Tuishi kwanza..harusi itafuata baadae!

Tuishi kwanza..harusi itafuata baadae!

Imagine kama ni ww umeishi na kijana kama 6month hivi halafu mnashindwana tabia, jamii itakuchukuliaje? baada ya hapo unatafuta mwingine ambae mtaoana hapo baadae nae unaishi nae miezi mitano mnasomana tabia kisha unagundua hafai. Unatafuta mwingine tena inakuwa mwendelezo..........endless.

Nafikiri ndoa ni muhimu sana kama nafasi ya kufunga ndoa ipo kuliko kuishi na mtu. Ndoa na harusi Inakupa amani, uhuru, uhalali na umiliki na pia hata uvumilivu kwa yule uliye naye. Hii ya kuishi na huyu, mnakorofishana kesho uko na mwingine unaweza kujikuta umeishi na watu hata 5 jamb linaloweza kukufanya uonekane muhuni. Binafsi jambo la kuishi na mtu bila ndoa huwa nalifananisha na mtu kukwambia wewe fanya kazi tu, mwisho wa mwezi ukifika au kazi ikikamilika tutakubaliana na kulipana. Baada ya kazi kuisha, chochote chaweza kutokea ikiwepo kupunjwa haki yako.
Nakuunga mkono hapa.
 
kwa maisha ya vijana na mabinti wa sasa ni muhimu kuishi kwanza kabla ya ndoa maana ndoa za sasa utata mtupu!
 
kwa maisha ya vijana na mabinti wa sasa ni muhimu kuishi kwanza kabla ya ndoa maana ndoa za sasa utata mtupu!

Use your past failure as a catalyst of your future success. In other words you can use somebody's failure as catalyst of your future success. Hivyo basi hapo kwenye bluu inaonyesha ni jinsi gani vijana ama jamii ya leo tulivyo dhaifu kifikra. Lazima tuliface tatizo na kulisolve na sio kukimbia tatizo
 
Mkuu Himidini, niseme mtazamo wangu hapa...
Mimi nahis kupimana/kuishi pamoja bila ndoa, generally ni kitu kibaya, ie eti unakaa na mtu mwaka/miaka huku ukimtumia afu eti unasema huwezi kumuowa coz umegundua anatabia mbaya as well as mlikua mkipimana, sasa hayo ndio majibu! Umeshaula utamu wake wote, umeshamueka limvungu mtoto wa watu, umeshamfanya hata akitingisha mashine watu hawaangalii mara mbili, nk.
Ubora wa kuishi bila ndoa unakuja kwa Wanaume wa kikristo tu! Coz kwao ndoa ndoana, Uislamu hakuna hii, unamuona leo, kesho unaoa, keshokutwa kazingua, unampa talaka, kwao! Hivyo basi mm nahis iyo kupimana iwe reasonable, izingatie mda na kuwe na limit za kumtumia mwenzio, ili ukigundua hakufai aweze kuwafaa wengine. Mkumbuke ktk kupimana kwenu hakuna aliyekamilika...!
Nawakilisha.
 
Kwa upande fulani inasaidia kupimana; kiasi kwamba mambo yasipokuwa mazuri mnaweza kuachana bila kuwa na kiwingu kile cha "until death do you apart".

Tukirudi upande mwingine, ndoa/harusi ni nini zaidi ya mkataba? So Mkataba unakupa uhalali, unakupa insurance na mengine ingawa sio lazima upendo wa kweli. So kwa mdada, kupata uhalali basi ndoa ni muhimu; lakini je mkaka yeye hahitaji huo uhalali?

Nakubaliana na wewe mia!
Maisha haya bila kupimana kidogo ukapata walau picha litakavyokuwa mbele unaweza ukajilaumu maisha yako yote!
Kaeni miaka miwili mitatu mkiona mnawezana then mnapeana contract ya moja kwa moja (ndoa),mkiona mmeshindwana basi kila mmoja na ustaarabu wake! Ndoa sio adhabu bwana wala kifungo
Me nnachoona kikwazo kikubwa ni dini haziruhusu vile vile wazazi wanaona sio heshima!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkuu Himidini, niseme mtazamo wangu hapa...
Mimi nahis kupimana/kuishi pamoja bila ndoa, generally ni kitu kibaya, ie eti unakaa na mtu mwaka/miaka huku ukimtumia afu eti unasema huwezi kumuowa coz umegundua anatabia mbaya as well as mlikua mkipimana, sasa hayo ndio majibu! Umeshaula utamu wake wote, umeshamueka limvungu mtoto wa watu, umeshamfanya hata akitingisha mashine watu hawaangalii mara mbili, nk.
Ubora wa kuishi bila ndoa unakuja kwa Wanaume wa kikristo tu! Coz kwao ndoa ndoana, Uislamu hakuna hii, unamuona leo, kesho unaoa, keshokutwa kazingua, unampa talaka, kwao! Hivyo basi mm nahis iyo kupimana iwe reasonable, izingatie mda na kuwe na limit za kumtumia mwenzio, ili ukigundua hakufai aweze kuwafaa wengine. Mkumbuke ktk kupimana kwenu hakuna aliyekamilika...!
Nawakilisha.

^^
Mashaxizo
Nimekupata vema Mkuu,,hilo suala la muda maalum n.k
Vipi kwa wale ambao wanapendana ila mwanaume hana uwezo kifedha,je binti awe tayari kupoteza pendo la kweli kwa sherehe tu!
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
charminglady
Kwa maneno rahisi tu unaona waliopitia harusi kabla ya ndoa rasmi,,wanaishi bila nyumba ndogo?
^^

Pale niliposema za kufikia nilimaanisha nyingi au anakuwa anaona kawaida tu. Ila kama atakuwa amekupenda hata kama atakuwa na nyumba ndogo hutokaa ugundue na heshima itakuwa pale pale pamoja na caring. Ila kama atakuwa kalazimisna dharau zitakuwa square.....
 
Last edited by a moderator:
Tatizo wengi wanadhani ndoa ni sherehe na ndio maana inakuwa ngumu kufanya maamuzi ya kutangaza nia pia na nguvu ya ndugu na jamaa ambao huwa hawako tayari kumwona mtoto wao anakwenda kimya kimya bila kufanya sherehe na kupiga picha kwenye round about ya samaki kwa huku kwetu Ng'waza au Baharini. Lakini kwa upande mwingine, uzoefu unaonyesha wale walioamua kuishi pamoja wengi hudumu kwenye mahusiano na wachache huachana, ndoa za namna hii zipo sana katika yale maeneo yetu ambayo wengi huyaita ya uswahilini na huwa tunagundua watu hawajaoana pale linapokuja suala la kubariki ndoa.
 
^^
Mashaxizo
Nimekupata vema Mkuu,,hilo suala la muda maalum n.k
Vipi kwa wale ambao wanapendana ila mwanaume hana uwezo kifedha,je binti awe tayari kupoteza pendo la kweli kwa sherehe tu!
^^

Kupoteza pendo la kweli kwa sherehe tu, sio sahihi.
Kumbuka "in case of necessity haram inakuwa halali"
kwa mtizamo wangu ikiwa kweli wanataka kuoana, hakuna hela ya sherehe, huyo m/mke si atulie kwao kwanza, ili jamaa azichange, pia jamaa kama anapenda kweli ataingiwa na hamu ya kutekeleza hilo, wakiishi pamoja jamaa atapungua nguvu za kutaka ndoa kutokana na kuwa interest zake anapata, then wakiwa pamoja matumizi huzidi na kutotimia kwa hiyo hela ya arusi kwa sababu jamaa si kipato chake kidogo! Usiniambie m/ke akitulia kwao hakutokua na mapenzi. Hiyo rule ya juu (in c....) itatumika endapo m/ke anaishi mazingira magumu/hatarishi huko kwao.
Si unalionaje hili Mr. Himidini!
 
Last edited by a moderator:
Wanawake wengi siku hizi waharibifu sana, yani unakuta mwnmk katoa mimba mpk yai la mwisho, hapo unapigwa japo mtoto mmoja kisha ndoa inafuata.
 
^^
Naomba tujadiliane kwa mabinti ambao wamekutana na wanaume ambao hawako tayari kwa harusi au kuhalalisha ndoa.
Anakupenda sana lakini kwa sababu ambazo pengine ni za msingi au la! Hayuko tayari kwa harusi,,ndoto ambayo umeiota tangu utoto.
Lakini anakuambia "...tuishi kwanza,,harusi itafuata baadae"
Je,unamwelewa vipi mwanaume wa aina hiyo?
^^

Hakuna harusi hapo.
 
unigegede kila siku hivi hivi kisa ndoa? aah wapi.....siamii kwa mtu kamwe
 
Kupoteza pendo la kweli kwa sherehe tu, sio sahihi.
Kumbuka "in case of necessity haram inakuwa halali"
kwa mtizamo wangu ikiwa kweli wanataka kuoana, hakuna hela ya sherehe, huyo m/mke si atulie kwao kwanza, ili jamaa azichange, pia jamaa kama anapenda kweli ataingiwa na hamu ya kutekeleza hilo, wakiishi pamoja jamaa atapungua nguvu za kutaka ndoa kutokana na kuwa interest zake anapata, then wakiwa pamoja matumizi huzidi na kutotimia kwa hiyo hela ya arusi kwa sababu jamaa si kipato chake kidogo! Usiniambie m/ke akitulia kwao hakutokua na mapenzi. Hiyo rule ya juu (in c....) itatumika endapo m/ke anaishi mazingira magumu/hatarishi huko kwao.
Si unalionaje hili Mr. Himidini!

^^
Nimekuelewa kuwa zama hizi,,ndoa ya harusi yaweza kuwa silaha ya mwanamke kupima upendo wa mwanaume.
Da,,haya mambo yana ugumu kumbe,,nadhani wahusika wanatakiwa kuliangalia ikiwa litajitokeza kama changamoto.
Mashaxizo
^^
 
Last edited by a moderator:
unigegede kila siku hivi hivi kisa ndoa? aah wapi.....siamii kwa mtu kamwe

^^
Smile ule usemi wa "kwa raha na tabu tutadumu daima" huoni utashindwa kuutimiza mwanzo tu? By the way Kwa nini msiweke muda mf..within a year kila kitu kiwe tayari?
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
But lara 1 cheti cha ndoa hakikupi guarantee ya ndoa yenye furaha..i.e umemkataa mnae-match nae kwa kigezo cha kukunyima harusi tu.
Huoni kuwa wapo waliofanyiwa harusi za gharama lakini bado wanasota?
Cc. Heaven on earth Ablessed @FP @Cynithia Chriss
^^
Kiimani hairuhusiwi kuishi kwanza halafu ndoa baadae na pengine hata kwa jamii unayoishi inaweza ikawa haikubaliani na uamuzi wa kuishi bila ndoa. Lkn nimeshuhudia ndoa kadhaa baada ya kufungwa maisha yanakua ndivyo sivyo yaani wanakua hawafanani kabisaa utadhani walilazimishwa kuoana. Mpaka wakati mwingine unatamani bora wangeishi kwanza halafu ndoa ingefuata baadae na hasa ukizingatia ndoa zetu hakuna kuachana . Nionavyo mimi kila uamuzi unaochukuliwa na wahusika una risk . Sasa sina jibu moja kama je ni sawa kuisi kwanza bila ndoa kwa sababu yoyote au kufunga ndoa kwanza ijapokua moyoni mwangu ningependa ndoa ianze na si kuishi kiuchumba. Tukumbuke kadiri tunavyokua pamoja ndipo tunapojuana zaidi mpaka vile vitabia vya ndani kabisa, sasa huenda ulimpenda sana mhusika lkn waweza katishwa tamaa na vitabia hivyo so unaamua kutofunga nae ndoa wakati tayari mlishaishi pamoja. Kumbe mgefunga ndoa kabla ya kuishi wote hivyo vitabia usingevijali. Choice zote mbili zinategemea uamuzi wa walengwa na zote zaweza kuwafaa au kuwaangusha.
 
^^
Naomba tujadiliane kwa mabinti ambao wamekutana na wanaume ambao hawako tayari kwa harusi au kuhalalisha ndoa.
Anakupenda sana lakini kwa sababu ambazo pengine ni za msingi au la! Hayuko tayari kwa harusi,,ndoto ambayo umeiota tangu utoto.
Lakini anakuambia "...tuishi kwanza,,harusi itafuata baadae"
Je,unamwelewa vipi mwanaume wa aina hiyo?
^^

Kumbuka kuwa na mahusiano na mwanamme si lazima akuoe. Ni kosa la jinai kuoa mwanamke bila kujua tabia yake na kwao anakotoka wako vipi. Huwezi kuoa mwanamke halafu uje kusoma tabia yake wakati mmeshaoana, ni ujinga hata mimi Mkereketwa nitakutukana tu na kukupiga ban JF. Sawa, ndiyo unaweza ukampenda mwanamme lakini inabidi jamaa aangalie kwanza usawa wake na kama kweli wewe ndiye utakaemfaa katika maisha yake maana kila mtu ana mtazamo wake kimaisha. Mwanamke mwingine anajifanya ana tabia nzuri na mwema, ukioa tu anaanza vituko mara sitaki kazi wenzangu wananionea wivu, oh shosti wangu kanialika kwenye kibao kata, au leo ukirudi kazini nataka uniletee chips mayai na kuku mzima wa kukaanga kwani nataka kuwatambia wenzangu hapa mtaani kabla sijaenda kuona shoo ya bongo fleva, yaani use.nge mwingi tu....utaoaje mtu kama huyu? Inabidi umchunguze kwanza na kama roho inakubali then unaomba baraka za wazazi ufunge ndoa. Kosa wafanyalo wanawake wengi ni kule kulazimisha kuolewa baada ya kuota ndoto za abunuwasi, utatoka na demu wiki mbili tu utasikia sasa utanioa lini, au tukifunga ndoa yetu ningependa niwaalike watu fulani ili niwatambia mana wamezidi, what for? Nyie mademu nyie, basi tu. Na ndiyo maana sie tunafunga ndoa nayi si kwa kupenda bali kutekeleza matakwa yenu. Mmeshaona mwanamme ana furaha kwenye harusi? Mmewahi kujiuliza kulikoni? There you go, fikirini kwanza.
 
Watu wawili wakielewana ni vizuri sana hata wazazi wetu tumeshuidia wakifunga ndoa huku wana wajukuu tayari. lakini leo hii unakuta binti analazimisha ndoa then hata hajamaliza fungate ndoa inavunjika.
 
kwa sisi wakaka huu mkataba sio muhimu sana, why I don't know why, ila tu sidhani kama ni muhimu sana na kama ni wa muhimu basi sio wa haraka kihivyo
Kwa upande fulani inasaidia kupimana; kiasi kwamba mambo yasipokuwa mazuri mnaweza kuachana bila kuwa na kiwingu kile cha "until death do you apart".

Tukirudi upande mwingine, ndoa/harusi ni nini zaidi ya mkataba? So Mkataba unakupa uhalali, unakupa insurance na mengine ingawa sio lazima upendo wa kweli. So kwa mdada, kupata uhalali basi ndoa ni muhimu; lakini je mkaka yeye hahitaji huo uhalali?
 
Kiimani hairuhusiwi kuishi kwanza halafu ndoa baadae na pengine hata kwa jamii unayoishi inaweza ikawa haikubaliani na uamuzi wa kuishi bila ndoa. Lkn nimeshuhudia ndoa kadhaa baada ya kufungwa maisha yanakua ndivyo sivyo yaani wanakua hawafanani kabisaa utadhani walilazimishwa kuoana. Mpaka wakati mwingine unatamani bora wangeishi kwanza halafu ndoa ingefuata baadae na hasa ukizingatia ndoa zetu hakuna kuachana . Nionavyo mimi kila uamuzi unaochukuliwa na wahusika una risk . Sasa sina jibu moja kama je ni sawa kuisi kwanza bila ndoa kwa sababu yoyote au kufunga ndoa kwanza ijapokua moyoni mwangu ningependa ndoa ianze na si kuishi kiuchumba. Tukumbuke kadiri tunavyokua pamoja ndipo tunapojuana zaidi mpaka vile vitabia vya ndani kabisa, sasa huenda ulimpenda sana mhusika lkn waweza katishwa tamaa na vitabia hivyo so unaamua kutofunga nae ndoa wakati tayari mlishaishi pamoja. Kumbe mgefunga ndoa kabla ya kuishi wote hivyo vitabia usingevijali. Choice zote mbili zinategemea uamuzi wa walengwa na zote zaweza kuwafaa au kuwaangusha.
Hapo uliposema ku rist nadhani ndio penyewe zaidi maana mtu anaweza ishi vizuri na mtu kabla ya ndoa kwa muda mrefu, wakaja wakaoana na wakaishi vizuri siku za mwanzo ila hali ikabadilika tena baadae, maana kuna vitu vingi vinaweza changia watu kubadilika, mf kipato, elimu, exposure, hata jamii inamzunguka mtu nk so kwa pande zote kuishi na mtu kabla ya ndoa au kutokuishi lolote laweza tokea baadae. Pia ni muhimu kujua kuwa ndoa sio paradiso muda wote ndio maana wengine wakibatiza kuwa ni umoja wa mataifa, ndio maana kwa kanisani unakula kiapo kuwa upo tayari kwa shida na raha, tena kabla ya kiapo mara nyingi watu wanaulizwa kama wamekuwa wakomavu kiakili na wana akili timamum maana wafungishaji wanajua kabisa hawa wanapokwenda kuna hasa na chanya, ila yote kwa yote wengi tunashangaa ndoa za sasahivi tunasahau kushangaa maisha ya sasahivi kabla ya ndoa, maana kwenye ndoa mara nyngi huonyesha matokeo ya maisha kabla ya ndoa, maana kuna tabia ni ngumu kuzianza baada ya ndoa, kama umalaya, uchoyo, ubinafsi nk
 
Back
Top Bottom