Heri ya pasaka Mwl Oluoch Naibu katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), mimi ni shabiki wako sana lakini kinachonichanganya ni kitu kimoja, kwamba ninyi viongozi CWT taifa hapo juu mpo watano, sijawahi kuona tuhuma hata moja ikielekezwa kwa kiongozi mwingine yeyote kati yenu isipokuwa wewe tu; mara waseme nafasi za uwakilishi wa chama kwenye mashirika unajipendekeza wewe, mara madeni yako ndani ya chama umeyafuta eti kinyemela, wakati katibu mkuu akiwa kwenye tume ya mabadiliko ya katiba, mara eti unadaiwa power-tillers ulizokopa na ambazo wewe umekiri kwamba ulikopa, hivi ukweli ni upi? Pia naomba mkuu wangu nikushauri upunguze kutoa koments mara kwa mara kwenye hii face book kwa kuwa baadhi ya hizo mimi huwa sizifurahii na naona zitakuangusha zaidi kwa mfano, hata kama wewe ni 'Think-Tank' la chama sio lazima useme, si watu wataona vitu vyako? Hata kama unataka mabadiliko ya uongozi kwenye chaguzi zinazoendelea ndani ya chama CWT huko mawilayani na mikoani sio lazima useme kwa kuwa hii Movement for Change unayoipigia debe inaweza kupanda mpaka huko taifani. Mkuu wangu jambo jingine unamipigia debe Stela Kiyabo kuwa makamu wa rais, nikiri kwamba mimi simfahamu huyu mtu ila nime-google na kusoma taarifa zake kwa lengo la kugundua ni mtu wa aina gani, hata hivyo, mtindo ambao unatumia kumpigia debe kwa mtazamo wangu utakutengenezea madui wa kudumu, naamini wewe ni muumini wa wa biblia ambapo tunaaswa "iweni na amani na watu wote", kama ana uwezo mwache aogelee mwenyewe na uwaachie wanachama uhuru wa kuchagua na kama lilikuwa ni wazo la secretariat kama ulivysema, mtanisamehe viongozi kwani hamkupaswa kuteua mtu kwa nafasi yeyote kwa kuwa wanachama wote wana haki sawa ndani ya katiba, unafikiri wanaogombea naye wanakuelewaje mpaka sasa? Na kuhusu marumbano yako na Heleni mbezi kwa maoni yangu hayana tija sio kwa chama hata kwako pia. Kwa yale ninayoyajua kuhusu wewe ninaamini kuwa unawezo wa kurejea kwenye nafasi yako lakini hoja yangu ya kwanza hapa ndio inayonipa mashaka. Pasaka njema.