Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

mweongo

Member
Aug 23, 2010
62
228
Mnyonge mnyogeni haki yake apewe, Lissu leo amenigusa kwenye swala la lugha ya kufundishia. Jambo hili limekuwa mwiba kwenye elimu na maisha ya Watanzania miaka na miaka. Ni ukweli usiofichika kwamba lugha ya kufundishia ni tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa elimu. Magufuli mwenyewe ni mhanga Mawaziri wetu ni wahanga, Wabunge ni wahanga. Tuunge mkono chadema vijana wetu wapone.

Magufuli huongea kwa Kiswahili na kuhubiri kukuza Kiswahili si kwamba anakipenda sana. Sababu kubwa ni kwamba hajui English vizuri, Ingawa alikua mwalimu na PHD aliandika kwa kizungu. Yeye mwenyewe ni mfano mzuri wa halihalisi na shida tuliyonayo kwenye elimu yetu. Lakini cha kushangaza hajachukua hatua kundoa shida hii inayoliamiza tafa. Tundu lisu ameona tatizo na yupo tayari kulitatua.Tumunge mkono Lisu tuiokoe Tanzani.

Kwenye hili la elimu tuambiane ukweli. Hatutaendelea kwa kuhimiza vijana wawe wamachinga, wajaze mitaa wakichuuza vitu vya mchina wakati maduka yapo. Leo Barabara, Reli nk ni wageni wanajenga. kwani nani alienda kujenga Reli China au Korea? Kijana akitoka na zero form 4 utampeleka wapi? CCM imetuangusha kwa tangu Uhuru. Tanzania tunahitaji mabadiliko.

Vijana wetu wengi wanashindwa kupata maarifa ya kutosha mashuleni na vyuoni kwa sababu tu hawaelewi lugha inayotumika kuwafunza. Mfano;mtihani wa kitato cha 4 si mgumu kiasi cha zaidi ya nusu ya wahitimu kupata alama (division) 4 na 0.

Wawekezaji wakija Tanzania wanashindwa kupata wafanyakazi wanaoweza kuwasilana nao vizuri na wenye weledi na marifaya ya kutosha kwenye lugha. Matokeo yake wanaamua kuajiri Wakenya kwenye nafasi za juu. Uliza Managers kwenye makampuni makubwa hapa kwetu ni akina nani. Tunge mkono Lisu Tupate Tanzania mpya.

Tanzania itaweza tu kusonga mbele endapo tutaamua kuborosha elimu yetu itowe wasomi wenye viwango vya kimataifa na sio kupelka watoto shule kwa mazoea tu lakini watoka watupu.

Hakuna nchi yoyote Duniani amboyo ina mifumo miwili ya lugha za kufundia kama ilivyo kwa Tanzania. Wanachi waliona tatizo hilo wakamua kuazisha shule zinazofundisha kwa Kingereza ili kuziba pengo, hivyo Tanzania hakuna watoto wanafunzwa kwa Englishi na Wale wa Kiswahili.

Tundu Lissu na CHADEMA ameamua kulivalia njuga suala hli tumuunge mkono.
 
Kwa dunia ya leo lugha sio kigezo cha kumkwamisha mwekezaji kuwekeza na kupata matokeo chanya. Lissu mwenye amekaa Ubelgiji miaka 3, je alikuwa anaongea kifaransa, ki datchi au kijerumani? Kama unataka kuongea kiingereza au lugha yoyote ile ni juhudi zako mwenye zitakusaidia na utaongea tu.
 
Hopeless kabisa! Tulishasema Urais wa TZ mtausikia tu. TZ imefika hapa kwa sababu ya kuheshimu lugha yetu na mila zetu! Leo unataka kudharau lugha yetu kwa sababu ya kiingereza. Nchi zote za kiafrika zilizofanywa kama alivyosema mzungu huyu zinamatatizo ya kitamaduni sana tu!

IMG-20200608-WA0007.jpg
 
Problem is, not hearing anything of substance from anyone else that's running. All the talk is about bashing the other guy.
 
Ata kusoma uelewi kabisa. Ujerumani au China mtaala wao unasemaje? Kule ukitaka kusoma lugha tofauti ni wewe mkuu muwe mnatumia akili tulizopewa bure.
Wewe mwanasaccos hapo Afrika ya Kusini tu wameamua Kiswahili kuingizwa kwenye mtaala wao wakufundishia kwenye shule zao!! Wewe unadharau Kiswahili!!
 
Dah ndo nimestuka sa hivi kumbe tuna lugha mbili za kufundishia , aisee hata nchi zilizoendelea hawana mfumo huu na discrimination kwenye utoaji elimu , yaani eti kuna shule zinazoitwa, shule ya msingi za serikali zenyewe zinatoa elimu kwa lugha ya Taifa kiswahili, halafu kuna private school zenyewe kwa english, halafu mtoto akiingia secondary anaanza kusoma kwa kiingereza😂😂😂 kweli ni shida , Taifa tungeamua lugha moja tu kama lugha ya Taifa ni kiswahili watu wafundishwe kwa Kiswahili, shule ya msingi hadi chuo na sio kusumbuana kudakia dakia lugha, au kama vipi tuamue lugha ya kufundishia shule ya msingi hadi chuo iwe Kiingereza kwa wote hadi shule za serikali na sio watoto wa Taifa moja kutenganishwa na lugha, Tz ina systems mbovu sana za elimu ambazo kwa mtu wa kawaida kuzistukia ni kazi kwa sababu tumezikuta na tumeziishi tangu tukiwa watoto.

Pili: Mifumo ya kikoloni mashuleni
Waafrica tunapinga ukoloni lakini bado tunauishi kwa mfano :mambo ya kuchapana viboko mashuleni si yametoka kwa wakoloni na watumwa , mfumo huu sijui waafrika walichukua wapi
 
Ila kitumike kiswahili.

Au kuwe na shule aina 3.

Za english medium na kiswahili medium.

Pia Na kama zilizopo sasa.

Alafu tupime ufanisi wa kila medium.
 
English ni lugha inayotumika duniani kibiashara,kweye vyuo vikuu ndio maana watz wengi wanakosa kazi kwenye mashirika ya kimataifa sababu hawawezi kujieleza kiufasaha
Kama English ndo lugha ya kimataifa mkuu unabisha mifumo ya elimu kwako unaona ipo sawa? Hauoni Tanzania ina mifumo mibovu ya elimu, kwa mfano hauoni elimu ya msingi inaubaguzi kuna wanaofundishwa kwa kiswahili masomo, na kuna wa private wanafundishwa kwa english, kwa nini serikali isiamue elimu itolewe kwa lugha moja kama Kiingereza iwe kwa wote private na government school vivyo ivyo chuo ndo itakuwa fresh.
 
Tatizo la lugha Tanzania limekua kubwa, hata Kiswahili chenyewe kinatushinda. Ukisoma machapisho ya watu humu JF utagundua hata kiswahili hatujui kuandika vizuri. Najiuliza kama Taifa tunaelekea wapi? Hatupo kwenye English wala Kiswahili. majirani zetu ambao tunapenda kujlinganisha nao Wakenya. Siku hizi wanafusnwa kiswahili vizuri kuliko sisi. Wao wanamafaa kuliko sisi kwa vile wanajua Kingereza vizuri na Kiawahili wanakijua vyema.
 
Back
Top Bottom