Tuition Chuo Kikuu cha Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuition Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mabuba, Dec 4, 2009.

 1. mabuba

  mabuba Senior Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 133
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.

  Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.

  Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:

  1. Je tution chanzo chake ni nini?
  (a). uhaba wa walimu
  (b) Ugumu wa maisha ya walimu
  (c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
  2. Sera ya elimu ina matatizo
  3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
  4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
  5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
  6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
  7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
  8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
  (a). mnalifahamu hilo
  (b). tatizo ni nini?
  (c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
  (d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili

  Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.

  Tujadiliane
   
 2. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Makubwa! hiyo ya Open University sawa kwani wale ni kama Distance learning hawapewi lecture, lakini huyu wa UDSM apewe lecture, notes, reference/literature then ana muda wa kukaa tena apewe tuition? au anapewa DESA au paper? UDSM kuna mambo sasa! yaani atafuniwe awekewe mdomoni - mh EAC inakuja huko sijui tutaweza kweli?
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Napata shida kuamini kama hilo jambo ni la kweli. Yaani University au Chuo kikuu wanazoma tuisheni? Hilo haliwezekani na kama lipo basi ndiyo laana ya mwisho kwa vyuo vyetu. Tumewambia vijana siku zote wakae imara kutetea misingi bora ya elimu badala yake wameendekeza starehe na ushabiki wa vyama (wengi nasikia wamejiunga na CCM). Sasa kama wamefikia hapo pa kuanza kukimbia kimbia na tuisheni tumekwisha.
   
 4. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi nilithani wanadai Tuition fee kutoka Bodi ya Mikopo
   
 5. chishango

  chishango JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  SUA hakuna huo ujinga wa tuition tuition hadi university!! MUNGU atusaidie yalianza madesa tukasahau vitabu kwa visingizio vya ukata sasa jipu lizidi kuvimba waungwana wahitimu wa UDSM kemeeni hili madogo ndo wana chepuka njia hivyo kaaaazi kwelikweli
   
 6. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Wanahitaji maombi waache kwenda mabash na madash ili wasome. Chuo Kikuu twisheni. Raha kweli
   
 7. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  hao ni vilaza wanaitwa vidu pale coet...yani ni project ya mama mkapa kuwainua wanawake kwenye masomo ya sayansi, wanalipiwa ada mpaka accomodation na tuisheni ili kuwa-boost.

  vidu kirefu chake ni viwango duni.
   
 8. P

  Pied Piper Member

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Great thinkers haya yana ukweli? labda mleta habari hajafanya uchunguzi wa kina.
   
 9. P

  Pied Piper Member

  #9
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ubaya wa twisheni ni nini?
   
 10. GP

  GP JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huyu mleta habari hajasema TWISHENI hiyo ni watu gani, WANAFUNZI WA UDSM, WANAFUNZI WA PRIMARY AU SEKONDARI.
  kwani pale chuo kikuu kuna shule ya msingi, labda ndio hao wametoka twisheni, kwa level ya NTA sidhani kama kuna uwezekano na ekweli wanafunzi wafundishwe twisheni kama za shule ya msingi/sekondari. HAIINGII AKILINI @ ALL
   
 11. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Changamoto kubwa hiko kwenye mfumo wa Elimu ambao wanafunzi hawana-access na vitabu toka elimu ya awali hadi vyuo vikuu.Watu wanakuwa wanasoma notes tu ambavyo zimekwisha tayarishwa na mwalimu na ambazo zinawasaidia kufaulu mitihani.

  Hivyo mtu anapoona notes alizonazo haziwezi kumfikisha sehemu anaona aende tuisheni ili apate version nyingine ambazo ni bora zaidi ndo maana kuna miaka fulani hapa mjini paliibuka majina makubwa sana ya walimu wa tuisheni wakina Mkandawile,Mama Shija....hawa ni maarufu sana among wanafunzi wa Science.Basically,sifa ya walimu hawa ilikuwa notes nzuri.

  Sasa katika mfumo huu hatuwezi kuwa na watu ambao wanapenda kuumiza kichwa....kutafuta vitabu vilipo na kujisomea.Wanafunzi wanakuwa wanapenda kutafuniwa...yaani wanafanya elimu ni bazoka....watafute tu na kupata utamu!

  Na nadhani tatizo la tuishini liko kwenye vyuo vyote kwa sasa maana watu wanaandikiwa hata disertation ili wapate degrees zao sasa inapofika hapa kazi inakuwa kubwa sana.Ukitaka kuona kuwa graduates wengi wanamaliza wakiwa shallow kweli yaani njoo mtaani unakuta mtu hawezi hata kuandika kitu kwa kiswahili....kazazi hiki chetu ni hatari sana!
   
 12. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jamani hakikisheni hili kwanza kabla hamjaanza kuumia kichwa yawezekana mnajadili hewa hapa au uzushi.
   
 13. GP

  GP JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kweli mpwa!.
  nimekugongea senksi.
   
 14. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  COET! kwa hiyo ni engineering! mi nadhani sio viwango duni inayopelekea hiyo tuition ila hivyo vijisent vimewalemaza wanaendekeza starehe wakijua watapata kutafuniwa, pili hao waalimu nao njaa ya namna gani hiyo lol! Kama mwl wa Univ anashindwa kuwa creative kutafuta hela kwa njia halali kwa kutumia elimu yake je wanafunzi wake watakuwa nini?
  KAMA NI KWELI HAWA WAALIMU WAWAJIBISHWE HASA, WANATUHARIBIA WATOTO.
   
 15. D

  Dina JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Tuition chuo kikuu?! Hii kali sasa...
   
 16. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Lisemwalo lipo ,kama halipo.................Chukua tahadhari kabla ya hatari
   
 17. P

  Pied Piper Member

  #17
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu kumbuka elimu sio vita. na unapoitafuta elimu lazima uzingatie kuokoa muda na nishati. kwanini mwanafunzi ahangaike kusoma vitabu kama UP 10 wakati anaweza kupata summary ya topics za fiziks kwa Mkandawile zinazoeleweka vizuri na kuwekwa pamoja? Kumbuka hao watoa twisheni wametutoa watu wengi sana tuliokuwa tunatoka shule za hovyo.
   
 18. P

  Pied Piper Member

  #18
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mama joe, hili la coet si hivyo kama unavyolielezea.

  Program (sio twisheni) inayoendeshwa coet kwa taarifa nilizonazo imelenga kuwasaidia watoto wa kike, kuwaandaa kwa ajili ya masomo yanayotarajiwa kuanza. Nia ni kuhakikisha wanamudu masomo yao na kuwahamasisha kuchukua masomo ya sayansi. Inawalenga watoto wa kike wenye maksi za wastani.
   
 19. m

  masaiti Senior Member

  #19
  Dec 4, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chuo kikuu cha DSM, kuna kitu kinaitwa Pre entry, hii ni kwa wanafunzi wa kike katika course za sayansi na injinia. Wanafunzi hawa hawakuweza kufaulu vizuri sana kidato cha sita, hivyo wanafanyiwa masomo ya ziada kwa muda wa wiki 10 kabla ya wengine kufungua chuo, baada ya hapo wanafanya mitihani na watakaofaulu huwa wanaendelea na wanafunzi wengine wa kawaida. Tulikuwa tunawaita VD yaani viwango duni kwani hawakufanya vizuri kidato cha sita. Nakumbuka kuna mmoja wao alikuwa anatukimbiza darasani kwelikweli.

  Mtoa mada sijui anawasema hao, au? Twisheni kama twisheni kwa wanafunzi wa kawaida, sijui ila kwangu haiingii akilini. Kama ni kweli basi twafwaaa. Ngoja nifanye upelelezi
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  eeeh Mahabuba sore mabuba hebu tuweke sawa kwanza kwa sababu wanafunzi wa UDSM huwa wanawafundishe Tuisheni wanafunzi wa sekondari na wale wa akademiz....sasa wewe unazungu

  It is not clicking kwa kichwa eti at that level watu wanasoma tuisheni...makubwa
   
Loading...