Mkuu ninaunga mkono hoja!
Kiongozi ukishagaragazwa mara mbili kwenye uchaguuzi mku, lazima ufubae na kukosa mvuto na kuhitajika sura mpya toka miongoni mwa wanachama kindakindaki kuziba pengo.
Mfano wa ving'ang'anizi ni kama kina Lipumba na wengineo kama hao.
Nilivyofuatilia kujua kwa nini kuwe na uking'ang'anizi wa madaraka na sura zile zile miaka nenda rudi, nikaelezwa kuwa viongozi hao huwa wanashiriki kwenye uchaguzi huku wakielewa pasi na shaka kuwa wanaenda kushindwa.
Kinachoendelea baada ya uchaguzi huwa ni manufaa yao(ruzuku) na mema mengine ya nchi.
Na kwamba Uenyekiti wa chama, kwao ni kama uenyekiti wa Sacoss, ukiupoteza mambo yako hayakunyokei kwa kukosa maslahi binafsi.
Na usipoparangana kwenye uchaguzi, chama kinaonekana ni cha kwenye laptop kinafutwa, sasa lazima uonekane kila "term" ya uchaguzi unachakarika kuzugia!
Tungelipata vichwa chipukizi na vyenye vision na misimamo kama ya Dr. Slaa wa Chadema, Sisiem sasa hivi wasingelala usingizi wa pono na kula likizo za kisiasa kama ilivyo sasa.
Chadema hii hii ikibadilisha safu ya uongozi, kinaweza kuitikisa sana Sisiem na kuchukua uongozi wa nchi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Lakini zikibakia sura zile zile za viongozi waandamizi, waalah piga ua hata wadurufu katiba mpya na kuboresha tume huru ya uchaguzi ili uchaguzi uwe huru na wa haki, lakini Chadema haitashinda aslani.