Tuiteje Fasihi simulizi iliyoandikwa?

kwa mtazamo wangu,inabakia kuwa fasihi simulizi sema tu imehifadhiwa katika maandishi ili isipotee..

uko sawa, kwa kuwa ishu sio kuandikwa, ishu ni msingi wayo. Hata nyimbo ni fasihi andishi ingawa huimbwa mdomoni.
 
halafu hizi teknoloji hizi....sijui tutasemaje

mfano filam hizi kwenye gadgets...
 
Niondoleeni ukusi ukusi wa mawazo. Fasihi simuliz iliyoandkwa 2iteje?

Inaitwa Fasihi andishi

Hii ni sanaa itumiayo maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.

Fasihi andishi hugawanyika katika matawi mawili: nathari na ushairi.

Pia fasihi andishi ina tanzu nyingi mbalimbali, hasa riwaya, tamthiliya, insha, shairi n.k.
Kulingana na mada ya kazi ya kifasihi, inawezekana kutofautisha bunilizi na kazi zinazowakilisha ukweli.

Marejeo: Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.
 
sio sawa kusema kuwa ni fasihi andishi, kwani uwasilishwaji sio kigezo pekee cha kuitambua fasihi. ile ni fasihi simulizi iliyohifadhiwa kwenye maandiko.
 
naunga mko hoja coz fasihi cmulizi iliyoandikwa nitofauti kabisa na fasihi andishi.
 
uko sawa, kwa kuwa ishu sio kuandikwa, ishu ni msingi wayo. Hata nyimbo ni fasihi andishi ingawa huimbwa mdomoni.

y nyimbo ni fasihi andishi? Kuna hadith kibao zinakua na nyimbo ndani yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom