Kwanza kabisa napenda kujahamisha wanajf kuwa mimi ni mwalimu mwenye shahada ya uzamili jamii katika elimu, shahada ya elimu katika elimu ya watu wazima zote hizi kutoka chuo kikuu cha Dar es es Salaam, pia nina stashada ya elimu kutoka chuo cha ualimu korogwe ninauzoefu wa kufundisha miaka sekondari maika 7. Napenda kusema kuwa jina la Mabuba ni jina langu halisi na sio jina kivuli.
Naweza kutofautisha kati ya Tutorial na tuition. Hapa ninachozungumzia ni TUITION. Labda wanajf tujadili ukweli (issue) kuliko mtu. Tution ile inafundishwa na wanafunzi waliomaliza udsm, somo ni uchumi, kila mtu hulipa shilingi za kitanzania 500/= kwa kipindi. Mimi nadhani wote wanaotetea ni waathirika wa tuition.
Jamani tuition za aina hii hazijengi taifa. Hebu fuatilia wanafunzi wengi waliosoma tuition, utakuta hajuikujenga hoja, ni mtu wa kuelewa maswali kuliko dhana ya jambo. Wanakariri kuliko kuelewa. Pia wajf kuna vitabu TUITION yaani vile vya maswali na majibu, vitabu hivi kwa sasa ndio vianaongoza kwa mauzo ya vitabu.
Tujadiliane ukweli kuliko kuukimbia, tutatue tatizo