mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
- Thread starter
- #61
Tunakushukuru mtoa mada hii kwa kuileta hapa jamvini ili wanataaluma wenzako (walimu) waweze kutoa michango yao mbalimbali kwamba tatizo la tuition ninini? ikizingatiwa kwamba hapo kabla haya mambo hayakuwepo na bado kiwango cha uzamivu naamini kilikuwa kizuri kuliko ilivyo sasa.
Kwa haraka haraka nadhani tuition ni matokeo ya wanafunzi kutopata muda wa kutosha ili kuhudhuria masomo, walimu kutotumia ipasavyo muda uliopangwa kwa lecture na badala yake kufanya mambo yao kutokana na kazi yenyewe (taaluma ya ualimu) kutothaminiwa na mwajiri mkuu (serikali). Yote mawili au uwezo mdogo wa wanafunzi na walimu na hivyo kuchukua muda mrefu kufidia vitu ambavyo mwanafunzi alitakiwa awe anafahamu kabla ya kuwa katika level hiyo ki elimu.
Mwisho kabisa, ni bahati mbaya kwamba tuition imeshakuwa utamaduni.utashangaa kwamba mzazi ana mpeleka mwanafunzi tuition kwa ajili ya pre std one. Kama taifa tuone jinsi hali ilivyo mbaya ki elimu.
[Asante kwa udadafuzi huu]