Tuition Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

SUA hakuna huo ujinga wa tuition tuition hadi university!! MUNGU atusaidie yalianza madesa tukasahau vitabu kwa visingizio vya ukata sasa jipu lizidi kuvimba waungwana wahitimu wa UDSM kemeeni hili madogo ndo wana chepuka njia hivyo kaaaazi kwelikweli

Jamani ni kweli, ni kwa nini wanataaluma wa UDSM wasiangalie wenzao wa SUA wanafanya vipi. Maana pale SUA kinachokuokoa ni kukaa Library au chini ya mtu na kupeleka msuli. Hakuna haya mambo ya aibu ya tuition. hii ni aibu kubwa kwa wanafunzi wa chuo kikuu kusoma tution.
Hili ni kweli lipo, Nenda pale Buguruni malapa, kuna kinjia kinaelekea kwenye dispensary ya kanisa la anglicana, Utakuta wanafunzi wa chuo kikuu pale wanasoma tution. Hili ni jambo ambalo linabidi liwe adressed mapema sasa na litafutiwe ufumbuzi wa kudumu. Mwisho wasomi watahitaji tuisheni ya kufanya kazi, ya kuongoza n.k pale wamalizapo masomo na kuingia ajirani.

TAFAKAR CHUKUA HATUA
 
J........

Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:

1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili

Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.

Tujadiliane

Jibu la jumla juu ya thread yako ni kuwa TUITION ni ishara ya kuporomoka kwa kiwango cha elimu katika Chuo Kikuu cha Dar FULL STOP!
 
Sijafanya utafiti kujua ukweli wa taarifa hizo ila UWEZEKANO HUO UPO!
Nimekuwa nikibadilishana mawazo na baadhi ya Waadhiri hapo MLIMANI wengi wanalia UKATA na CHUO KINAENDESHWA KISIASA ZAIDI TOKA MUKANDARA awe VC.
Ina wezekana WAMEBUNI njia ya kujiongezea Kipato.
Nasikia hata DARUSO siku hizi ni kama haipo !
Wenye taarifa za ndani watupatie tuzifanyie kazi !
 
Jamani is this possible? ungewauliza ni tuition ya masomo gani mbona aibu?! Mimi ninaelewa wale wakufunziw anaokwenda kutoa lecture za ziada (ambazo kwangu ni tuition tu) kwenye vyuo vingine yaani mwalimu toka UDSM anakwenda kutoa kwa wale wanaosoma Open ambao huwa hawana lectures za kutosha na katu si kwa wanafunzi wao wa UDMS kama ni kweli basi MKANDALA ashughulikie hilo haraka iwezekanavyo.Kwa sababu ada ya chuo ambayop mwanafunzi analipa inacover mshahara wa mwalimu sasa kama mwalimu anafundisha masomo ya ziada kwa malipo ni wizi, unyonyaji na ufisadi wa hali ya juu!! Ni kama anayepokea mshahara miwili kwa majina tofauti kwa kazi moja!
 
Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.

Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.

Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:

1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili

Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.

Tujadiliane

Huenda walikupatia jibu hilo kuwa wanatoka TUITION ili usiendelee kuwabughudhi. Kwa uzoefu wangu wa elimu ya juu niliyoipatia hapo hapo UDSM suala la TUITION in Higher education ni suala butu linalohitaji mwendawazimu tu ili aweza kuhudhuria hiyo TUTION kwa sababu zifuatazo

1. Mitihani yote unayofanya inatungwa na LECTURER wako anayekufundisha darasani, ambaye anahitaji wewe ujibu kama anavyofahamu yeye na alivyokufundisha darasani. Sasa kufundishwa na mtu yeyote ambaye hana connection na LECTURER wako (Hapa namaanisha Tutorial assistant ambaye anapewa nondo na LECTURER kuja kuendesha Tutorial/Seminars) ni upotezaji wa muda na resources.

2. Njia pekee ya kufaulu Elimu ya juu ni kuhudhuria Lecture zote na tutorials zake, kusoma vitabu alivyopendekeza Lecturer kwenye course outline na handouts kwani ndiyo msingi wa yeye kufundishia darasani na kufanya mazoezi yote anayotoa kwa kuelewa na si kukariri solutions.

3. Kuwa na group discussions ambazo zinaongeza uelewa kwa kujieleza na kuwa challenged na wenzako ambao mnahudhuria lectures pamoja.

4. Different lecturers may have different approaches to the same subject, hivyo ndiyo maana utakuta mtu anarudia mwaka(enzi zile za term system) au ana carry subject (enzi hizi za semester system) kwa somo/masomo ambayo alisoma mwaka mzima na ana material ya kutosha ila kwa kuwa anayemfundisha ni mwalimu mwingine still bado ana-fail tena.

Chuo kikuu ni sehemu ambayo watu wanakuwa trained to think, if you can't think there's a slim chance for you to be successful regardless umehudhuria Tuition ya Professor au Mr ambaye hana responsibility ya ku-set your final exams.
 
Kawaida si mpenzi wa kuandika makala ndefu lakini kwa vile umenigusa, nitajitahidi hususan kwa sababu suala hili linanikera sana na halihusu tu walimu - wamo madaktari na watu wa fani nyingine. Nianze na tuition ambayo haikuwepo wakati wa zama zangu - na sijafika miaka hamsini bado. Hata hivyo, sehemu mbalimbali duniani tuition hutumika kwa wanafunzi wanaohitaji msaada wa ziada kutokana na matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na dyslexia uwezo mdogo wa kujifunza. Lengo huwa ni kuwasaidia wafikie kiwango kinachotakiwa au wanachotegemewa. Sasa, katika mazingira wanayosomea watoa tuition hutoa huduma hiyo kama sehemu ya kazi yao na kwa malipo yaleyale yaliyo katika mikataba yao. Zipo, hata hivyo, sehemu ambazo mtu huweza kwenda au kumpeleka mwanae kwa malipo - motisha wa hili ni kwamba mwanafunzi au mzazi wake anatambua kwamba hawezi, kwa namna moja au nyingine, kwenda sambamba na masomo katika muda wa kawaida. Yote haya mawili ni mambo ya kawaida - na hayatakiwi kutushangaza tuwe Musoma au Geneva.

Moja la kushangaza ni pale ambapo mwalimu huyo huyo amalizapo darasa huendeleza darasa jingine la kulipia kwa wanafunzi walewale. Mdogo wangu ana watoto anawasomesha shule ya msingi moja maarufu sana Dar - kama si ya kwanza kwa maarufu - na wanaotoa tuition kwa watoto wake baada ya shule ni walimu kutoka madarasa yao! Pengine hapana sheria ya kuzuia hili lisitendeke (toka Ujamaa ulipokufa) katika mazingira ya ubinafsi - lakini kwa hakika ni kinyume cha maadili. Wakati huohuo wanafunzi wanavutika kwenye tuition si tu kwa sababu wanahitaji msaada wa ziada bali ipo imani kwamba huenda wasifaulu wasipohudhuria tuition hizo kitu ambacho kitawapunguzia nguvu ya ushindani katika soko la kazi. Kwa haya mawili kunakuwa na mduara wa tatizo. Kama nilivyosema awali, tabia hiyo ambayo nimesema inanishangaza pia wanayo madaktari wetu sehemu nyingi saana nchini ambao huwaona wagonjwa katika sehemu zao za kazi y aumma na kuwashauri waende kwenye hospitali zao binafsi nyakati zingine.

Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.

Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.

Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:

1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili

Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.

Tujadiliane
 
Pengine hapana sheria ya kuzuia hili lisitendeke (toka Ujamaa ulipokufa) katika mazingira ya ubinafsi - lakini kwa hakika ni kinyume cha maadili.

Kama itapita hiyo sheria ianze kwanza kuwabana wataalamu ambao wanatumika zaidi ya sehemu moja. Kwa mfano madaktari kwenye Hospitali za Umma ambapo pia wamefungua vizahanati binafsi na pengine kushinda muda mwingi huko na kuelekeza wagonjwa kwenye hizo zahanati zao. ,Je wao hawakiuki pia maadili na pengine hata kuhujumui madawa na vifaa ambavyo vimenunuliwa kwa fedha za umma?.

Azimio la Arusha halipo tena, Nyerere na TANU walileta Azimio la Arusha, CCM ya 1990's imelitupilia mbali Azimio kwa kuwa fikra zake zilikuwa za upotoshaji wa ukweli na kwamba liliwanyima raha "mafedhuli" kwa kuwazuiwa wasiwe na mishahara miwili, wasiowe na fikra za kibepari, wasiwe na nyumba za kupangisha nk.nk.

Leo kila sekta imekuwa "binafsi" na watu wote ni "wabinafsi" kuliko nafsi zao wenyewe.

Hata kanisani na misikitini sasa kuna tuisheni. Kuna madrasa na madarasa, halafu kuna sala na Ibada za maombi (maombi ya faragha hufanyika nje ya utaratibu wa ibada za kawaida, na hayo ndo yanatengeneza chakula ya makasisi/ wachungaji/ mapadri, maimam/ Sheikhe na familia zao.

Ebu ona leo sio kama zamani, vijana ambao pengine hawajasoma kabisa hawaogopi kusimama madhabahuni na kutaja jina la Mungu, kukemea hata wazee na hata wasomi kwa kivuli cha Uchungaji/ Upadri na kusema wao wanajua ya duniani na mbinguni. Kazi ya kanisa au msikiti haiogopwi tena kwa kuwa inaposho nono na isiyo na jasho wala makelele ya watu.

Dunia imebadilika!
 
Jamani kwa kweli inasikitisha sana niko UDSM najaribu kufuatilia suala hili na nimepata baadhi ya majibu kuwa wanaofundisha si walimu bali wanafunzi waliomaliza chuo kikuu na kukosa ajira then wanakuja kuhadaa wanafunzi hapa na kufundisha tuition. Sidhani kama uongozi wa juu unalifahamu hili. Ngoja nifuatilie tena
 
Mwaka jana mwishoni ililetwa hapa mada juu ya ubora wa shahada wanazotunukiwa watu wanaosoma chuo kikuu huria, eti wanalala jioni-asbuhi na pale mtu wa chuo kikuu cha dar es salaam anabanwa na mwalimu juu ya supp!! Binafsi nilijiuliza maswali mengi sana. Hili la masomo ya ziada kwao, linazusha tena makovu ndani ya nafsi yangu,na hapa napata mwanga juu ya chanzo cha chuo chetu kushuka viwango. Hili halihitaji mjadala nje ya chuo wala nchi. Hapa ndipo wanapotoka watu kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili Taifa na Dunia hii, wakufunzi, kama mlilifumbia hili macho motisha kwenu ni fedheha. Tafadhali liepusheni Taifa na hili jinamizi.
 
Mi nadhani tuache kushambuliana hapa cha msingi ni kufanya utafiti then mambo yawekwe hadharani
 
Jamani kwa kweli inasikitisha sana niko UDSM najaribu kufuatilia suala hili na nimepata baadhi ya majibu kuwa wanaofundisha si walimu bali wanafunzi waliomaliza chuo kikuu na kukosa ajira then wanakuja kuhadaa wanafunzi hapa na kufundisha tuition. Sidhani kama uongozi wa juu unalifahamu hili. Ngoja nifuatilie tena

Pia mi nadhani hiki chuo kiliharibika pale ambapo vilaza wote waliruhusiwa kuingia as long as wanaweza kulipa fees. Kwa hiyo ile mitoto ya mama yote ambayo inajua starehe tu bila kukaza msuli ilivyojazwa chuoni pale, ikawa mwisho wa elimu, its business as usual.
 
Sijafanya utafiti kujua ukweli wa taarifa hizo ila UWEZEKANO HUO UPO!
Nimekuwa nikibadilishana mawazo na baadhi ya Waadhiri hapo MLIMANI wengi wanalia UKATA na CHUO KINAENDESHWA KISIASA ZAIDI TOKA MUKANDARA awe VC.
Ina wezekana WAMEBUNI njia ya kujiongezea Kipato.
Nasikia hata DARUSO siku hizi ni kama haipo !
Wenye taarifa za ndani watupatie tuzifanyie kazi !

Taifa linaangamia, kwani mbaya zaidi hao wenda tuition ndo watakao onekana wana GPA kubwa, na wale waendensha misuli library watakua na GPA ndogo ambazo hazitawawezesha kubaki Mlimani kama wahadhiri, nisikilizie hapo kama kuna wazee wa GPA kubwa kama watakua na uwezo wa kufanya tafiti yakinifu wa maendeleo ya taifa. Shame on them!!!!!!!!! Mungu ibariki tanzania.
 
huyu mleta habari hajasema TWISHENI hiyo ni watu gani, WANAFUNZI WA UDSM, WANAFUNZI WA PRIMARY AU SEKONDARI.
kwani pale chuo kikuu kuna shule ya msingi, labda ndio hao wametoka twisheni, kwa level ya NTA sidhani kama kuna uwezekano na ekweli wanafunzi wafundishwe twisheni kama za shule ya msingi/sekondari. HAIINGII AKILINI @ ALL
Mzee hili halina ubishi hata kidogo,kipindi nabukua pale mlimani kuna wanafunzi wa kozi moja walikuja na kuniomba niwafundishe tuition ya hesabu topic ya statistic, nkawahoji sana na mwisho nikwaambia kama mkipata utata njooni nitakusaidieni na siyo kukaa darasani na kuwafundisha tuition.Sasa kama chuo kikuu unasoma tuition na darasa la saba lifanye nini?
Kwa hili lazima likemewe kwa nguvu zote na kila mpenda nchi yake na maendeleo ya Taifa lake.
 
Back
Top Bottom