Tujadili elimu ya Mnyika au wanafunzi 240,903 kupata sifuri?

Kutakuwa na hujuma sehemu. Binafsi siamini kuwa kweli kuna div 0 zaidi ya laki 2. Hiyo mitihani irudiwe tena kusahihishwa na taasisi makini. Tatizo jingine ni walimu waliopo. Licha ya kutopata maslahi mwafaka, hawa walimu wengi wao ni 'vihiyo'. voda fasta. wanafunzi wanafundishwa kujibu maswali badala ya kujua somo linataka nini. Hao wanaosahihisha wenyewe ni vihiyo. hawana marking scheme. Hawana maadili. Nasema pamoja na hao wanafunzi kuwa na nafasi yao katika kufeli, wamefelishwa pia. Mitihani irudiwe kusahihishwa.
 
nilikuwa namaanisha umekuwa critic kwa wana jf so watakuwa offensive kwako ingawa ulichoandika ni kina mantiki.

Oh yea, WanaJF hawatakiwi kuwa criticised kwa kujadili hoja za kipuuzi, kijinga na za kipumbavu?

Naomba niazime maneno ya Magembe R. Malima "Huenda nikakuweka katika presha zaidi kwa kukujibu sasa hivi na labda kwa namna hii. Ah, ndiyo ukubwa huo. Najibu: Ni sawa na wale wapiga violin katika filamu ya Titanic wakati inazama, wanapiga kutuliza watu lakini watu wanawakimbia na wao pia wanakimbia kwa kuwa muziki ule hauonekani kuwa na mashiko dhidi ya hatari DHAHIRI KABISA INAYOWANYEMELEA"

Kwa nini MwanaJF atumike kujadili hoja za kipuuzi, kijinga na za kipumbavu kuhusu elimu ya Mnyika na kuacha kujadili hoja za msingi kama watahiniwa 240,903 kupata sifuri simply because hoja hiyo ya kipuuzi, kijinga na ya kipumbavu imetolewa na mwanasiasa?

Heshimu utu wako kwanza.
 
Wabunge wa CCM walimzomea mh. Mbatia alipohoji kuhusu mitaala ya shule zetu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
tutajadili vyote !ila tutajadili kwa undani zaidi juu ya kufeli kwa vijana wetu hasa waliosoma katika shule zinazotambulika kama mitambo ya kufyatua mayai.
 
Kutakuwa na hujuma sehemu. Binafsi siamini kuwa kweli kuna div 0 zaidi ya laki 2. Hiyo mitihani irudiwe tena kusahihishwa na taasisi makini. Tatizo jingine ni walimu waliopo. Licha ya kutopata maslahi mwafaka, hawa walimu wengi wao ni 'vihiyo'. voda fasta. wanafunzi wanafundishwa kujibu maswali badala ya kujua somo linataka nini. Hao wanaosahihisha wenyewe ni vihiyo. hawana marking scheme. Hawana maadili. Nasema pamoja na hao wanafunzi kuwa na nafasi yao katika kufeli, wamefelishwa pia. Mitihani irudiwe kusahihishwa.
Tanzania ni nchi pekee isiyokua na mitaala ya kufundishia. Hata tukiwa na waalimu wenye G.P.A ya 5.0 hawataweza kufundisha vema watoto wetu kama serikali haitakuwa na mitaala yenye tija.
Unajua ni kwa nini mkurugenzi wa wizara ya elimu alijiuzulu mapema?
Tafathali waombe radhi walimu kwa maneno uliyoyatunga juu yao.
CCM ni mtambo wa kuzalisha mbumbumbu kwaajili ya mtaji wao wa kura.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
naunga mkono hoja CCM imegeuza shule zetu za elimu ya sekondari mitambo ya kufyatulia mayai, watoto wamekunya eggs balaa, kusubiri mpaka 2015 ndo tuwapige chini hawa magamba tutakuwa tumetengeneza wajinga takribani milioni moja na mamia kadhaa, we need to hijack this train and take it into the right direction.
 
mkuu umekuwa critic
sana unaweza kupata resistance kidogo, ila hayo mbatia alishawaeleza
wakamuona mpuuzi, ile wizara inaongozwa na mawaziri wajinga kabisa
kuwahi kuingia katika baraza la mawaziri toka uwepo wa
ulimwengu.
Na aliyewateua na hajawaondoa?
 
I totally agree with you. Unajua hii hoja ya elimu ya Mnyika imeletwa makusudi na adui zake wa kisiasa hasa Nape na hao masalia. Kimsingi hii ni hoja dhaifa ambayo haina hata mshiko kwa sababu hata kama hajamaliza elimu yake ya chuo kikuu the guy is doing good job, na inaonekana kuliko hicho kinachofanywa na masalia. Tujiulize tu kwa nini suala la Mnyika kutokumaliza chuo kikuu (if at all it is true) limekuwa hoja wakati ukiingia tovuti ya Bunge asilimia kubwa ya wabunge ni form four na certificate? kwa umri wa wabunge hao utaona kuwa zamani ilikuwa ukipata division ya chini ilikuwa vigumu kuendelea kusoma. Maana yake ni kuwa Wabunge wengi wa CCM ni failures wa wakati ule. Why then Mnyika ambaye anafanya vyema kuliko hao wanaosinzia hovyo. Bahati mbaya sana bado wananchi wetu wanaendelea kushabikia vitu vya kipuuzi. Hivi kweli tunaweza kuendelea kama tunaweza kurubuniwa na watu wenye uelewa mdogo hivi kuamini wanachotaka ili kutimiza ndoto zao za kumuodoa Mnyika jimbo la Ubungo. Matokeo yake sasa ni haya kuacha kuongelea hoja za masingi za mustakabli wa elimu ya watoto wetu na wadogo zetu na kuaza kuvutwa kushabikia maslahi ya watu wachache wasiokuwa na nia njema kwako wewe Mtazania. Mbatia alitoa hoja nzuri tu kuwa elimu ya Tanzania haina miongozo/mitaala wengi tukapelekwa kuamini Mbatia ni mwongo sasa matokeo yake ndiyo haya. Ukweli ni kwamba ni aibu kwa Waziri wa Elimu kuendelea kuwepo Madarakani hadi sasa. Hapo ndipo utaona viongozi wetu hawapo kwa ajili ya wananchi bali kwa manufaa yao binafsi.
Nimesikitishwa sana kuona Watanzania wengi wamechotwa kirahisi mno na wanaojiita wanasiasa kujadili elimu ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika. Ukiangalia hapa JF, kule Facebook, Twitter na hata kwenye baadhi ya vyombo vingine vya habari Watanzania eti kutwa nzima wanajadili elimu ya Mnyika.

Yaani unamkuta mtu eti yuko bize kwenye keyboard akiandika juu ya elimu ya Mnyika, lakini hajiulizi kabisa ni kwa nini kati ya watahiniwa 480,036, waliosoma miaka minne 240,903 wamepata sifuri. Tunaona kujadili elimu ya Mnyika, mbunge bora kwa mwaka 2012, ni dili zaidi kuliko wanafunzi 240,903 waliotaga mayai leo.

Tuache kutumiwa kama wapuuzi, wapumbavu na wajinga wa kutupwa kujadili mambo ya kipuuzi, kijinga na ya kipumbavu. The more you entertain hizo hoja za kipuuzi, kijinga na kipumbavu, the more you keep them coming. Kilichotakiwa kujadiliwa siyo elimu ya Mnyika bali ni matokeo mabaya ya Kidato cha Nne. Waliopata Division One: 1,641; Division Two: 6,453; Division Three: 15,426; Division Four: 103,327; na Division Zero: 240,903. Hapa ndipo Mtanzania yoyote mwenye akili timamu anatakiwa kuhoji.

Kujadili elimu ya Mnyika ni kuwafanya Watanzania kutojadili na kuhoji matokeo mabaya sana ya Kidato cha Nne. Hili limefanywa kwa makusudi kabisa ili kupotezea kuhoji matokeo mabaya ya Kidato cha Nne. Kuna watu humu siku nzima wamejikita kujadili elimu ya Mnyika, lakini wana ndugu, jamaa na marafikri ambao leo wametaga mayai baada ya kusoma kwa muda wa miaka minne.

Narudia tena: Acheni kutumiwa kama kondomu. Bahati mbaya tunatumia Kiswahili kuficha upuuzi, ujinga na upumbavu wetu ili watu wa mataifa mengine wasisome upumbavu tunaojadii kila kukicha huku tukiongozwa na wanaojiita wanasiasa.
 
Mtaji wa CCM, ni UMASIKINI NA UJINGA wa Watanzania, sishangai kuona wanafunzi wamefeli kiasi hiki...kwa sababu CCM wanafurahi kwa kupata mtaji wa kura...
 
Yaani waliotaga na kuzungusha ni 60%
Maisha bora kwa kila mtanzania.
Bongo tambarare
Mambo yote bongo
 
Na hili ndo tatizo la baadhi ya wanasiasa wanakaa kujadili opponents wao kisiasa badala ya kujadili masuala yanayoliathiri taifa kama mfumo wetu wa elimu na matatizo yake. Mnyika hapo alipo amesha-prove beyond reasonable doubts kwamba ameelimika bila kujali anavyeti vingapi. Matokeo ya form four ni aibu na waziri Kawambwa anahitajika kuwajibaka right away. Haiingii akilin watoto laki 200+ wanaziro halafu nchi ikae kimya.
 
QUOTE=FJM;5726076]
DIVION I
DIVISION II
DIVISION III
DIVISION IV
DIVISION 0

1,641

(0.45%)

6,453

(1.75%)
15,426
(4.19%)

103,327

(28.10%

240,903

(65.51%)

Nitashangaa sana kusikia bado Waziri, Naibu waziri wa Elimu na wakuregenzi wao wanapanda mashangingi kwenda ofisini! Baada ya kukaa darasani miaka 4, zaidi ya nusu ya watahiniwa wanapata division 0, hapo tunategemea taifa lisinge mbele?

Bado sijaona matokeo ya nchi nyingine ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini sidhani kama kuna scandal kubwa kama hii ya Tanzania. 65.51% ZERO?[/QUOTE]

FJM kwa hali halisi hata hao wa Div Four bado huwezi kusema kuwa amefaulu. Hapo ni kwamba ni vile tu ana uwezo wa kupata cheti na anaweza kwenda kusaka saka akasoma cheti kwenye vyuo vya chini mpaka aje afikie juu ila ni kuwa nao wamefeli kwa hali halisi. Hii ni hatari waziri bado yuko ofisini ilhali robo tatu ya wanafunzi wake wamefeli na hawana uwezo wa kwenda kidato cha sita.
Kwa wanafunzi 240 000 kufeli ni janga ambalo sijui waziri na serikali yake wanakuja na taarifa gani kutuambia. Hao watoto wataenda wapi waliopata zero ambao hawajui kesho na kesho kutwa watafanya nini maishani mwao. Wamepoteza miaka minne ya maisha yao na wametoka hawana kitu.

@
 
Last edited by a moderator:
Nimesikitika sana..kwa kweli kwa kutoa machozi!ile shule ya kata kule kijijini kwangu..ambapo wengi wa wanafunzi ni watoto wa ndugu,jamaa na marafiki haijafaulisha hata mmoja?!ndio shule ya kijijini kwangu,ambayo licha ya kuwa sikuwa mwalimu kitaaluma,lakini likizo zangu nimekuwa nikitumia kujitolea kuwafundisha..wote wameanguka!Inaniuma sana kwa vijana hawa..ambao hawakuwahi hata kutumia Laptop mpaka nilipoenda nayo!Taifa la majanga linakuja...serikali ijipange na ifanye kitu!watoto hawawezi kufaulu wakati hakuna vitabu,maabala ya shida na walimu hawana motisha..unategemea watoto wafaulu kwa mazingira haya?Walatin wanasema "Nemo dat quod non habet= No one gives what he doesnt have"....watafaulu vipi wakati hakuna walichopewa?......"Amat Victoria curam =Victory loves preparation"....Serikali iwaandae walimu ili watoto wapate ushindi!

Ahsante kwa comment zako mkuu. Umemsikia waziri anasema shule kadhaa zimekuwa za mwisho? Mi najiuliza kwa nini aseme ni za mwisho wakati ule ulikuwa mtihani na si mashindano? Pia kwa nini useme wamekuwa wa mwisho wakati vigezo vya hayo mashindano havilingani/havipo/havijawekwa!? Chukulia shule ya sekondari kata ya bagamoyo na Al Muntanzir au ile shule aliyosoma mtoto wa baba mwanaasha, hapa si tayari unajua ipi itakuwa ya mwisho? Mi napendekeza shule zinapofunguliwa tu watangaze hayo matokeo ya nani wa kwanza na nani wa mwisho kwa kuwa inajulikana kabla! kawa mbwa rejea usanii wako katika hoja ya mbatia uliyosaidiwa vya kutosha na thenkyu vere muuuuuuch!
 
QUOTE=FJM;5726076]
DIVION I
DIVISION II
DIVISION III
DIVISION IV
DIVISION 0
1,641

(0.45%)
6,453

(1.75%)
15,426

(4.19%)

103,327

(28.10%
240,903

(65.51%)


kwa hali halisi hata hao wa Div Four bado huwezi kusema kuwa amefaulu. Hapo ni kwamba ni vile tu ana uwezo wa kupata cheti na anaweza kwenda kusaka saka akasoma cheti kwenye vyuo vya chini mpaka aje afikie juu ila ni kuwa nao wamefeli kwa hali halisi. Hii ni hatari waziri bado yuko ofisini ilhali robo tatu ya wanafunzi wake wamefeli na hawana uwezo wa kwenda kidato cha sita.
Kwa wanafunzi 240 000 kufeli ni janga ambalo sijui waziri na serikali yake wanakuja na taarifa gani kutuambia. Hao watoto wataenda wapi waliopata zero ambao hawajui kesho na kesho kutwa watafanya nini maishani mwao. Wamepoteza miaka minne ya maisha yao na wametoka hawana kitu.

@

Ni kweli, Division IV nao wanaangukia kwenye kufeli and that makes matters much much worse. Kwa kifupi, 93.61% ya watahiniwa kidato cha 4 wamefeli! 93.61% !

Division hawifiki hata asilimia 1! Waziri na wakubwa wenziwe wa Wizara ya Elimu wanatakiwa waondoke - haraka. Na tukumbuke hii si mara ya kwanza, kila mwaka matokeo yanazidi kuwa mabaya na hawaonekani kuja na solution. Sasa kwanini wabaki?
 
Hivi Kawambwa na Mulugo(Zimbabwe plus one ninteen sixty four??) kuna la maana litafanyika?
 
Hakuna mchawi matokeo ya form four, Ni akili za serikali yenu hii kutatua migogoro. Walimu swala sio wingi wala nini swala ni moyo wa kujituma. Basi wafanye research shule zilizokuwa na walimu wa masomo fulani je watoto walifaulu hayo? Utakuja gundua kuwa wanafunzi wamefaulu masomo ambayo hawana hata walimu. Walimu madai yao yawekwe mezani yajadiliwe na walidhike na majibu. Madaktari nako ungekuwepo mtihani mngeona walivyofeli kutibu lakini huko kuona ni ngumu lakini hali ni mbaya sana Tanzania. Kaeni na madaktari mmalize hizi tofauti kumpiga Ulimboka sio suluhisho kwa mtu mwenye akili bali ni kuongeza tatizo.
 
Mimi ni Mtanzania asilia, nauchungu na nchi yangu. Tutapata wapi wataalamu wa baadae? kama elimu ya Tanzania inazidi kushuka.Mwaka 2005 waliohitimu kidato cha nne walikuwa 130000, Waliopata DIV 1, 2& 3 walikuwa 23000. Mwaka huu matokeo ya 2012 waliopata DIV 1,2 & 3 ni 24000 na watahiniwa ni 400000. Hakuna kitu tulichofanya katika elimu baada ya miaka saba. Ukifanya mahesabu ya haraka elimu imeshuka kwa asilia 300%
 
Back
Top Bottom