Maoni nitakayotoa kwenye Tume ya Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni nitakayotoa kwenye Tume ya Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlitika, Apr 7, 2012.

 1. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hi JF Members.
  Mkulu ndo huyo keshaunda Tume ya Katiba. Fikra zetu wakati huu zisiwe tena kuijadili tume bali kujiandaa kuipa majukumu. Ndiyo maana nafungua peji hapa chini.

  Ili tuendelee tunahita misingi ya kikatiba yenye kutujengea nidhamu inayotulazimisha kuelekeza rasililmali tulizonazo katika shuguli za maendeleo ya kweli na ya mipango mkakati ya muda mrefu. Hatuwezi kufanikiwa katika hili bila kwanza kuwa na katiba itakayobomoa kwa lazima lelemama hii ya kimaadili inayoruhusu serikali zetu na watumishi wake kuelekeza rasilimali katika mambo ya kifahari na ya muda mfupi. Namna pekee ya kuisaidia serikali ni kuijengea mazingira ya kikatiba yanayoifanya iwajibike kwa wananchi; na siyo kinyume chake. Katiba tunayoihitaji inapaswa kuchukua sura hii:

  MUUNGANO
  Hii kitu isitishwe kwanza maana longolongo za upande mmoja zimetuchosha MNO sisi wa upande mwingine, na hii inagharama kubwa na imedidimiza mno maendeleo ya nchi hii. Upande utakaoumisi upande mwingine basi upewe dirisha la kuaplai ndoa; then MOU itengenezwe afu tupige kura za maoni na hoja ipite baada ya asilimia 80 kila upande kuafiki ndoa.

  MUUNDO WA SERIKALI

  1. Makamu wa raisi ndiyo atakuwa Waziri Mkuu
  2. Wizara 15 zinatutosha sana. Sifa za kuwa waziri zibainishwe.
  3. Jukumu la uteuzi wa Mawaziri na wakuu wa mikoa (ambao wataitwa Wakurugenzi wakuu wa Mikoa) apunguziwe raisi. Utaratibu utengenezwe atakaofuata raisi katika kuteua Mwanasheria mkuu, waziri mkuu, wakuu wa majeshi, ......
  4. Wakuu wa wilaya hawahitajiki; Kurugenzi zinatosha. Sifa za wakurugenzi zibainishwe then wawe wanaaplai kazi kwa ukomo wa miaka mitano tu then wanaaplai upya na wapo answerable kwa Mkurugenzi mkuu wa mkoa (MMM). MMM atakuwa hana majukumu ya kisia bali ni kumonita maendeleo ya kurugenzi zake.
  5. Iwepo nafasi ya Mkurugenzi Mkuu Taifa (MMT) ambaye jukumu lake ni kumonita wakurugenzi wa mikoa, (MMM's). Huyu ni kama makamu waziri mkuu, ila anashughulikia kurugenzi/mikoa na waziri mkuu anadili na politics na ni mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri.

  TUME YA UCHAGUZI
  Jukumu hili ni nyeti hivyo mwenyekiti wa tume lazima achaguliwe na WANANCHI au na wawakilishi wao yaani madiwani na wabunge wote. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi awe answarabo kwa Bunge.

  MAFAO (BENEFITS) ZA WATUNISHI WA SERIKALI NA UMMA
  Matumizi ya kifahari yapigwe ban kikatiba. Mfano: Magari ya kifahari aina zote serikalini iwe taboo.

  • VX inamtosha sana rais. Mikoani atumie helikopa na hahitaji msururu wa magari ya waambata.
  • Gari la Makamu wa Raisi/Waziri Mkuu hadhi ya Toyota Sequoia inatosha sana.
  • Mawaziri, MMM's, Wabunge: Prado (kaulizeni kwa wenzetu hapo Kenya)
  • Wakurugenzi wa wilaya: Rav4.
  Ninayo mengi hapa wakuu, yaani daftari limejaa, lakini nataka kwanza niwasome mmekaaje kikatiba.

  Nawasilisha.
   
 2. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwanza tungejifunza kuhusu huyu jamaa 'Baron de Montesquieu' na philosophy zake kuhusu katiba Separation of powers - Wikipedia, the free encyclopedia katibaya Taifa iweje maana kawafunza mengi wazungu kuhusu checks. Na kitabu chake kuhusu hii issue, his patents rights are no longer respected, therefore somewhere on the net the book is available for free.

  Hayo mengine ya muungano baadae first things first right we can not allow the abuse of the system to continue, these people are not living in our world and they have taken our votes for fear of them.
   
 3. kalendi

  kalendi JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 895
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Kuwe na kipengere katika katiba yetu;"NI MARUFUKU KWA KIONGOZI WA AINA YEYOTE NA HATA FAMILA ZAO KUSOMA AU KUTIBIWA KWENYE SEKTA BINAFSI".
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  umesahau, MARUFUKU KUTIBIWA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI. ili nao wajue ugumu wa maisha unaotupata walipa kodi wa nchi hii.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jamani angalieni wajumbe wa kamati hiyo wamewahi kufanya Nini katika nchii katika kuendeleza haki za binadamu, kusimamia haki na rasilimali za taifa, kusimamia mazingira and the like. Wengi ni waganga njaa na kwa sababu hiyo watatengeneza taasisi na kuweka mazigira ya wao kuwemo kwenye hizo taasisi.

  Makamu na makamu wake walifanya Nini wakati wa utumishi wao kwa watanzania kitu ambacho tunaweza sema walituachia, hasa ukuzingatia nafasi za juu walizoshika kwa muda mrefu katika uongozi waziri mkuu na jaji mkuu.
   
Loading...