Tuhuma nzito kwa Abbas Mtemvu mbunge wa Temeke-CCM

Tuhuma nzito kwa Abbas Mtemvu mbunge wa Temeke-CCM

waliozoea kuishi kwa uwongo kwa miaka 50 hawawezi kuishi kwenye ukweli ndo wale wale ccm uko panya huyu binti anatudanganya ss anafikiria ss ni wapuuzi wenzake mjinga sana ccm ni janga la taifa
 
waliozoea kuishi kwa uwongo kwa miaka 50 hawawezi kuishi kwenye ukweli ndo wale wale ccm uko panya huyu binti anatudanganya ss anafikiria ss ni wapuuzi wenzake mjinga sana ccm ni janga la taifa

Unajua mi liliposemwa hilo jina kuwa ndo mshindi wa miss Tanzania nilikuwa naangalia na mke wangu nikamwambia palepale kuwa hapa wamechakachua,maanake niliona kuna harufu ya rushwa na ufisadi sema uthibitisho ndo nikawa sina leo mambo hadharani,duh noma kishenzi!
 
Jf noma watu hadi passport mnayo
attachment.php
 
Da! Kiukweli mashindano hayo ya miss Tanzania yamekosa mvuto na maadili hatuwezi fanywa wajinga kiasi hiki ndani ya miaka 50 ya Uhuru uchakachuaji unafanyika tu ktk tasinia hiii yaaani waliowahi kutufichia aibu kidogo ktk tasinia hyo ni Nancy sumari, Hoyce temu na Miriam odemba basi wengine wote ni kula pesa za walala hoi tu ambazo lundenga unafadhiliwa na watu alafu na wewe una Fanya maujinga kwa nini uc ache hao wafadhili wanaokufadhili wawasaidie watu wasiojiweza ktk nchi hii
Kwa nini watanzania tumekosa uzalendo kiasi hchoo!!!!
 


18yrs of age

Minus 2yrs masters 3yrs bachelor = 13yrs of age

Minus 6yrs secondary education = 7yrs of age

Minus 7yrs primary education = 0yrs of age

Minus 2yrs nursery school = -2yrs of age

Minus 3yrs ya kugrow at hom kabla ya nursery xcul = -5 yrs of age

So ur friend jus conjured a new miracle,, alianza kusoma 5yrs kabla hajazaliwa

Huyo ni Miss Tz wetuuu...Bado tu wanamwandama miss tz
 
Last edited by a moderator:
Abbas Mtemvu ambaye ni mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CCM anadaiwa kutumia mbinu chafu ili binti yake aitwaye Sitti Abbas aweze kuipatia umaarufu taasisi yake ijulikanayo kama 'Mtemvu foundation' yenye ofisi zake kuu maeneo ya Mbezi beach Dar es Salaam, taarifa mbalimbali zimebainisha.

Abbas Mtemvu amedaiwa kuchukua fedha za mfuko wa jimbo la Temeke takribani shilingi milioni 65 ambazo alidai ni za kuisaidia taasisi yake hiyo ya 'Mtemvu foundation' ambayo inajinasibu kama taasisi inayosaidia watoto wasiojiweza ili kuzihonga kamati za miss Chang'ombe mwaka 2014-15, miss Temeke mwaka 2014-15 na ile ya miss Tanzania mwaka 2014-15 kwa lengo la kumpitisha binti yake huyo ajulikanaye kama Sitti ambaye alikuwa akiishi Marekani ili kutwaa mataji hayo.

Aidha kamati zote zilisimamiwa na Hasheem Lundenga ambaye alitakiwa kuhakikisha binti huyo wa Mtemvu ananyakuwa mataji hayo.Hasheem Lundenga ndiye muasisi na mwenyekiti wa kamati inayoandaa na kuratibu shughuli zote za kumsaka miss Tanzania.

Binti huyo wa Abbas Mtemvu (Sitti Abbas) ambaye ana umri wa miaka 29, alizaliwa mnamo mwezi wa tano mwaka 1985 kama alivyothibitisha mama yake mzazi na hivyo moja kwa moja kukosa sifa za kushiriki mashindano hayo.

Hata hivyo hali hiyo imepewa msukumo na Abbas akitumia fedha ili binti yake huyo aitangaze taasisi yake hiyo ya Mtemvu foundation kimataifa huku akijua kuwa binti yake hakuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo kutokana na kigezo cha umri ambapo inatakiwa mshiriki asizidi miaka 24.

Hata hivyo katika mashindano hayo binti huyo wa Mtemvu alidai kuwa ana umri wa miaka 18 na ana shahada ya uzamili (masters) jambo ambalo lilipingwa vikali na MAMA YAKE MZAZI ambaye alithibitisha kuwa mwanaye alidanganya umri kwa kupunguza takribani miaka 11.Sitti Abbas ndiye aliibuka mshindi wa mataji ya miss Chang'ombe, miss Temeke na miss Tanzania mwaka 2014-15 hivyo kutimiza ndoto za baba yake ambaye ni Abbas Mtemvu mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CCM za kuitangaza taasisi ya Mtemvu foundation katika ngazi ya kimataifa kama alivyotarajia.

Hivi unafahamu taratibu za utoaji na matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ? Nakushauri tafuta uweze kuandika kitu cha uhakika
 
Jamani nilikuwa nimepwekeka lakini uchambuzi was umri nimecheka hadi machozi.kweli ni mnene ananilingana kumbe naweza Kuwa miss.e?
 
swala la huyu binti kuwa na mtoto lundenga aliambiwa akakataa na alipewa uzibitisho akakataa kabisa
HIYO ILIKUA KABLA YA MASHINDANO
 
na mpaka miss world mwakani atakua na miaka 26

wakati mwisho ni 24
 
KUTANA NA MISS TANZANIA 2014(Kati ya
Warembo hawa hapa chini)....Sitti binti
Mtemvu...
Eti anadai ana miaka 18 tu na ana shahada ya
uzamili (Masters).....
.......................................................
HEBU TUPIGE HESABU; Kwa mfano;
Masters(Shahada ya uzamili) miaka 2,
Shahada ya kwanza = miaka 3,
Sekondari = miaka 6,
Shule ya Msingi = miaka 7.
Chekechea = Mwaka 1
2 + 3 + 6 + 7 + 1 = 19
Hii ina maana kuwa alianza chekechea na
miaka 0, "hakuwa amezaliwa"
Kabla ya 2015 tutajionea mengi.

kwa elimu ya kwetu ya kitanzania haiwezekani kwa umri huo kuwa na masters. Ila ukiwa huko mambele inawezekana sana tu cz kuna maprofesa wana miaka 23
 
Aka kanchi ketu kana mambo, huyu mtemvu si ndioyo anahusishwa na kuwapeleka mabinti uarabuni?
 
Back
Top Bottom