Tuhuma za uongo dhidi ya PPF, wana JF tuache kukurupuka

Kumekuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya JF kuwa inawachafua watu binafsi, taasisi na vyama vya siasa kutokana na tuhuma za uongo. Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeanzisha tuhuma za uongo humu JF kuwa kuna ufisadi ndani ya PPF. Sidhani kama alikuwa ana nia mbaya, tatizo ni kuwa kuna ignorance kubwa sana. Watu huwa wanakurupuka na kutoa tuhuma zisizo sahihi.

Moderators wa JF kuruhusu matusi, kejeli na tuhuma za uongo kama hizi ndiyo chanzo cha malalamiko mengi dhidi ya JF. Kuna umuhimu wa free speech ila ni changamoto kwa JF kutoruhusu tuhuma zisizokuwa na msingi, kwani hatimaye JF itapoteza credibility na kuonekana kuwa ni kichaka cha kutoa tuhuma za kutungwa na kashfa na si "The Home of Great Thinkers" kama inavyojitamba.

Mzee Mwanakijiji anayeheshimika sana huku JF alikuja na post inayosema -- "MALIPO YA Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption"

Imekuja kubainika kuwa zile tuhuma za malipo kwa menejimenti ya PPF zilizoanzishwa na Mzee Mwanakijiji humu JF ambaye aliziita kimakosa kuwa ni "corruption" na kudakiwa na Zitto Kabwe na kamati yake ya POAC, si tuhuma sahihi.

Kuhusu hii post mpya yenye kichwa cha habari: "Hivi SSRA ni kichaka cha mafisadi wa PPF? SSRA Haitaipendelea PPF kwenye ufisadi na uizi?", huu ni uzushi na udaku mtupu.

Kazi zilitangazwa SSRA na zikafanywa interview pale. Ukweli ni kuwa wafanyakazi kutoka mifuko mbalimbali ya pensheni, ikiwemo PPF, NSSF, PSPF, LAPF na kutoka sekta ya fedha waliomba kazi SSRA na kulikuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya interview, waliokuwa wafanyakazi kadhaa wa PPF wakapita na kushinda nafasi za kazi SSRA. Pengine hii ni sifa kwa PPF kuwa na wafanyakazi wenye sifa kubwa na shirika lenyewe kuheshimika mpaka wakapata nafasi za kazi SSRA.

These are the real facts. Hakuna ufisadi wowote PPF kama inavyodaiwa humu JF kila mara. Ukweli ni kuwa mfuko huu umepewa "clean audit opinion" na CAG na good governance award kwa nchi za Afrika.

Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amewahi kuwa director general wa NSSF na hivyo anafahamu vizuri uendeshaji wa mifuko ya pensheni Tanzania amesema kuwa malipo hayo yanayolalamikiwa sana PPF ni sahihi na yanafanywa na kila shirika la umma tangu miaka ya 1990s. Mkulo amesema kuwa malipo hayo ya gratuity na group endowment scheme yamepitishwa kisheria na serikali, hivyo PPF haijavunja sheria yoyote. Hakuna rushwa, wizi wala ubadhirifu wowote wa pesa.

Jamani wana JF tuache kukurupuka na kuharibu credibility ya JF kuifanya ionekane kama jukwaa la kashfa, matusi, kejeli, uongo na tuhuma zisizokuwa na msingi.

Mkulo defends PPF managers' payments

By ALVAR MWAKYUSA in Dodoma, April 20, 2011

MINISTER for Finance Mr Mustafa Mkulo has said the gratuity and endowment payments to management of Parastatal Pension Fund (PPF) were in line with regulations.

The minister made the clarification in the National Assembly on Wednesday evening while contributing to reports by three parliamentary committees, presented to the House earlier in the morning.

"The payments are in accordance with the decision of the PPF Board of Trustees in 2002. The management of the fund operates on a contractual basis and they are entitled to the gratuity.

PPF employees are of two categories, permanent and pensionable and those on contracts," elaborated the minister.

Apart from gratuity, the fund has in place arrangement for group endowment to all its employees which is paid to employees who have completed their terms of service, retiring, retrenched or deceased.

"The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law," maintained the minister.

He said the endowment payments are made to all employees of the pension fund, adding that they were designed in the early 1990s under the then National Insurance Corporation (NIC).

If the payments are to be stopped then the management of PPF has to be hired on permanent basis, said Mr Mkullo.

The Parliamentary Public Organisations Account Committee (POAC) had recommended that the Controller and Auditor General (CAG) and the Treasury Registrar intervene in the matter, saying the payment system gave room to double payment in the form of gratuity and endowment benefits.

Source: (Daily News | Mkulo defends PPF managers' payments)

Najua watakurupuka watu humu JF na kusema nimetumwa, nimehongwa, kwa kuitetea PPF kama kawaida ya watu kukurupuka. Lakini tusimame kwenye facts na mambo yaliyo sahihi. Tujenge hoja kwa kutumia facts na si matusi, kejeli na tuhuma za kutungwa.

Ngao One,

Without research, no right to speak.

Inawezekana ukawa unajaribu kutaka kudodosa ili kujua ukweli.

Ukweli ni kuwa Mustapha Mkulo kalidanganya Bunge na waheshimiwa wabunge. Mkulo bila kufanya utafiti, kakurupuka kwa kudanganywa na William Erio kuwa malipo haya ni sahihi.

Utaratibu wa Group endowment upo PPF na hauna utata, tatizo waliolipwa sio walengwa. Utaratibu huu ulianzishwa ili kutoa golden shake hand kwa wafanyakazi wa kudumu pale wanapostaafu kwa kufikisha miaka 55.

Wafanyakazi wa mikataba wana malipo yao yanayoitwa gratuity. Kosa lililopo ni hawa wakurugenzi ambao ni wa mikataba kuamua kujilipa pia group endowment ambayo sio haki yao. hili ndilo kosa. Mkulo anasikisha na sijui CPA yake kama ni sahihi, malipo kutozwa kodi sio kigezo cha uhalali.

Mkulo na serikari yake wanatakiwa kupata ukweli toka kwa wafanyakazi wasio wa mkataba hasa hasa aliyekuwa Mhasibu Mkuu mwaka 2008. Huyu anajua vizuri. Pia serikali wasome majibu ya wakurugenzi kwa Bodi ya wadhamini vikao vya May, 2008 na June 2008 wataona jinsi majibu ya kila wakati yanavyotofautiana.

Serikari pia iangalie malipo ya Mr. David Mattaka alipokuwa kwenye mkataba, ione kama alilipwa group endowment. Mattaka alilipwa 25% gratuity kwa miezi 19 tu aliyofanyia kazi. Kama alistahili group endowment, kwa kipindi cha mkataba mbona hakupewa, apewe sasa kama aliibiwa.

Mkulo anaposema If the payments are to be stopped then the management of PPF has to be hired on permanent basis, kwahiyo waendelee kuiba kwa kuwa Waziri anaogopa kuwaajiri kwenye mfumo wa kudumu.

Naandaa majibu mazuri kwa mpangilio na ushahidi kuwa PPF Management wameliibia shirika.
 
Ngao One,

1. Mataka sio wa kwanza kunufaika. Mkulo alisema kweli kabisa kuwa Mataka alilipwa wakati anastaafu. Alistaafu kutoka ajira ya kudumu, akalipwa group endowment. Akaajiliwa kwa mkataba akalipwa gratuity ya miezi 19 aliyofanyia kazi. Sasa hawa wakurugenzi wa sasa iweje walipwe group endowment na gratuity vyote kwa pamoja kila baada ya miaka mitatu?

2. Mkulo amesema alilipwa, huu ni uongo, NSSF hawana huu utaratibu, na kama walikuwa nao, alilipwa wakati wa kustaafu sio mwisho wa mkataba.

3. Hivi kwa nini serikali, PCCB, CAG wanawauliza wale wale walioiba kuwa ni sahihi walichokiiba? au wanaonewa?. Unatarajia wajibu nini.

4 Unasema Ingeleta tija kama tungeweka juhudi kupinga sera/utaratibu huu wa malipo serikalini na tudai mabadiliko, si kutoa tuhuma hewa za "corruption" dhidi ya shirika moja hili la PPF bila ushahidi wowote.

USHAHIDI unatolewa wewe unabisha tukusaideje

Ngao one kama si mmoja wao basi umehongwa au ni mdokoaji sehemu nyingine ambako nako tutafika kukukamata.

MUDA utafika ambapo UKWELI utakapo onekana na ndio utakaowaweka HURU WOTE.

5. Mustafa Mkulo ni kati ya wakurugenzi walioiibia PPF wakati wa kustaafu. Alikuwa na mshahara mdogo marupurupu kibao. Alipoona anakaribia kustaafu akaunganisha na kuwa mshahara mmoja mkubwa na akastaafia huo na kutumika na PPF kumlipia mafao. Ndio maana PPF wakabadili taratibu wa kutumia mshahara wa mwisho na kutumia wastani wa mishahara sitini ya mwisho na kupata wastani. Je huyu sio fisadi?

Ndiyo yaleyale ya kukurupuka. Kwa vile mimi nimehoji hizo tuhuma za "corruption" na kutaka kuona ushahidi, basi na mimi napokea hizo gratuity au nimetumwa. Hayo ni majibu mepesi. Mkulo ameeleza kuwa malipo haya ni "halali" kwa mujibu wa utaratibu wa serikali. Tena mtu wa kwanza kunufaika nayo alikuwa David Mattaka wakati anastaafu PPF.

Ingeleta tija kama tungeweka juhudi kupinga sera/utaratibu huu wa malipo serikalini na tudai mabadiliko, si kutoa tuhuma hewa za "corruption" dhidi ya shirika moja hili la PPF bila ushahidi wowote.

Kama tuko serious, tufanye mjadala mpana kuhusu matumizi mabaya ya pesa kwenye mashirika ya umma yote (si PPF tu) na serikalini, Mfano, tupinge pia Bunge kupitisha azimio hivi majuzi kuwa Wabunge wote sasa wakopeshwe pesa za kununulia magari, kufanya service kwa magari na kununulia fenicha nyumbani kwa mashart yafuatayo:

1. Serikali kutoa msamaha wa 50% kwa mkopo wa wabunge (eg. Mheshimiwa akikopa 50m/-, atarejesha 25m/- tu)
2. Mkopo kutolewa bila ya riba kwa Wabunge

Walimu, polisi, manesi, mbona hawapewi upendeleo huu kama wabunge?
 
Mimi sielewi kwa nini PPF na sasa SSRA kama inavyodaiwa iajiri Mganda au raia mwingine wowote wa nje kama Head of IT wakati kuna Watanzania wengi sana wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo. Ni muhimu kwa wakuu wa mashirika ya umma na binafsi na waajiri wengine kuwa na uzalendo na kuajiri Watanzania wenye sifa. Sidhani kama huyo Mganda ana sifa exceptional/unique ambazo hakuna Mtanzania mwenye sifa hizo. Hapo ni kuangalia sheria za uhamiaji zinasemaje. Kuna udhaifu kwa Idara ya Uhamiaji kuruhusu wageni kuajiriwa hovyo. Pia, wafanyakazi wenye data SSRA wapeleke taarifa Idara ya Uhamiaji kuhusu tuhuma hizo kuwa Mganda alitokea PPF akaajiriwa SSRA kinyume na sheria.
...Jamani watanzania kumbukeni tumeshasaini Protocol na Nchi wenzetu wa Jumuia ya Africa Mashariki ambayo sasa ni Ruksa Mwananchi mwenye vigezo kufanya kazi katika mojawapo ya Nchi yoyote katika hizo Nchi Tano za EAC. Soma Attachment hapo chini
 
Attachments

  • Annex on the Free Movement of Workers.pdf
    452.4 KB · Views: 30
Hiyo sheria haifai kabisa inatakiwa ifanyiwe marekebisho,inaumiza wafanya kazi kwa kweli.
 
Mkuu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, aliongea Bungeni na kusema kuwa: "The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law."

Wewe umesema kuwa malipo ya PPF ni "rewarding and defending corruption." Hii inaleta hisia potofu kuwa kuna wizi na rushwa kubwa PPF, kumbe malipo hayo ni kwa mujibu wa sheria na sera za serikali. Malipo haya yanafanywa kwenye mashirika karibu yote makubwa ya umma hapa Tanzania, si PPF tu.

Ingeleta tija zaidi kama tungejadili sera hii ya serikali ya malipo ya gratuity and endowment kwenye mashirika ya umma yote kwa ujumla wake na kushauri kama yafutwe au yarekebishwe badala ya kuinyooshea kidole PPF tu kila siku na kujenga hisia potofu kuwa kuna ufisadi mkubwa huko wakati ukweli ni kuwa malipo hayo yanafanywa kwa kufuata utaratibu uliopo. Hapa ni vigumu kwa mtu kutoamini kuwa kuna witch-hunting inafanyika dhidi ya PPF au watu wanakurupuka tu na tuhuma za uongo.
Hivi ninyi vibaraka vya Chama cha Magamba mpaka uone nini ndo uamini kuwa kuna wizi sehemu fulani? Hapa sijaona logic ya wewe kukaa na kukomaa na hoja yako hii ambayo kwa mtu yoyote tu aliyewahi kupata hata elimu ya msingi tu atakudharau toka vidoleni hadi utosini kwa kutetea malipo hayo. hata kama yapo kisheria, sheria zingine ukumbukwe zinapitishwa kwenye "DARK MARKET" ili ziwanufaishe CCM kwenye kampeni. Ikumbukwe kuwa wabunge wenu wengi ni wajumbe wa bodi za mashirika hayo na hivyo kila wanapotaka kutunga sheria za mafao hutaka yawanufaishe wao. I hate any process done by CCM members of Parliament under "Dark Market" for the purpose of favouring themselves instead of the majority poor Tanzanians.
 
......[COLOR=blue said:
malipo hayo ni kwa mujibu wa sheria na sera za serikali. Malipo haya yanafanywa kwenye mashirika karibu yote makubwa ya umma hapa Tanzania[/COLOR], si PPF tu.

Ingeleta tija zaidi kama tungejadili sera hii ya serikali ya malipo ya gratuity and endowment kwenye mashirika ya umma yote kwa ujumla wake na kushauri kama yafutwe au yarekebishwe ....

I agree with you na pia sipingani sana na Mwanakijiji either. Kwa taarifa za uhakika nilizonazo waliozitunga hizi sheria wakati huo (walikuwepo ma-CEO wa mashirika ya umma etc) walizitunga wakiangalia zitawanufaishaje wao lakini hawakuangalia effect yake in the future. Kwa mtizamo huo, sasa hivi ndio imekuja kuonekana effects zake kwamba kwa mujibu wa sheria hizo mtu anaweza kupokea billions kwa mfumo huo wa malipo na hivyo itafika wakati PPF itabidi ifilisike/ife. Taarifa za uhakika ni kwamba bosi wa PPF ameshaiandikia na kulalamika kwa wizara husika na kutuma copy kwa raisi mwenyewe not once not twice lakini hakuna kinachofanyika. Kuna mawili hapa:1) labda wizara husika haielewi what to do (Lots of vihiyo in place), au(2) someone anazuia mabadiliko ya haraka yasifanyike. Nafikiri bosi wa PPF akibanwa vizuri atatoa vidhibitisho vya barua aliyomuandikia bwana mkubwa kuhusu hii issue. So I totally agree with you on this issue. I also think Mwanakijiji anatendea haki watanzania anavyoipigia kelele hii issue kwasababu bosi wa PPF, and his inner circe wanaogopa ku-speak loud maana issue imeshafika inapohitajika lakini no body acts. In other words bila wananchi kuelewa kuhoji nobody will act. Tunahitaji kufanya kazi kwa transparency ilitujue makosa yako wapi, yalifanyika vipi, na tunasahihisha vipi.
 
Naomba nijieleze vizuri pengine utapata kunielewa. Sawa, MMM anaweza kuwa si mtu wa kwanza kuleta tuhuma za PPF humu JF lakini thread aliyeipost ni moja ya muendelezo wa tuhuma hizo. MMM na wengine wameituhumu PPF kwa corruption, wizi, etc, lakini sijaona any evidence ya hayo. Nimeona invoice tu za malipo kwa baadhi ya directors. Lakini ukweli kuwa malipo hayo (pamoja na kwamba ni makubwa) ni malipo halali kutokana na utaratibu wa serikali uliowekwa kuhusiana na gratuity na group endowment scheme.
Malipo haya yanafanywa na mashirika mengi ya umma na si PPF tu tangu enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi (Mzee wa Rukhsa) miaka ya 1990s ndiyo maana Mkulo akatetea malipo haya Bungeni.

Hoja ni kuwa badala ya kukurupuka na kuwashutumu PPF kwa "corruption" tuangalie utaratibu huu mzima wa malipo haya ili tushinikize ufutwe au urekebishwe. Kama watu wanatoa tuhuma za "corruption" basi leteni huo ushahidi.

So far sijaona ushahidi wowote kuwa kuna ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na wizi ndani ya PPF kama inavyodaiwa humu ndani ya JF na baadhi ya watu. Vinginevyo tuhuma hizi zinaonekana kama udaku tu.

Kuhusu Mganda, mimi napinga vikali wageni kuajiriwa kwenye nafasi ambazo wako Watanzania wengi, tena wenye uwezo mkubwa zaidi, ambao wanaweza kuzifanya. Kama PPF waliajiri Mganda kinyume na sheria hilo ni kosa. Pia hao wafanyakazi wa PPF waliojua hili kwa nini hawakutoa taarifa uhamiaji au kwenye kamati za Zitto Kabwe ya POAC?
nafikiri tatizo ni wewe umeshindwa kuelewa nini maana ya coruption. coruption inaweza kuwa katika mifumo mingi ya wazi na isiyo ya wazi, kwa mfano wewe mkurugenzi ukaajiri mtu sema uwezo wake ni mdogo kuliko mwingine, lakini huyu mwenye uwezo mdogo ukampaa mshahara mkubwa au ukawa una mpa safari , mafunzo nk dhidi ya wengine, hii wewe utaita nini, ingawa sheria au taratibu za kazi zina ruhusu hiyo safari.. mafunzo au mkurugenzi kukubaliana na mfanyakazi wake huo mshahara.
 
halafu kwa kuongezea kidogo bwana/bibi ngao one kwanini unafikiri taratibu za kihasibu zinataka malipo yote kwa wakurugenzi yawekwe au kutangwazwa /reported separately na mkagunzi mkuu ayapitie? ili wanachama au wanahisa waweze ya kuyaona kwa jicho la pekee na kama kuna hoja ya kuulizawafanye hivyo, sasa wewe unayeona hayo malipo, siju mkulo kayaeleza, oh mashirika yote , au sheria inaruhusu nk nk, kwani na wewe usilete sema invoice /voucher za mashitika hayo ili kuonyesha uhalali wake, na nafasi ya wanahisa/wanachama kuhoji hayo malipo yake? ai ni siri ya walipwa na mkaguzi wao na bodi ya hilo shirika.
 
Watanzania tuna kazi kubwa sana na watu wa type hii, tena wapo wengi tu katika kizazi hiki, wamezoa zulumati mpaka wanapata ujasili wa kuja hazalani kuhalisha mambo ambayo ni immoral kwenye jamii tena bila woga as if kinachofanyika ndiyo stahili yao hata kama kina athari kubwa kwa maskini wa nchi hii.

Hoja ni kuwa badala ya kukurupuka na kuwashutumu PPF kwa "corruption" tuangalie utaratibu huu mzima wa malipo haya ili tushinikize ufutwe au urekebishwe. Kama watu wanatoa tuhuma za "corruption" basi leteni huo ushahidi.

So far sijaona ushahidi wowote kuwa kuna ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na wizi ndani ya PPF kama inavyodaiwa humu ndani ya JF na baadhi ya watu. Vinginevyo tuhuma hizi zinaonekana kama udaku tu.

Kuhusu Mganda, mimi napinga vikali wageni kuajiriwa kwenye nafasi ambazo wako Watanzania wengi, tena wenye uwezo mkubwa zaidi, ambao wanaweza kuzifanya. Kama PPF waliajiri Mganda kinyume na sheria hilo ni kosa. Pia hao wafanyakazi wa PPF waliojua hili kwa nini hawakutoa taarifa uhamiaji au kwenye kamati za Zitto Kabwe ya POAC?[/QUOTE]
 
These are the real facts. Hakuna ufisadi wowote PPF kama inavyodaiwa humu JF kila mara. Ukweli ni kuwa mfuko huu umepewa "clean audit opinion" na CAG na good governance award kwa nchi za Afrika.
Cooked Clean audit report ni moja ya njia zinazotumika kuficha corruption na uozo kwenye mashirika. Kabla ya EPA kuibuliwa BOT ilikuwa na clean audit report ni baada ya tuhuma kuwa kwenye public true clean Audit ikaonyeshsa ukweli kuwa kuna dirty transaction.

Hatuatki watu na viongozi walisoma kujua jinsi ya kuchota mafedha kihalali .tunataka watu waadilifu wanaweza kujua kutofautisha uhalali na uadilifu.

Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amewahi kuwa director general wa NSSF na hivyo anafahamu vizuri uendeshaji wa mifuko ya pensheni Tanzania amesema kuwa malipo hayo yanayolalamikiwa sana PPF ni sahihi na yanafanywa na kila shirika la umma tangu miaka ya 1990s.
Again usahihi wa kitu haumanishi ni uadilifu. I think watendaji wengi neno uadilifu/ ethics wamelisahau.

Nakupa mfano moja wa kisheria.
Fundi bomba kaenda kutengeneza bombalimeziba kwa bibi fulani. kangundua tatizo anamwambia bibi yule kurekebisha atahitaji 5 Mil. sababu bibi haelewi mambo ya ufundi na ana mahela na pesa anamwambia twende benki nikakuchukulie .

Kufika beki bibi anammwabia cashier anahitaji 5 mil. Cashier anamuuliza za nini. Bibi anamwambia za kutengenza bomba.

Cashier anapiga simu polisi kuwaambia kuwa kuna bibi anataka kuibiwa. ........ simalizii ilikuwaje kuwa judge mwenyewe

Hapo unajifunza nini.?

kisheria inawezekana yule fundi hana kosa ni kwani makubaliano ya malipo ni kati yake na bibi na bibi kakubali na anasema hana tatizo na hayo malipo.Lakini Kiadilifu huyo fundi amekuwa ni tapeli na mwizi na corrupt

NB.
Pamoa na ujuzi wetu wa sheria, ufundi na taaluma tulizonazo bado tunakiwa ku observe moral and ethical resposibility.So kwa kuwa yaafanyika toka miaka ya 1990 na kwa kisheria yanaubalika haimaanishi moraly yako right.

Ngao One said:
Ndio matatizo ya wabongo wanakimbilia kuwalaumu watu wanaopokea mafao badala ya kulaumu utaratibu

Shirika la pensheni ni shirika nyeti wacha walipwe accordingly wanafanya kazi kubwa ya kutunza pensheni zetu .

Na ni watu qualified ndio maana hajapewa Baba Enoki hizo position, they deserve. mheshimiwa alisema tuache wivu wa kike.
Yah wabongo lazima tuwalaumu sababu ni viongozi waadilifu ndio wanatakiwa kwanza kuyaona matatizo haya. Ni yale yale ya wabunge kujipangia mishahara yao. Hakuna mbunge aliyewai kupendekeza iundwe taaisis huru ya kuratibu malipo yao. Simply no matter uwe na phd ngapi za fani ukikos auadilifu hauna manufaa kwa jamii.
 
Kwa kuwa mleta mada kashajijibu kwenye mistari mitatu ya mwisho isipokuwa mmoja wa mwisho kabisa,mi namwambie kajijibu na sisi wanaoishi chini ya dola moja kwa siku tunamwombea aishi na ujasiri huo huo wa kutetea na kufadhili utapeli na ufisadi wa watawala wetu!
 
Naomba nijieleze vizuri pengine utapata kunielewa. Sawa, MMM anaweza kuwa si mtu wa kwanza kuleta tuhuma za PPF humu JF lakini thread aliyeipost ni moja ya muendelezo wa tuhuma hizo. MMM na wengine wameituhumu PPF kwa corruption, wizi, etc, lakini sijaona any evidence ya hayo. Nimeona invoice tu za malipo kwa baadhi ya directors. Lakini ukweli kuwa malipo hayo (pamoja na kwamba ni makubwa) ni malipo halali kutokana na utaratibu wa serikali uliowekwa kuhusiana na gratuity na group endowment scheme.
Malipo haya yanafanywa na mashirika mengi ya umma na si PPF tu tangu enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi (Mzee wa Rukhsa) miaka ya 1990s ndiyo maana Mkulo akatetea malipo haya Bungeni.

Hoja ni kuwa badala ya kukurupuka na kuwashutumu PPF kwa "corruption" tuangalie utaratibu huu mzima wa malipo haya ili tushinikize ufutwe au urekebishwe. Kama watu wanatoa tuhuma za "corruption" basi leteni huo ushahidi.

So far sijaona ushahidi wowote kuwa kuna ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na wizi ndani ya PPF kama inavyodaiwa humu ndani ya JF na baadhi ya watu. Vinginevyo tuhuma hizi zinaonekana kama udaku tu.

Kuhusu Mganda, mimi napinga vikali wageni kuajiriwa kwenye nafasi ambazo wako Watanzania wengi, tena wenye uwezo mkubwa zaidi, ambao wanaweza kuzifanya. Kama PPF waliajiri Mganda kinyume na sheria hilo ni kosa. Pia hao wafanyakazi wa PPF waliojua hili kwa nini hawakutoa taarifa uhamiaji au kwenye kamati za Zitto Kabwe ya POAC?
PPF is wrotten, kutetea kwa juma rosa adamu au hawa hakuusafishi

acha upumbavu na fincha upumbavu wako
 
MMM anaweza kuwa si mtu wa kwanza kuleta tuhuma za PPF humu JF lakini thread aliyeipost ni moja ya muendelezo wa tuhuma hizo.
Rejea maelezo yako mwenyewe uone kama haya unayosema ni kweli, maana inaonekana wazi unamshambulia MMkJ na sasa unabadili msimamo. Je unayoandika ni maneno yako au umetumwa?

MMM na wengine wameituhumu PPF kwa corruption, wizi, etc, lakini sijaona any evidence ya hayo. Nimeona invoice tu za malipo kwa baadhi ya directors. Lakini ukweli kuwa malipo hayo (pamoja na kwamba ni makubwa) ni malipo halali kutokana na utaratibu wa serikali uliowekwa kuhusiana na gratuity na group endowment scheme. Malipo haya yanafanywa na mashirika mengi ya umma na si PPF tu tangu enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi (Mzee wa Rukhsa) miaka ya 1990s ndiyo maana Mkulo akatetea malipo haya Bungeni.
Sijui kumtaja Rais Mwinyi umelenga nini, ingekuwa busara ungetaja mwaka yalipoanza hayo malipo, nina shaka unataka kujificha au kuficha jambo kwa kumhusisha Mwinyi. Hili tulishaliona siku nyingi na tumeliweka sawa, kwa bahati mbaya unataka kuturudisha nyuma.Tunaona unapokwenda kwenye udini! hatuna interest na mambo hayo,kwamba kuna uhalali kwasababu tu...
Hoja ni kuwa badala ya kukurupuka na kuwashutumu PPF kwa "corruption" tuangalie utaratibu huu mzima wa malipo haya ili tushinikize ufutwe au urekebishwe. Kama watu wanatoa tuhuma za "corruption" basi leteni huo ushahidi
.
Sijui unajua maana ya corruption. Unachojua ni kuwa corruption lazima iwe katika karatasi au pesa za PCCB basi. Corruption inaweza kuwa indirect or under the influence. Nenda kasome kwa undani maana ya corruption, unayoijua ni too shallow.
So far sijaona ushahidi wowote kuwa kuna ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na wizi ndani ya PPF kama inavyodaiwa humu ndani ya JF na baadhi ya watu. Vinginevyo tuhuma hizi zinaonekana kama udaku tu.
Sasa unasema malipo ni makubwa na yajadiliwe ili ikiwezekana yapunguzwe,ni maneno yako mwenyewe, halafu unasema huoni ubadhirifu, haa! unafahamu nini unachoongelea ndugu yangu!
Kuhusu Mganda, mimi napinga vikali wageni kuajiriwa kwenye nafasi ambazo wako Watanzania wengi, tena wenye uwezo mkubwa zaidi, ambao wanaweza kuzifanya. Kama PPF waliajiri Mganda kinyume na sheria hilo ni kosa. Pia hao wafanyakazi wa PPF waliojua hili kwa nini hawakutoa taarifa uhamiaji au kwenye kamati za Zitto Kabwe ya POAC
Huyu inaweza kuwa ameajiri kihalali kama malipo yalivyo halali kwa mujibu wa maelezo yako!!! sasa kinakukera kitu gani, unaendelea kujichanganya tu. Hapo mwanzo umekiiri hujui Mganda ni nani, sasa unabadilika na kusema unakerwa. Hivi huoni hata ajira hiyo inaweza kuwa corruption!

Jenga hoja kwa kuzingatia hoja. Jaribu kuangalia mambo kwa definiition pana zaidi ya ile moja unayoiona katika dictionary. Acha kuchomeka hoja za 'za kitabaka' ili kujenga uhalali usiokuwepo.
Na jitahidi kujenga hoja zako, kwasababu za kutumwa zitakusababishia usumbufu.
 
Guys Mganda anayelalamikiwa ni mwanamke na ameolewa na mtz,somebody mwita from tarime. Kisheria yeye ni mtz na ana haki zote za kuajiriwa na b4 that alikuwaana piga lecture pale aru na udsm...
Hizo sheria wanazotunga na kuzibadilisha kila ck ndo zinazotukula mchana kweupe...
 
Najua watakurupuka watu humu JF na kusema nimetumwa, nimehongwa, kwa kuitetea PPF kama kawaida ya watu kukurupuka. Lakini tusimame kwenye facts na mambo yaliyo sahihi. Tujenge hoja kwa kutumia facts na si matusi, kejeli na tuhuma za kutungwa.

Hujatoa ushahidi wowote wa maana kuonyesha kwamba PPF hakuna ufisadi.

Tukuamini kwa maneno yaliyotungwa tuu? Haiwezekani. Halafu huyo Mkulo unayemwongelea possitively,to me he is just another fisadi. Unakumbuka comments zake alizotoa kuhusu zile hela za EPA, pale ndipo nilipomdharau kabisa.

Halafu unasema pia kuwa CAG ame endorse financial report ya PPF, mbona ame-endorse nyingi tu ambazo ni mbovu?

Thread yako frankly haina substance kabisa,please go back to the drawing board.
 
Zuhura/sakia Meghji alidai amedanganywa na Balali , akajibi query eti ni matumizi ya usalama wa taifa mwishowe akawafukuza mauditor, je hakuwa ndani ya sheria? na je kulikuwa hakuna huo uwozo uliongelewa? huyu huyu sakia tunasikia kwenye kamati yao anasema aazizi ostam ni muongo alimdanganya kuhusu kagoda, na watu kama wewe mtakubaliana kwa sababu sheria, hakuna ushahidi, kauli ilitolewa bungeni ipo kwenye hansard nk nk. fikiria vitu kwa mapana na marefu. inabidi ukuwe kijana/bibi/bwana nk na hilo jina la ngao naona ubadilishe maana unashusha hadhi ya ngao.
 
Mkuu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, aliongea Bungeni na kusema kuwa: "The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law."

Wewe umesema kuwa malipo ya PPF ni "rewarding and defending corruption." Hii inaleta hisia potofu kuwa kuna wizi na rushwa kubwa PPF, kumbe malipo hayo ni kwa mujibu wa sheria na sera za serikali. Malipo haya yanafanywa kwenye mashirika karibu yote makubwa ya umma hapa Tanzania, si PPF tu.

Ingeleta tija zaidi kama tungejadili sera hii ya serikali ya malipo ya gratuity and endowment kwenye mashirika ya umma yote kwa ujumla wake na kushauri kama yafutwe au yarekebishwe badala ya kuinyooshea kidole PPF tu kila siku na kujenga hisia potofu kuwa kuna ufisadi mkubwa huko wakati ukweli ni kuwa malipo hayo yanafanywa kwa kufuata utaratibu uliopo. Hapa ni vigumu kwa mtu kutoamini kuwa kuna witch-hunting inafanyika dhidi ya PPF au watu wanakurupuka tu na tuhuma za uongo.

Hujui kuna sheria za kifisadi? Ndio hizo kama ulikuwa hujui
 
Kumekuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya JF kuwa inawachafua watu binafsi, taasisi na vyama vya siasa kutokana na tuhuma za uongo. Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeanzisha tuhuma za uongo humu JF kuwa kuna ufisadi ndani ya PPF. Sidhani kama alikuwa ana nia mbaya, tatizo ni kuwa kuna ignorance kubwa sana. Watu huwa wanakurupuka na kutoa tuhuma zisizo sahihi.

Moderators wa JF kuruhusu matusi, kejeli na tuhuma za uongo kama hizi ndiyo chanzo cha malalamiko mengi dhidi ya JF. Kuna umuhimu wa free speech ila ni changamoto kwa JF kutoruhusu tuhuma zisizokuwa na msingi, kwani hatimaye JF itapoteza credibility na kuonekana kuwa ni kichaka cha kutoa tuhuma za kutungwa na kashfa na si "The Home of Great Thinkers" kama inavyojitamba.

Mzee Mwanakijiji anayeheshimika sana huku JF alikuja na post inayosema -- "MALIPO YA Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption"

Imekuja kubainika kuwa zile tuhuma za malipo kwa menejimenti ya PPF zilizoanzishwa na Mzee Mwanakijiji humu JF ambaye aliziita kimakosa kuwa ni "corruption" na kudakiwa na Zitto Kabwe na kamati yake ya POAC, si tuhuma sahihi.

Tuhuma zako kuhusu hizo tuhuma zinahitaji pia kusomwa kwa tahadhari.
Umenishangaza sana kunijulisha kwamba Kumbe Zitto POAC hawana uwezo wa kupata nyaraka, taarifa na ripoti moja kwa moja, wanazunguka nchi nzima, kisha wanaandika ripoti kwa kutumia JF!!!
Nina maswali mengi sana kuhusu taarifa yako, mengi kuliko niliyoyapata niliposoma taarifa ya MM.
 
Mimi sielewi kwa nini PPF na sasa SSRA kama inavyodaiwa iajiri Mganda au raia mwingine wowote wa nje kama Head of IT wakati kuna Watanzania wengi sana wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo. Ni muhimu kwa wakuu wa mashirika ya umma na binafsi na waajiri wengine kuwa na uzalendo na kuajiri Watanzania wenye sifa. Sidhani kama huyo Mganda ana sifa exceptional/unique ambazo hakuna Mtanzania mwenye sifa hizo. Hapo ni kuangalia sheria za uhamiaji zinasemaje. Kuna udhaifu kwa Idara ya Uhamiaji kuruhusu wageni kuajiriwa hovyo. Pia, wafanyakazi wenye data SSRA wapeleke taarifa Idara ya Uhamiaji kuhusu tuhuma hizo kuwa Mganda alitokea PPF akaajiriwa SSRA kinyume na sheria.

Kwa hiyo unakubali Mganda anakula mamilioni yetu hapo?
 
Back
Top Bottom