba watu wenye ngozi nyeupe(wazungu), wanawabagua watu wa rangi(weusi). Utasikia watu waishio nje ya bara la Afrika na ndani ya bara la Afrika hasa kama umeajiriwa na watu weupe wanalalamika kwamba washawahi kubaguliwa kwa mwonekano wao, rangi, umbo na katika kazi.

Hata hivyo habari za ubaguzi huwa zinasikika sana kama mtu au watu mashuhuri wamepatwa na kadhia hii hasa, wanamichezo wa kandanda wenye rangi, wanaochezea vilabu vya nje ya bara la Afrika. Mara nyingine utasikia wananchi waishio ndani ya nchi (ambao wamewahi kufanya kazi na watu weupe) wanalalamika juu ya kubaguliwa kwa namna moja au nyingine.

Lakini mimi nataka kujua, hivi ni kweli watu wenye ngozi nyeupe pekee ndio wanaowabagua watu wenye rangi nyeusi?. Kama ni ndiyo, je, sisi watu wenye rangi huwa hatubaguani sisi kwa sisi kwa namna moja au nyingine? Kwa maana utaona mtu mwenye rangi anamtukana mwenye rangi mwenzie kwamba ni mweusi sana, au mweupe sana, mfupi sana au mrefu sana. Vivi hivyo na kwenye kazi utaona watu wa rangi wanabaguana.

Je, wewe ushawahi kubaguliwa na Mwafrika mwenzako kwa namna moja au nyingine iwe ni kwa mwonekano wako, rangi yako, umbo lako na hata katika kazi?. Kama ni ndiyo je, huo siyo ubaguzi?. Au ubaguzi ni pale tu ukifanywa na watu weupe(wazungu) kwa mtu mwenye rangi? Na vipi kama Mzungu akimbagua Mzungu mwenzie au Mwafrika akimbagua Mwafrika mwenzie, hapo utakuwa ubaguzi au kuna neno jingine la kutumia?.

Karibuni kwa mjadala.
 
Ubaguzi upo kwenye kila kona ya maisha ya binadamu labda uwe specific kwenye ubaguzi wa nini.
Inashangaza sana kama hujaona ubaguzi wowote ule.
 
Ubaguzi upo sana na ni Mpana sana, hata kwetu sisi Weusi tunabaguana, nitakupa mifano miwili bila kutaja majina ya sehemu husika.

Nilienda kwenye moja ya hoteli za Kifahari jiji Dar kwa ajili ya ku confirm chumba nilichobook week moja nyuma, nakumbuka hiyo siku ilikuwa jumamosi nilikuwa nimejivalia kawaida tu, nikimaanisha sikuwa smart, lakini hii haikunizuia kuingia kwenye hiyo hoteli.

Nikafika mapokezi nikaunga mstari kama wengine niliowakuta....nakumbuka mbele yangu kulikuwa na wazungu na pia nyuma yangu kulikuwa na wazungu, ilipofika zamu yangu, yule muhudumu alimwita mzungu aliyekuwa nyuma yangu na kuniacha mimi, sikufanya lolote, nilijua labda alikuwepo kabla yangu.

Alipomaliza nikaona amemwita tena mzungu mwingine aliyekuwa nyuma yangu, hapo sikuweza kuvumilia nikaingilia kati. Cha kushangaza sikuambiwa sababu na wala hawakuona kama nahitaji kuombwa radhi.

Nilimaliza kilichonileta pale, nikaomba kuonana na Mkuu wao wa kazi, ambaye ni mtu ninaye fahamiana maana huwa naitumia sana hiyo hoteli. Issue tukaimaliza kiungwana ila nilijisikia vibaya sana kubaguliwa nikiwa ndani ya Nchi yangu tena na Mweusi mwenzangu, kisa ameona Wazungu.

Kisa cha pili, ni katika Hospitali moja kubwa tu Jiji Dar, nilikuwa na mgonjwa wangu pale.
Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nikawa nashindwa kuwahi muda uliopangwa wa kuona wagonjwa, nikawa na chelewa, lakini naongea namlinzi ananielewa napita....

Sasa akabadilishwa mlinzi, siku hiyo nafika akanikatalia kabisa, nikaaa nje nafikiria cha kufanya, Mara wakaja Wazungu wakaongea nikaona wameingizwa, nikajua wanaweza kuwa m Dr, mda si mrefu wakaja Wahindi nao wakaingizwa, hapo sasa nilipoona yamefikia huko, kilichoendelea ni siri yangu...

Ubaguzi wa sisi weusi kwa weusi upo na unaumiza sana.
 
Ubaguzi upo sana
Baada ya kushinda WC France
Na mengine kuhusu sisi kwa sisi ntaliandika baadae.

IMG-20180719-WA0014.jpeg
 
Hebu tuzungumze leo juu ya ubaguzi. Mara nyingi huwa tunasikia na kuangalia kwenye vyombo vya habari juu ya ubaguzi dhidi ya watu wengine. Mara nyingi habari zinazosikika zaidi ni kwamba watu wenye ngozi nyeupe(wazungu), wanawabagua watu wa rangi(weusi). Utasikia watu waishio nje ya bara la Afrika na ndani ya bara la Afrika hasa kama umeajiriwa na watu weupe wanalalamika kwamba washawahi kubaguliwa kwa mwonekano wao, rangi, umbo na katika kazi.

Hata hivyo habari za ubaguzi huwa zinasikika sana kama mtu au watu mashuhuri wamepatwa na kadhia hii hasa, wanamichezo wa kandanda wenye rangi, wanaochezea vilabu vya nje ya bara la Afrika. Mara nyingine utasikia wananchi waishio ndani ya nchi (ambao wamewahi kufanya kazi na watu weupe) wanalalamika juu ya kubaguliwa kwa namna moja au nyingine.

Lakini mimi nataka kujua, hivi ni kweli watu wenye ngozi nyeupe pekee ndio wanaowabagua watu wenye rangi nyeusi?. Kama ni ndiyo, je, sisi watu wenye rangi huwa hatubaguani sisi kwa sisi kwa namna moja au nyingine?. Kwa maana utaona mtu mwenye rangi anamtukana mwenye rangi mwenzie kwamba ni mweusi sana, au mweupe sana, mfupi sana au mrefu sana. Vivi hivyo na kwenye kazi utaona watu wa rangi wanabaguana.

Je, wewe ushawahi kubaguliwa na Mwafrika mwenzako kwa namna moja au nyingine iwe ni kwa mwonekano wako, rangi yako, umbo lako na hata katika kazi?. Kama ni ndiyo je, huo siyo ubaguzi?. Au ubaguzi ni pale tu ukifanywa na watu weupe( wazungu) kwa mtu mwenye rangi?. Na vipi kama Mzungu akimbagua Mzungu mwenzie au Mwafrika akimbagua Mwafrika mwenzie, hapo utakuwa ubaguzi au kuna neno jingine la kutumia?.

Karibuni kwa mjadala.
 
Wasukuma wanawaozesha mabinti weupe kwa mahari kubwa kuliko weusi sasa huu kama si ubaguzi ninini.

Msiba wa fukara wakishazika tu watu wanajiondokea lkn kwa tajiri wanakaa hata wiki mbili huu si ubaguzi pia.
Hata wazungu wanabaguana huko kwao.

Binadamu ni mbaguzi tu naturally.
 
Hizi ni mila unajua sababu ya mweupe kutolewa mahari kubwa?
 
Tatizo waafrika unafki umetuzidi. Ubaguzi upo kati ya sisi kwa sisi.

Na mimi naombea hao wazungu na other light skinned races wazidi kutubagua zaidi na zaidi hadi tutakapojitambua.
 
Back
Top Bottom