-Mimi ningewashauri ndugu zangu tuwe na taarifa kamili ya jambo tunalochangia humu jamvini na sio kuongea kwa chuki na jazba tu.
Je watu wote walioomba kazi benki ya Posta walizipata kwa sababu ya kujuana na watu??? Mimi siamini hilo na hata wengi wametoa ushuhuda wao humu jamvini. Mimi nimejaribu tu kulifuatilia hili jambo na hata kuangalia financial performance za benki hii katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya mwaka huu 2013, 2012, 2011. Kwa kweli ukiangalia utaona ni kweli benki imebadilika kwani mapato na hata assets zao zimekua sana, yaani Zaidi ya maradufu. Benki hii imetengeneza faida ya bilioni 7 mwaka jana. Hebu tujaribu kuangalia pia na upande huu kuliko kuwabeza tu kwani hii hi Benki ya Umma, yaani benki yetu.
Vile vile hata ukiangalia gharama za Benki kwa upande wa mishahara zimekuwa kwa kiasi kikubwa.Hii inamaanisha kwamba benki katika kipindi cha miaka hii imeongeza mishahara kwa kiasi Fulani.--Mimi ninawajua baadhi ya watu waliotoka kwenye hizo benki tunazoziona kama bora, wakitafuta kujiunga na benki hii.
Kwa ujumla hizi changamoto zipo sana kwenye taasisi nyingi za umma hapa nchini na hata nyingin zimeshakufa kwa ubadhilifu. Kwa zile taasisi ambazo zinajitahidi kufanya kazi na kutengeneza faida kama benki hii mimi nafikiri ni vizuri tukawatia moyo kuliko kutoa maneno ya kashfa na yasiyo na ukweli wowote. Tukumbuke kwamba taasisi kama hizi ndio zinazotoa ajira kwa ndugu zetu wengi hapa nchini.
-