mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.
Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.
Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:
1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili
Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.
Tujadiliane