Tuhuma za uongo dhidi ya PPF, wana JF tuache kukurupuka

Tuhuma za uongo dhidi ya PPF, wana JF tuache kukurupuka

Mimi sielewi kwa nini PPF na sasa SSRA kama inavyodaiwa iajiri Mganda au raia mwingine wowote wa nje kama Head of IT wakati kuna Watanzania wengi sana wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo. Ni muhimu kwa wakuu wa mashirika ya umma na binafsi na waajiri wengine kuwa na uzalendo na kuajiri Watanzania wenye sifa. Sidhani kama huyo Mganda ana sifa exceptional/unique ambazo hakuna Mtanzania mwenye sifa hizo. Hapo ni kuangalia sheria za uhamiaji zinasemaje. Kuna udhaifu kwa Idara ya Uhamiaji kuruhusu wageni kuajiriwa hovyo. Pia, wafanyakazi wenye data SSRA wapeleke taarifa Idara ya Uhamiaji kuhusu tuhuma hizo kuwa Mganda alitokea PPF akaajiriwa SSRA kinyume na sheria.

Wanalinda mikata nan mfumo mzima wa kumbukumbu na document zisifuje kwa watu ukizingatia ukiwekwa wewe mzawa siri itavuja like hizi kampuni zetu za kigeni ni za vigogo ila wakiweka watukutoka nje wanalinda maslai yao kifupi wapo kwa maslai ya watu wachache.
 
This is when Zitto becomes a star, anajenga hoja vizuri, mkullo anabwabwaja tu na kile kipara kama yai
 
Mimi nafikiri ndugu yangu Ngao One umekosea sana kutoa hii shutuma.

Sikulaumu ila najua hujapata kuwafahamu vizuri watu wenye akili wanapotaka kuiba. Kama tutaenda kwa mtazamo wako, basi nchi itaendelea kufilisika kwa kasi kubwa. Je, unafikiri MAFISADI hawana vielelezo vizuri vya kujihalalishia kujichotea pesa? Mara ngapi wanatetewa na Wabunge, Mawaziri mpaka hata Mh. Rais kwa kutumia vifungu vya sheria.

Pia wewe inaonyesha siyo muathirika wa huu mfuko.

Binafsi nilishawahi kumuuliza hili swali Bwana William Erio kikaoni tulipokuwa tunavutana kuhusu maslahi yetu. Habari hizi sikuwa nimezipata JF kipindi hicho, nilizisoma gazeti la Rai. Kwa kweli hakujibu swali, alichojibu ni kuwa walishakanusha kwenye gazeti. Pia wamejiwekea kinga kubwa sana serikalini hawa watu, kumbuka mfuko huu ndiyo shock absorber ya serikali pia. Pia nilimuuliza taarifa za faida na jinsi wanachama tunavyoweza kufaidika, akaniambia eti mahesabu yake ni magumu sana, na watu wenye ujuzi wa hayo mahesabu ni wachache sana nchini. Nikamwambia huwezi kuyatafasiri hayo mahesabu katika majibu rahisi kama wanachama tukayaelewa? hakujibu swali hilo. Wakati tunaendelea na madai yetu, nilisikitika kumsikia Bwana George Yambesi ambaye Permanent Secretary, Public Service Management, President's Office, akiwatolea majibu PPF kwa kuwatetea na kupotosha umma kutumia TV na magazeti pamoja na kututishia sana. Hatukukata tamaa tukawabananisha viongozi wengine serikalini na Wazirimkuu Pinda mmoja wapo ila bado wanakwepakwepa.

Hivyo hii habari yako ya kuzungumzwa na Mh. Mkulo pamoja na hiyo hati safi bado hayajatatua matatizo yetu na kuhalalisha urasimu wa kujichotea pesa zetu eti kwa kutumia sheria waliyojiwekea wachotaji na siyo sisi wachangiaji wa mfuko wenyewe. Najua hujatumwa, maana hawa watu wapo smart sana kwenye kutuhujumu michango yetu na huwa hawapendi yazungumzwe.

Sisi wanachama ndiyo wenye maamuzi, na tuna nguvu ya kuhoji chochote pale ambapo haturidhiki. Hivyo Tumekuwa tunalipwa fedha ndogo sana, huku pesa yetu ikiwekezwa kwenye miradi mikubwa mbalimbali na hatujawahi kupewa taarifa ya faida na zitatunufaishaje. Ni bora ukae kimya tutakuona una busara sana, kuliko kutetea udhalimu wa namna hii. Nakuhakikishia kama wachangiaji wote wangeyaelewa maudhi haya, sidhani kama kunaatakaye watuliza.
 
Najua watakurupuka watu humu JF na kusema nimetumwa, nimehongwa, kwa kuitetea PPF kama kawaida ya watu kukurupuka. Lakini tusimame kwenye facts na mambo yaliyo sahihi. Tujenge hoja kwa kutumia facts na si matusi, kejeli na tuhuma za kutungwa.
Mtu akisuka 'kauongo' kake vizuri alafu ndio anataka kukapresent mara nyingi ataanza na kauli za "...najua mtakataa", "...najua mtasema nimehongwa" nk nk lakini kumbuka hakuna kitu kikubwa na chenye nguvu kama UKWELI! Kama unaamini ukweli wako huwezi kuwa na hofu daima!
 
Tunakwenda vizuri nafikiri- Ngao unasema " Malipo haya yanafanywa na mashirika mengi ya umma na si PPF tu tangu enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi (Mzee wa Rukhsa) miaka ya 1990s ndiyo maana Mkulo akatetea malipo haya Bungeni"

Na wewe unakaribishwa utuwekee hapa in the open majina ya hayo mashirika mengine yanayofanya mchezo huu wa dhuluma kwa wachangaiji.Utakuwa umetoa mchango mkubwa sana towards uwajibikaji na kuonesha UZALENDO wako.

:hug:
 
Ndugu zanguni, nisiwachoshe wala msinichoshe kwa mabishano yasiyoisha. Nikisoma comments zenu naona tunakubaliana baadhi ya mambo lakini kuna mengine hatuelewani sawasawa.

Kwa msisitizo, haya ndiyo maoni yangu kwenye mjadala huu:


  • Sijaona hata chembe ya ushahidi wowote wa tuhuma za rushwa, wizi na ubadhirifu dhidi ya PPF ambazo zinatolewa humu JF mara kwa mara.


  • Malipo ya gratuity na group endowment scheme yanafanywa kwenye mashirika karibu yote ya umma kufuatia utaratibu ulioanzishwa na shirika la Bima (NIC) miaka ya 1990s.


  • Wakurugenzi wa PPF wanalipwa gratuity kwa vile ni haki yao kama contract workers. Kuna utata juu ya Group Endowment Scheme, wengine wanasema wanatakiwa walipwe permanent and pensionable employees tu, Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo na wengine serikalini wanasema hata menejimenti ambao ni contract employees nao walipwe. Hivyo malipo ya PPF ambayo watu wameweka invoice humu JF na kusema ni ufisadi ni halali kwa mujibu wa utaratibu wa serikali ULIOPO. Hoja ni kushinikiza huu utaratibu ufutwe, ubadilishwe au uendelee.


  • Kamati ya Bunge ya POAC imemuagiza CAG achunguze malipo ya gratuity na Group Endowment Scheme PPF, mifuko ya pensheni mingine na mashirika yote ya umma ili kuona uhalali wake na kama kulikuwa na uvunjaji wa sheria. Huu mjadala utapata jibu sahihi baada ya hiyo ripoti ya CAG kutolewa.


  • Ni muhimu kuangalia THE BIGGER PICTURE. Ripoti ya CAG itatusaidia kwenye hili jambo ili tujue ni mashirika mangapi yana huu utaratibu au ni PPF tu. Je, utaratibu huu ni halali? Je, umekuwa abused? Je, kuna wizi, corruption, fraud au embezzlement of public funds?

Natumaini mmenisoma hapo. Over and out.
 
Ndugu Ngao One naona unajitahidi tuamini unavyolielewa hili jambo. Sawa walitumia hiyo sheria ya mashirika ya umma. Kumbuka huu ni mfuko na wanachama ni wachangiaji.

Napenda kukwambia pia, utaratibu uliopo wa kuwachagua/kuwateuwa wajumbe wa bodi sisi wanachama tulishaukataa, imepelekea wengi hata wasio wanachama kusimamia mfuko wetu. Hivyo kwanini wanashindwa yaweka sawa kwa kukaa pamoja na sisi wachangiaji? Pia ikumbukwe awali serikali ilifanya makosa sana, wakati tunaajiriwa serikalini, ile form ya ajira ilikuwa tayari ina kipengele cha kuchangia mfuko huu kama lazima.

Kuna sehemu nyingine wamebadili na kwingine bado wanaendelea na huu ukiukwaji wa sheria. Sijui na hili utalielezea vipi kisheria. Hivi kwanini watumie Serikali na wao watufanyie maamuzi. Nasisi zipo sheria zinatupa nguvu kufanya maamuzi na kuhoji vilevile. Hata kama watakuja na majibu ya aina gani, swala la sisi kuhoji na kufanya maamuzi tutakayokubaliana ni muhimu. Nasikia wameshabadilisha factor ilingane na mifuko mingine, ila hatutatulia kwa hilo. Ngoja tukishafikishana nao mahakamani ndiyo utajua jinsi hili swala lilivyo tete.

Hivyo nakushauri uliongelee hivihivi ukiwa invisible, maana kuna wanachama tunaoelewa dhuluma hii tunahasira na hatupendi kusikia hizi blabla. Nakuomba ukipata muda angalia mifumo ya nchi nyingine jinsi wanavyoendesha hii mifuko utaelewa kwanini hatuachi kupiga kelele. Hatutegemei jibu zuri kutoka serikalini, maana na wao wanahusika kinamna na kuhujumu nguvu zetu. Tupo tayari kufika hata mahakama za kimataifa kama tutakosa haki yetu iliyo wazi.

Sipendi nianike mambo mengi sababu bado tunapambana, ila kama nilivyokushauri awali:

Kama wewe si muathirika kwenye huu mfuko, basi ni bora ukae kimya. Ni aibu kusema mfuko wenye pesa nyingi kuliko mifuko yote, halafu wanachama wake wanapokea malipo duni kuliko mifuko yote nchini kasoro wenzetu wa SSSS. Na kwataarifa yako, viongozi wakuu wa serikali na wajumbe wengine wanaoendesha huu mfuko akiwamo waziri hawapo/hawachangii mfuko huu. Tena wengine walikuwa mfuko huu, wakishapata wadhifa mkubwa wanahamishwa kwa sheria hizohizo walizojiwekea.

Sijui hawa Social Security Regulatory Authority wanasimamia fairness au wanawasimamia wao. Naomba kawaulize/fatilia kwanini wao si wanachama/wachangiaji wa PPF, ila wanajiwekea sheria inawaruhusu kujikwapulia gratuity?

Ndugu zanguni, nisiwachoshe wala msinichoshe kwa mabishano yasiyoisha. Nikisoma comments zenu naona tunakubaliana baadhi ya mambo lakini kuna mengine hatuelewani sawasawa.

Kwa msisitizo, haya ndiyo maoni yangu kwenye mjadala huu:


  • Sijaona hata chembe ya ushahidi wowote wa tuhuma za rushwa, wizi na ubadhirifu dhidi ya PPF ambazo zinatolewa humu JF mara kwa mara.


  • Malipo ya gratuity na group endowment scheme yanafanywa kwenye mashirika karibu yote ya umma kufuatia utaratibu ulioanzishwa na shirika la Bima (NIC) miaka ya 1990s.


  • Wakurugenzi wa PPF wanalipwa gratuity kwa vile ni haki yao kama contract workers. Kuna utata juu ya Group Endowment Scheme, wengine wanasema wanatakiwa walipwe permanent and pensionable employees tu, Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo na wengine serikalini wanasema hata menejimenti ambao ni contract employees nao walipwe. Hivyo malipo ya PPF ambayo watu wameweka invoice humu JF na kusema ni ufisadi ni halali kwa mujibu wa utaratibu wa serikali ULIOPO. Hoja ni kushinikiza huu utaratibu ufutwe, ubadilishwe au uendelee.


  • Kamati ya Bunge ya POAC imemuagiza CAG achunguze malipo ya gratuity na Group Endowment Scheme PPF, mifuko ya pensheni mingine na mashirika yote ya umma ili kuona uhalali wake na kama kulikuwa na uvunjaji wa sheria. Huu mjadala utapata jibu sahihi baada ya hiyo ripoti ya CAG kutolewa.


  • Ni muhimu kuangalia THE BIGGER PICTURE. Ripoti ya CAG itatusaidia kwenye hili jambo ili tujue ni mashirika mangapi yana huu utaratibu au ni PPF tu. Je, utaratibu huu ni halali? Je, umekuwa abused? Je, kuna wizi, corruption, fraud au embezzlement of public funds?

Natumaini mmenisoma hapo. Over and out.
 
Kumekuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya JF kuwa inawachafua watu binafsi, taasisi na vyama vya siasa kutokana na tuhuma za uongo. Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeanzisha tuhuma za uongo humu JF kuwa kuna ufisadi ndani ya PPF. Sidhani kama alikuwa ana nia mbaya, tatizo ni kuwa kuna ignorance kubwa sana. Watu huwa wanakurupuka na kutoa tuhuma zisizo sahihi.

Moderators wa JF kuruhusu matusi, kejeli na tuhuma za uongo kama hizi ndiyo chanzo cha malalamiko mengi dhidi ya JF. Kuna umuhimu wa free speech ila ni changamoto kwa JF kutoruhusu tuhuma zisizokuwa na msingi, kwani hatimaye JF itapoteza credibility na kuonekana kuwa ni kichaka cha kutoa tuhuma za kutungwa na kashfa na si "The Home of Great Thinkers" kama inavyojitamba.

Mzee Mwanakijiji anayeheshimika sana huku JF alikuja na post inayosema -- "MALIPO YA Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption"

Imekuja kubainika kuwa zile tuhuma za malipo kwa menejimenti ya PPF zilizoanzishwa na Mzee Mwanakijiji humu JF ambaye aliziita kimakosa kuwa ni "corruption" na kudakiwa na Zitto Kabwe na kamati yake ya POAC, si tuhuma sahihi.

Kuhusu hii post mpya yenye kichwa cha habari: "Hivi SSRA ni kichaka cha mafisadi wa PPF? SSRA Haitaipendelea PPF kwenye ufisadi na uizi?", huu ni uzushi na udaku mtupu.

Kazi zilitangazwa SSRA na zikafanywa interview pale. Ukweli ni kuwa wafanyakazi kutoka mifuko mbalimbali ya pensheni, ikiwemo PPF, NSSF, PSPF, LAPF na kutoka sekta ya fedha waliomba kazi SSRA na kulikuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya interview, waliokuwa wafanyakazi kadhaa wa PPF wakapita na kushinda nafasi za kazi SSRA. Pengine hii ni sifa kwa PPF kuwa na wafanyakazi wenye sifa kubwa na shirika lenyewe kuheshimika mpaka wakapata nafasi za kazi SSRA.

These are the real facts. Hakuna ufisadi wowote PPF kama inavyodaiwa humu JF kila mara. Ukweli ni kuwa mfuko huu umepewa "clean audit opinion" na CAG na good governance award kwa nchi za Afrika.

Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amewahi kuwa director general wa NSSF na hivyo anafahamu vizuri uendeshaji wa mifuko ya pensheni Tanzania amesema kuwa malipo hayo yanayolalamikiwa sana PPF ni sahihi na yanafanywa na kila shirika la umma tangu miaka ya 1990s. Mkulo amesema kuwa malipo hayo ya gratuity na group endowment scheme yamepitishwa kisheria na serikali, hivyo PPF haijavunja sheria yoyote. Hakuna rushwa, wizi wala ubadhirifu wowote wa pesa.

Jamani wana JF tuache kukurupuka na kuharibu credibility ya JF kuifanya ionekane kama jukwaa la kashfa, matusi, kejeli, uongo na tuhuma zisizokuwa na msingi.

Mkulo defends PPF managers' payments

By ALVAR MWAKYUSA in Dodoma, April 20, 2011

MINISTER for Finance Mr Mustafa Mkulo has said the gratuity and endowment payments to management of Parastatal Pension Fund (PPF) were in line with regulations.

The minister made the clarification in the National Assembly on Wednesday evening while contributing to reports by three parliamentary committees, presented to the House earlier in the morning.

"The payments are in accordance with the decision of the PPF Board of Trustees in 2002. The management of the fund operates on a contractual basis and they are entitled to the gratuity.

PPF employees are of two categories, permanent and pensionable and those on contracts," elaborated the minister.

Apart from gratuity, the fund has in place arrangement for group endowment to all its employees which is paid to employees who have completed their terms of service, retiring, retrenched or deceased.

"The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law," maintained the minister.

He said the endowment payments are made to all employees of the pension fund, adding that they were designed in the early 1990s under the then National Insurance Corporation (NIC).

If the payments are to be stopped then the management of PPF has to be hired on permanent basis, said Mr Mkullo.

The Parliamentary Public Organisations Account Committee (POAC) had recommended that the Controller and Auditor General (CAG) and the Treasury Registrar intervene in the matter, saying the payment system gave room to double payment in the form of gratuity and endowment benefits.

Source: (Daily News | Mkulo defends PPF managers' payments)

Najua watakurupuka watu humu JF na kusema nimetumwa, nimehongwa, kwa kuitetea PPF kama kawaida ya watu kukurupuka. Lakini tusimame kwenye facts na mambo yaliyo sahihi. Tujenge hoja kwa kutumia facts na si matusi, kejeli na tuhuma za kutungwa.

Hapo kwenye wekundu nadhani kuna katatizo. Nakumbuka ndani ya Bunge la Tisa kulikuwa na hoja kwamba watu wanofanya kazi kwa mkataba wanalipiwa michango (pension scheme) na waajiri wao na kisha wanachukua Gratuity kwa hiyo inakuwa kama double payment! Nisaidieni
 
Ndio matatizo ya wabongo wanakimbilia kuwalaumu watu wanaopokea mafao badala ya kulaumu utaratibu

Shirika la pensheni ni shirika nyeti wacha walipwe accordingly wanafanya kazi kubwa ya kutunza pensheni zetu .

Na ni watu qualified ndio maana hajapewa Baba Enoki hizo position, they deserve. mheshimiwa alisema tuache wivu wa kike.


Siamini ninachokisoma, duh.
 
Wana JF hivi kama watumishi wetu hao wa PPF (mimi ni mwanachama wa mfuko huo) wanajilipa marupurupu manono kiasi kile nilichokiona humu kupitia Mwanakijiji, baada ya mikataba yao kuisha je wao wanawalipaje waajiri wao (wanachama wa mfuko) baada ya kustaafu? Nategemea wanachama watakuwa wakivuna viwango bora vya malipo ya uzeeni. Lakini nina shaka kwa kuwa ni mwaka jana tu wahadhiri wa vyuo vikuu walikuwa wakilalamikia viinua mgongo vya PPF. Tusaidiane
 
kwani oongo ?? Ni kweli kabisa kwa ppf kuna waganda na wakenya wengine ndani.. Mimi nauliza kila mara kwani akuna watanzania wenye ujuzi zaidi ??? Wapoo tena sana.

Kwa kweli we have to get rid of this rotten mentality yakuona hawa waganda au wakenya kwa bora zaidi kushida watanzania. Can a tanzanian go to this neighbouring countries to get a job easily ..... Never under the sun sasa why in tanzania ??
 
kwa hakika malipo yale yanastahili majina yote mawili: wizi na rushwa, ukitaka weka hongo, na unaweza kutupia ufisadi. huu ni ufisadi ulioidhinishwa na bodi ili kujinufaisha. kwani kuna tofauti gani kati ya maamuzi ya bodi na mabaraza ya madiwani wa ccm ambayo yalikuwa yakihamisha mali za wananchi na kuzifanya za ccm, kwa mfano kule moshi na kwingineko nchini? sheria mbovu km hizi zinahalalisha rushwa na ufisadi.
 
Ngao one hii ndio original thread yako
Kumekuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya JF kuwa inawachafua watu binafsi, taasisi na vyama vya siasa kutokana na tuhuma za uongo. Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeanzisha tuhuma za uongo humu JF kuwa kuna ufisadi ndani ya PPF.

Moderators wa JF kuruhusu matusi, kejeli na tuhuma za uongo kama hizi ndiyo chanzo cha malalamiko mengi dhidi ya JF.

Imekuja kubainika kuwa zile tuhuma za malipo kwa menejimenti ya PPF zilizoanzishwa na Mzee Mwanakijiji humu JF.huu ni uzushi na udaku mtupu.

These are the real facts. Hakuna ufisadi wowote PPF kama inavyodaiwa humu JF kila mara. Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amewahi kuwa director general wa NSSF na hivyo anafahamu vizuri uendeshaji wa mifuko ya pensheni Tanzania amesema kuwa malipo hayo yanayolalamikiwa sana PPF ni sahihi na yanafanywa na kila shirika la umma tangu miaka ya 1990s. Hakuna rushwa, wizi wala ubadhirifu.

Jamani wana JF tuache kukurupuka na kuharibu credibility ya JF kuifanya ionekane kama jukwaa la kashfa, matusi, kejeli, uongo na tuhuma zisizokuwa na msingi.

Leo una retreat, soma hapo chini
Ndugu zanguni, nisiwachoshe wala msinichoshe kwa mabishano yasiyoisha. Nikisoma comments zenu naona tunakubaliana baadhi ya mambo lakini kuna mengine hatuelewani sawasawa.Kwa msisitizo, haya ndiyo maoni yangu kwenye mjadala huu:

Kamati ya Bunge ya POAC imemuagiza CAG achunguze malipo ya gratuity na Group Endowment Scheme PPF, mifuko ya pensheni mingine na mashirika yote ya umma ili kuona uhalali wake na kama kulikuwa na uvunjaji wa sheria. Huu mjadala utapata jibu sahihi baada ya hiyo ripoti ya CAG kutolewa.

Waombe radhi wana JF kwa usumbufu uliowasababishia ikiwa ni pamoja na kashfa, kejeli, dhihaka na utambuzi finyu wa kujenga hoja bila kuweza kuzitetea.

Ahsante

Nguruvi
 
nimeona japo niandike mawili matatu kinyume na hoja za mtoa hoja mkuu...!
Kuvunjwa kwa AZIMIO TUKUFU LA ARUSHA ndiyo matokeo ya yote haya...sasa mmejipitishia sheria ya kujilipa kupita mtumishi anayefanya kazi miaka 30.......! LINGEKUWEPO AZIMIO LILE LA ARUSHA nadhani hata haya malalamiko yasingalikuwepo...!
MY HOPE:
NAPE KASEMA KUJIVUA GAMBA KUTAINGIA SERIKALINI...TUSUBIRI TUONE KAMA SEHEMU KAMA HIZI ZITAGUSWA
 
Kwa sababu ya watu kama akina nyie mlioko serikalini.......mme-limit...thinking abilities zenu........No wonder......tunawalipa DOWANS.........damn!!
 
Ngao 1

Kwa kweli unakurupuka tu huna kitu taarifa au hoja yeyote kwenye JF yaani ww ni mbuzi wa kafara na kama umepewa vijisenti karudishe haraka utapata msituko wa moyo na kufa bure kwani watu unaowatetea hawabebeki we agaika na mkate wako wa kila siku.
 
No matter what Ngao One says, nimeshindwa kuelewa anadefend nini, gratuity? Erio? Ulaji? or what...

He is on the wrong side of things

the clock is ticking
 
Ndiyo yaleyale ya kukurupuka. Kwa vile mimi nimehoji hizo tuhuma za "corruption" na kutaka kuona ushahidi, basi na mimi napokea hizo gratuity au nimetumwa. Hayo ni majibu mepesi. Mkulo ameeleza kuwa malipo haya ni "halali" kwa mujibu wa utaratibu wa serikali. Tena mtu wa kwanza kunufaika nayo alikuwa David Mattaka wakati anastaafu PPF.

Ingeleta tija kama tungeweka juhudi kupinga sera/utaratibu huu wa malipo serikalini na tudai mabadiliko, si kutoa tuhuma hewa za "corruption" dhidi ya shirika moja hili la PPF bila ushahidi wowote.

Kama tuko serious, tufanye mjadala mpana kuhusu matumizi mabaya ya pesa kwenye mashirika ya umma yote (si PPF tu) na serikalini, Mfano, tupinge pia Bunge kupitisha azimio hivi majuzi kuwa Wabunge wote sasa wakopeshwe pesa za kununulia magari, kufanya service kwa magari na kununulia fenicha nyumbani kwa mashart yafuatayo:

1. Serikali kutoa msamaha wa 50% kwa mkopo wa wabunge (eg. Mheshimiwa akikopa 50m/-, atarejesha 25m/- tu)
2. Mkopo kutolewa bila ya riba kwa Wabunge

Walimu, polisi, manesi, mbona hawapewi upendeleo huu kama wabunge?

Bwana Ngao One

1. PENYE RED: Mkulo ni mwongo, hivi ya Jailo na Ngereja nani alisema si sahihi serikalini? Hata CAG wako na Luhanjo walisemaje? Hata PPF ndivyo kulivyo,

2. Penye BLUE: Mataka aliondoka kwa kashfa na hata ATCL nako kaondoka kwa kashfa, Mkulo anatolea mifano ya vibaka bungeni na kufanya wabunge waamini kuwa walichokifanya PPF sio ubadhirifu.

3 Penye Zambalau: PPF, wakurugenzi hao hao wanakopeshwa magari ya kifahari (VX 200m kila mmoja) bila riba na kodi yote inalipwa na mfuko, na huu sio ubadhirifu? Kodi za magari haya ni karib 50% ya value, nao ni wabunge?

Ngao One aka Asia Erio usikurupuke, subiri lililompata mataka linakuja very soon maana CAG harudii makosa ya JAIRO kwa kumbeba Erio.

Rasjah umepotelea wapi? Usiogope hufukuzwi PPF maana ni incognito, watafukuza wapigania uhuru lakina hawatatumaliza.

Tupambane hadi uozo ndani ya PPF unaofanywa na ERIO, MMARI(Mzee wa matusi kwa wafanyakazi), KASHIMBA na MGANGA
 
Back
Top Bottom