Tuhuma za uongo dhidi ya PPF, wana JF tuache kukurupuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za uongo dhidi ya PPF, wana JF tuache kukurupuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngao One, Apr 20, 2011.

 1. N

  Ngao One Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kumekuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya JF kuwa inawachafua watu binafsi, taasisi na vyama vya siasa kutokana na tuhuma za uongo. Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeanzisha tuhuma za uongo humu JF kuwa kuna ufisadi ndani ya PPF. Sidhani kama alikuwa ana nia mbaya, tatizo ni kuwa kuna ignorance kubwa sana. Watu huwa wanakurupuka na kutoa tuhuma zisizo sahihi.

  Moderators wa JF kuruhusu matusi, kejeli na tuhuma za uongo kama hizi ndiyo chanzo cha malalamiko mengi dhidi ya JF. Kuna umuhimu wa free speech ila ni changamoto kwa JF kutoruhusu tuhuma zisizokuwa na msingi, kwani hatimaye JF itapoteza credibility na kuonekana kuwa ni kichaka cha kutoa tuhuma za kutungwa na kashfa na si "The Home of Great Thinkers" kama inavyojitamba.

  Mzee Mwanakijiji anayeheshimika sana huku JF alikuja na post inayosema -- "MALIPO YA Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption"

  Imekuja kubainika kuwa zile tuhuma za malipo kwa menejimenti ya PPF zilizoanzishwa na Mzee Mwanakijiji humu JF ambaye aliziita kimakosa kuwa ni "corruption" na kudakiwa na Zitto Kabwe na kamati yake ya POAC, si tuhuma sahihi.

  Kuhusu hii post mpya yenye kichwa cha habari: "Hivi SSRA ni kichaka cha mafisadi wa PPF? SSRA Haitaipendelea PPF kwenye ufisadi na uizi?", huu ni uzushi na udaku mtupu.

  Kazi zilitangazwa SSRA na zikafanywa interview pale. Ukweli ni kuwa wafanyakazi kutoka mifuko mbalimbali ya pensheni, ikiwemo PPF, NSSF, PSPF, LAPF na kutoka sekta ya fedha waliomba kazi SSRA na kulikuwa na ushindani mkubwa.

  Baada ya interview, waliokuwa wafanyakazi kadhaa wa PPF wakapita na kushinda nafasi za kazi SSRA. Pengine hii ni sifa kwa PPF kuwa na wafanyakazi wenye sifa kubwa na shirika lenyewe kuheshimika mpaka wakapata nafasi za kazi SSRA.

  These are the real facts. Hakuna ufisadi wowote PPF kama inavyodaiwa humu JF kila mara. Ukweli ni kuwa mfuko huu umepewa "clean audit opinion" na CAG na good governance award kwa nchi za Afrika.

  Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amewahi kuwa director general wa NSSF na hivyo anafahamu vizuri uendeshaji wa mifuko ya pensheni Tanzania amesema kuwa malipo hayo yanayolalamikiwa sana PPF ni sahihi na yanafanywa na kila shirika la umma tangu miaka ya 1990s. Mkulo amesema kuwa malipo hayo ya gratuity na group endowment scheme yamepitishwa kisheria na serikali, hivyo PPF haijavunja sheria yoyote. Hakuna rushwa, wizi wala ubadhirifu wowote wa pesa.

  Jamani wana JF tuache kukurupuka na kuharibu credibility ya JF kuifanya ionekane kama jukwaa la kashfa, matusi, kejeli, uongo na tuhuma zisizokuwa na msingi.

  Mkulo defends PPF managers' payments

  By ALVAR MWAKYUSA in Dodoma, April 20, 2011

  MINISTER for Finance Mr Mustafa Mkulo has said the gratuity and endowment payments to management of Parastatal Pension Fund (PPF) were in line with regulations.

  The minister made the clarification in the National Assembly on Wednesday evening while contributing to reports by three parliamentary committees, presented to the House earlier in the morning.

  "The payments are in accordance with the decision of the PPF Board of Trustees in 2002. The management of the fund operates on a contractual basis and they are entitled to the gratuity.

  PPF employees are of two categories, permanent and pensionable and those on contracts," elaborated the minister.

  Apart from gratuity, the fund has in place arrangement for group endowment to all its employees which is paid to employees who have completed their terms of service, retiring, retrenched or deceased.

  "The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law," maintained the minister.

  He said the endowment payments are made to all employees of the pension fund, adding that they were designed in the early 1990s under the then National Insurance Corporation (NIC).

  If the payments are to be stopped then the management of PPF has to be hired on permanent basis, said Mr Mkullo.

  The Parliamentary Public Organisations Account Committee (POAC) had recommended that the Controller and Auditor General (CAG) and the Treasury Registrar intervene in the matter, saying the payment system gave room to double payment in the form of gratuity and endowment benefits.


  Source: (Daily News | Mkulo defends PPF managers' payments)

  Najua watakurupuka watu humu JF na kusema nimetumwa, nimehongwa, kwa kuitetea PPF kama kawaida ya watu kukurupuka. Lakini tusimame kwenye facts na mambo yaliyo sahihi. Tujenge hoja kwa kutumia facts na si matusi, kejeli na tuhuma za kutungwa.
   
 2. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na hilo la mganda wa IT c la kweli?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mtu ninayeamini kila kitu ambacho "serikali imesema" kuwa ni kweli ningekuwa kwenye matatizo sana. Nilisema ripoti ya PPF bado inakuja tukishaweka vyote wazi watu wataamua kama ilikuwa ni corruption au not.
   
 4. N

  Ngao One Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mimi sielewi kwa nini PPF na sasa SSRA kama inavyodaiwa iajiri Mganda au raia mwingine wowote wa nje kama Head of IT wakati kuna Watanzania wengi sana wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo. Ni muhimu kwa wakuu wa mashirika ya umma na binafsi na waajiri wengine kuwa na uzalendo na kuajiri Watanzania wenye sifa. Sidhani kama huyo Mganda ana sifa exceptional/unique ambazo hakuna Mtanzania mwenye sifa hizo. Hapo ni kuangalia sheria za uhamiaji zinasemaje. Kuna udhaifu kwa Idara ya Uhamiaji kuruhusu wageni kuajiriwa hovyo. Pia, wafanyakazi wenye data SSRA wapeleke taarifa Idara ya Uhamiaji kuhusu tuhuma hizo kuwa Mganda alitokea PPF akaajiriwa SSRA kinyume na sheria.
   
 5. N

  Ngao One Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mkuu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, aliongea Bungeni na kusema kuwa: "The gratuity and endowment payments attract a 30 per cent deduction in taxes and are paid according to the law."

  Wewe umesema kuwa malipo ya PPF ni "rewarding and defending corruption." Hii inaleta hisia potofu kuwa kuna wizi na rushwa kubwa PPF, kumbe malipo hayo ni kwa mujibu wa sheria na sera za serikali. Malipo haya yanafanywa kwenye mashirika karibu yote makubwa ya umma hapa Tanzania, si PPF tu.

  Ingeleta tija zaidi kama tungejadili sera hii ya serikali ya malipo ya gratuity and endowment kwenye mashirika ya umma yote kwa ujumla wake na kushauri kama yafutwe au yarekebishwe badala ya kuinyooshea kidole PPF tu kila siku na kujenga hisia potofu kuwa kuna ufisadi mkubwa huko wakati ukweli ni kuwa malipo hayo yanafanywa kwa kufuata utaratibu uliopo. Hapa ni vigumu kwa mtu kutoamini kuwa kuna witch-hunting inafanyika dhidi ya PPF au watu wanakurupuka tu na tuhuma za uongo.
   
 6. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi mwenyewe nashangaa kwenye shirika la umma anahajiliwa mgeni! Tanzania inakwenda wap?
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo kila kinachosemwa na serikali au waziri ni sahihi! kama unavyotaka kutuaminisha.
  Kumbu kumbu zangu zinaonyesha kuwa bunge lilishawahi kuambiwa Richmond haikuwa na mkono wa rushwa. 'Down the lane' imethibitika bila shaka kuwa ule ulikuwa uongo 'uliotukuka' .

  Kumbu kumbu zangu zinanionyesha kuwa Waziri mkuu alishasema 'uongo' bungeni kwasababu hatujaambiwa tuhuma hizo zilikuwa ni kweli au uongo na hivyo tunabaki kuamini ni kweli hadi itakapothibitika vinginevyo.
  na kuna mifano lukuki ya namana hiyo

  Kwa muktadha huo kama kinachosemwa bungeni au na kiongozi wa serikali ni ukweli, ukweli mtupu nitakubaliana na wewe, vinginevyo ni suala la muda muda tu na tutakukaribisha tena ima tukupongeze au tukusute.
   
 8. W

  Warofo Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si kila jambo linalosemwa na serikali ni sahihi. Pia, si kila tuhuma inayotolewa humu JF na kwingineko ni sahihi. Ila kama alivyosema mtoa mada humu, ni muhimu pia kwa watu wanaotoa tuhuma za ufisadi humu JF nao waje na facts. Itaharibu sifa za JF iwapo watu wataruhusiwa kutoa tuhuma za rushwa, ufisadi na wizi bila ya kuwa challenged kuthibitisha tuhuma hizo. Watu wamesema PPF kuna ufisadi wanalipana pesa kwa njia za wizi. Waziri wa Fedha amesema Bungeni na kuwekwa kwenye kumbukumbu za hansard kuwa malipo hayo ni halali na yamefanywa kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa serikali.

  Hapa sasa watoa tuhuma wafanye homework/utafiti na kutuletea hiyo sheria/sera ya serikali inayokataza malipo hayo ya PPF na mashirika mengine ya umma ili kuthibitisha tuhuma zao za ufisadi. Talk is cheap.
   
 9. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Tumekusikia, whatever the case, huu ni wizi, It might and perhaps it is true malipo hayo ni ya kisheria, basi ni sheria mbovu ya kuiba mali ya wachangiaji wa mifuko hiyo. Huwezi kumlipa mtu milioni 500 kwa miaka mitatu halafu mtu aliyechangia miaka 30 akalipwa milioni 5. Nina mifano hai, ukitaka nitaiweke humu jamvini. ni sheria mbovu, ifutwe.
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Jamani wananchi tuache majungu

  Na wanasiasa waache kubeba kila kitu cha Jamii Forum kukipeleka bungeni

  Ni aibu!!!
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  au mkuu ngao one umehusika nini? jivue gamba tu km vp kabla Dr. hajakuingiza kwenye list mpya.
   
 12. N

  Ngao One Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Tusikurupuke. Tujadiliane kwa hoja. Waziri wa Fedha amesema malipo yanayofanywa kwa menejimenti ni kwa mujibu wa sheria na yalianzishwa na shirika la bima, NIC, tangu miaka ya 1990s. Controller and Auditor General (CAG) ambaye ndiye authority wa kugundua malipo yasiyo halali amewapa PPF hati safi ya ukaguzi. PPF imetambuliwa kimataifa kwa kuwa na utawala bora. PPF imesifiwa na kamati ya Bunge ya POAC pamoja na msimamizi wa mifuko ya pensheni SSRA kuwa ndiyo mfuko wa pensheni Tanzania unaoweza kudumu kwa miaka mingi kuliko mifuko yote kwa kuwa na usimamizi bora wa kifedha na mtaji mkubwa.

  Sasa huo wizi, ufisadi, uzinzi na ubadhirifu wa mali ya umma mnaotaka kutuaminisha nyie uko wapi? Msilete mambo ya udaku huku JF.
   
 13. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Unaposema JF wawe makini halafu unavuma ukurasa mzima sielewi kabisa. Unaposema Mkulo alisema kwamba gratuity na group endowment scheme yamepitishwa kisheri unamaanisha nini? Je kila kitu ambacho kipo kisherika ni haki? Mfano umeitwa mahakamani kama shahidi, huko kuna sheria inayosema unaweza kuongea au unaweza kunyamaza bila kusema chochote. Ni haki haki kisheria kunyamaza. Wewe kwa madaha kabisa ukanyamaza bila kusema chochote na kutokana na kunyamaza kwako mtu ambaye hakutenda kosa akafungwa. Je umetenda haki? Kisheria kufanya hivyo ni haki, lakini je katika hili umetenda haki?
  Hiki ndiyo ninachokiona hapa, hata kama sheria ilifuatwa je maandili ya kijamii yalifuatwa au wamesababisha hasara kwa wengine tu? Wito wangu ni kwamba tunapotetea mambo haya tunapaswa kuwa makini sana. Hata hivyo kwangu mimi simwamini mtu yeyote atakayesema kwa niaba ya thithiem. Hata siku moja. Niliwaamini wakanisodola, sitaki tena. Nukta.
   
 14. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  NgaoOne &co - Unajitahidi sana kwa kile 'ulichodhamiria kufanya'. no doubt yoyote anayekutegemea atakupongeza kwa kazi nzuri so far. Ila tu nikukumbushe kuwa kama 'ulivyokiri' umesema hili jukwa la wanaojitamba kuwa ‘great thinkers' kwa hiyo Tegemea kibarua chako hakitakuwa chepesi, hapa majibu mepesi hayana nafasi. Napenda kukuasa kwa kuanzia kuwa hapa uzito wa mtu si hoja, mantiki ya anachosema inapimwa bila kujali uzito wake, pia hapa sheria hazitufungi kufikiri.
  Nafikiri kuchanganua uliyoyasema kama utetezi wa fedha nyingi zilizolipwa PPF utanoga tutapopata taarfa zaidi nafurahi kusikia wako wanaolifanyia kazi.
  Kwa sasa napenda tu ujue haya ya kijumla kuwa

  Not all that is lawful is Right – hivyo kutokuvunja sheria hakumaanishi umewatendea sawa na haki wale wafanyakazi wanadunduliza vijisenti vyao kupitia mifuko ya akiba. Mpango wowote ule unaotoa fursa kwa ‘wajanja wachache kujilipa mamilioni ya wafanyakazi si sawa na pia siyo haki hata kama hauvunji sheria. Inawezekana ukawa hujavunja sheria moja lakini maamuzi hayo yaliyoidhinisha utaratibu yanawea kuwa yanakiuka dhamira ya mfuko. Sijui kama unfahamu kuhusu uongozi wa mabenki na mashirika ya kimataifa yalivyochangia sana financial crisis kwa mfano Marekani kwa kulipana 'bonus feki'

  Kufanyika kwingine au kuanzia miaka ya 90 (zamani) haiupi uhalali utaratibu huo sana sana unachotuambia ni kwamba tumedhulumiwa kwa muda mrefu. Hapa unchotuambia ni kuwa you are consistent in the wrong doing.

  Kwamba malipo yalilipiwa kodi sijui inahalalisha nini katika hoja yako nafikiri usahihi wa malipo hautokani na hilo sana sana itasadia kuthibitisha kuwa kweli ulilipwa pale litapohitajika hilo.
  Yatosha haya kwa ujumla ila tutakapokuwa na taarifa zaidi be assured tutaengage kuona imekaaje.


  Tuvute subira!:hug:
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwa hakika bila hoja ya msingi hakipiti kitu hapa. Hii inanifanya niipende zaid jf. Mungu bariki Tanzania, Mungu bariki wanachama wa jf, Mungu bariki Jf.
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Ngao one, nimesoma posts zako tatu tu, nimegundua hata wewe hujui unataka kusema nini.... and more important kwa kuanza kusema MMM ndiye wa kwanza kuleta tuhuma wakati kuna threads zilishakuwepo long time kuhusu PPF... Later unasema hata wewe hujui mganda kaingiaje

  nasubiri useme "mie nilitumwa tu kuleta hii sredi"
   
 17. N

  Ngao One Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naomba nijieleze vizuri pengine utapata kunielewa. Sawa, MMM anaweza kuwa si mtu wa kwanza kuleta tuhuma za PPF humu JF lakini thread aliyeipost ni moja ya muendelezo wa tuhuma hizo. MMM na wengine wameituhumu PPF kwa corruption, wizi, etc, lakini sijaona any evidence ya hayo. Nimeona invoice tu za malipo kwa baadhi ya directors. Lakini ukweli kuwa malipo hayo (pamoja na kwamba ni makubwa) ni malipo halali kutokana na utaratibu wa serikali uliowekwa kuhusiana na gratuity na group endowment scheme.
  Malipo haya yanafanywa na mashirika mengi ya umma na si PPF tu tangu enzi za Rais Ali Hassan Mwinyi (Mzee wa Rukhsa) miaka ya 1990s ndiyo maana Mkulo akatetea malipo haya Bungeni.

  Hoja ni kuwa badala ya kukurupuka na kuwashutumu PPF kwa "corruption" tuangalie utaratibu huu mzima wa malipo haya ili tushinikize ufutwe au urekebishwe. Kama watu wanatoa tuhuma za "corruption" basi leteni huo ushahidi.

  So far sijaona ushahidi wowote kuwa kuna ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na wizi ndani ya PPF kama inavyodaiwa humu ndani ya JF na baadhi ya watu. Vinginevyo tuhuma hizi zinaonekana kama udaku tu.

  Kuhusu Mganda, mimi napinga vikali wageni kuajiriwa kwenye nafasi ambazo wako Watanzania wengi, tena wenye uwezo mkubwa zaidi, ambao wanaweza kuzifanya. Kama PPF waliajiri Mganda kinyume na sheria hilo ni kosa. Pia hao wafanyakazi wa PPF waliojua hili kwa nini hawakutoa taarifa uhamiaji au kwenye kamati za Zitto Kabwe ya POAC?
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ngao One,

  Endelea kufaidi gratuity yako "according to the law".. Time will prove both of you, (Mkulo/Ngao One) - Very Wrong - Trust ME!

  Wakati PESA zinachotwa BOT was right "according to the law"
   
 19. N

  Ngao One Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ndiyo yaleyale ya kukurupuka. Kwa vile mimi nimehoji hizo tuhuma za "corruption" na kutaka kuona ushahidi, basi na mimi napokea hizo gratuity au nimetumwa. Hayo ni majibu mepesi. Mkulo ameeleza kuwa malipo haya ni "halali" kwa mujibu wa utaratibu wa serikali. Tena mtu wa kwanza kunufaika nayo alikuwa David Mattaka wakati anastaafu PPF.

  Ingeleta tija kama tungeweka juhudi kupinga sera/utaratibu huu wa malipo serikalini na tudai mabadiliko, si kutoa tuhuma hewa za "corruption" dhidi ya shirika moja hili la PPF bila ushahidi wowote.

  Kama tuko serious, tufanye mjadala mpana kuhusu matumizi mabaya ya pesa kwenye mashirika ya umma yote (si PPF tu) na serikalini, Mfano, tupinge pia Bunge kupitisha azimio hivi majuzi kuwa Wabunge wote sasa wakopeshwe pesa za kununulia magari, kufanya service kwa magari na kununulia fenicha nyumbani kwa mashart yafuatayo:

  1. Serikali kutoa msamaha wa 50% kwa mkopo wa wabunge (eg. Mheshimiwa akikopa 50m/-, atarejesha 25m/- tu)
  2. Mkopo kutolewa bila ya riba kwa Wabunge

  Walimu, polisi, manesi, mbona hawapewi upendeleo huu kama wabunge?
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ndio matatizo ya wabongo wanakimbilia kuwalaumu watu wanaopokea mafao badala ya kulaumu utaratibu

  Shirika la pensheni ni shirika nyeti wacha walipwe accordingly wanafanya kazi kubwa ya kutunza pensheni zetu .

  Na ni watu qualified ndio maana hajapewa Baba Enoki hizo position, they deserve. mheshimiwa alisema tuache wivu wa kike.
   
Loading...