Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..!

Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..!

CUF ni part and parcel of our government. Je wana nia ya kweli
 
molemo unamatatizo kweli watu wanajadili swala la ukombozi wa nchi ya viongozi mafisadi wewe unaleta habari ya ushirika wa cuf na ccm be serious and kama unaona hauna cha kuchangia tulia bwana.

au kisa ni hoja inayomhusu lipumba?????

molemo a great thinker,
sory for u.
 
Kwa mujibu wa Zitto vyama vyote viko tayari hata UDP ya Mzee Cheyo. Cheyo alikuwa tayari kusaini waraka wa kutokuwa na imani na waziri mkuu lakini bahati mbaya alisafiri!

ITV
 
Watu wamefikiaa point of no reTURN, tafadhali mtujulishe ni lini maandamano, kwani kwa sasa biashara haziendi tunafungua asubuhi na tunafunga jioni bila kuuza, mikopo benk hailipiki MABENK YAKO MBIONI KUFILISIKA, TRA hawana cha kukusanya kwani wafanya biashara hawauzi tena.Watanzania wote kwa sasa wamechoka kila kona ni mafisadi tu ndiyo wanapeta.
 
Kwanini tusubiri matamko kutoka kwa vikundi fulani vya watu? ina maana wao ndo wanaumia zaidi kuliko sisi au? Hivi kweli kitendo cha Maghembe kukiri kwamba wawekezaji wa mashamba hapa kwetu wanalipa Tsh 200 kwa mwaka, halafu anasema serikali italishughulikia na pia kukubali kwamba production cost ya sukari ni Tsh 1200 ila tozo za serikali ndizo zinazo sababisha kuwa 2500, ni suala la kuvumilia eti tusubiri hasasi mbalimbali zitoe tamko?
 
hata Libya walipewa vijimkwara kama hivi lakini mwishowe unajua nini kilitokea... hakuna kitu kibaya kama njaa kijana kinakufanya unafanya lolote.. maanake ukitulia utakufa na risasi pia inaua...
 
Uandamane ili iweje, yaani unataka wananchi waache shughuli zao za kulijenga Taifa ili washiriki huo upuuzi. Jaribuni muone. Kama manataka kutikisa kiberiti muone kama kina njiti, siku hiyo kitawaunguza.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

Unatumia kinywaji gani? Sikuwekei sumu japo sikupendi.
 
naunga mkono maandamano kwa asilimia 100
hii inamaanisha kwa kuwa hawakutaka kuwasikiliza tuliowatuma watuwakilishe sasa watatusikiliza sisi wenyewe wananchi.
na athari zake wataziona ila wasiwasi wangu KIBALI KITAPATIKANA?
 

Mie nasema Ijumaa sintokuwepo ntakuwa kwenye mihangaiko natafuta ugali wa familia yangu. Nyie wote mnao andamana mmeisha shiba

HUO UGALI WA FAMIMILIA UTAUPATA KWELI KAMA HALI YENYEWE YA SERIKALI NI KUUCHAKACHUA KILA SIKU ZINAZOENDA KWA MUNGU?
ENDAPO UTAUPATA BASI WEWE NI WALE WALE au ndio yale mambo ya individualism ambayo haitakufikisha mabali ikiwa serikali itaendelea kijichotea mali kila siku mwisho huko unakokwenda kutafuta ugali utasikia kumeuzwa ammka acha ubinafsi.
 
hapa ndio baadhi ya watanzania wanaponiacha hoi anaona bora atafute pesa yake ajijengee kabarabara kinachotoka barabara kuu kuelekea kwake na hali barabara kuu imejaa mashimo na madimbwi na viraka gari hiyo inaharibika kila siku haoni kuwa akijishughulisha kutengeneza barabara kuu gari yake haitaumia kabisa kwa uchoyo anaona barabara kuu haimuhusu na watafaidi wengi mi naboresha ya kwangu.uchoyo ubinafsi

anaona ni heri kununua jenereta mtaa mzima uko giza huku akiumia kununua mafuta kila siku hajisumbui kuboresha hali ya umee mji mzima uchoyo ubinafsi unmua bila kujua kwani anakosa kwenda saluni,kuenjoy na marafiki kote kuko giza.uchoyo ubinafsi

anaona bore aibe akanunue vitu kwa vificho kwa gharama za juu kuliko kuboresha hali ya bei ya bidhaa zote ili hata asipoiba aweze kuishi watanzania tumekuwa wabinafsi bila nguvu ya pamoja hatutaweza kuiokoa nchi hii
 
Unatumia kinywaji gani? Sikuwekei sumu japo sikupendi.

Sitatumia kinywaji chochote, lakini ushauri wangu kwako, kama hao wakoswa kazi wakiandamana usijumuike nao ili yasikupate ya kukupata.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Kugoma ni muhimu sana, tena ni lazima. NABARIKI....tugome kuanzia ijumaa owards hadi kieleweke. ANGALIZO....lazima tujue tutakacho, yaani utanzania na uafrika wetu, sisi ni wamoja, iweje kuwe na Tandale na Masaki, mkazi wa wapi ni mtanzania halisi? Kama wote mbona hawafanani, nani mwenye haki ya kuwa na hisa kubwa ya rasilimali zetu kuliko mwingine? Hao wanaojiita wakombozi wetu (CHADEMA) ni propaganda tupu katika siasa, kwanini watofautiane na watanzania sisi? Kwanini tuamini katika siasa juu ya ukombozi wetu? "NO MORE POLITICS" Sisi wenyewe ndio wa kuwajibika, tuongozwe na nafsi zetu katika umoja na kuthubutu. Lazima pia tule kiapo kuwa, tutakachofanya ni kwa ajili ya watoto wetu, na sio sisi wenyewe. Kwangu mimi kuamini katka siasa ni kujisaliti na kujinafiki mwenyewe, (CHADEMA, CCM, nk wote wezi tu) tuamuae sasa
 
Narudi tena....

Mapinduzi (mabadiliko) yoyote, ni lazima yaanze ndani ya nafsi ya mtu!
Tupindue nafsi zetu kwanza, ni kitendo cha sekunde kadhaa tu! Tupindue fikra finyu na imani potofu katika nafsi zetu, tujenge mantiki ya kweli, mantiki iliyo katika kila nafsi ya mtu, yaani mantiki ya UTU. Ni lazima tukiri kuwa UTU ndio msingi mkuu wa maisha ya sisi waafrika wote (mkiwemo watanzania) . Thamani ya UTU, haizidiwi na mali wala damu!
Nasema hivi....MAISHA NI FURAHA, KAMA HAIPO BASI NI UPUUZI TUPU. Na hakuna furaha ya mtu ila watu, kwa kuwa furaha bila upendo imekufa....fikiria hili, "furaha ya simba mwenye njaa mawindoni, amuonapo mwanaswala mnono" furaha ya simba imekosa mantiki, kwakuwa ni ya upande mmoja tu, kumbe mantiki ya furaha ya maisha ni kuwa na uwiano sawa. Nauliza tena... Kuna aina ngapi za utanzania? Nani mwenye haki ya kumiliki hisa kubwa ya mlima kilimanjaro, mito, mabonde, madini na vyote vilivyomo, zaidi ya mwenzake? Je,ni sahihi kupaki maprado na ma-Vx kadhaa uwani, wakati jirani yako na watoto wake wanapiga mihayo ya homa kutokan na njaa, na wamejitanda kwa matambaa, chini ya maboksi ikiwa ni usiku wenye baridi kali? Mnakula hoteni kila siku na kushinda club, kuponda rasilimali ya masikini anayekufa mkekani kwa kukosa panado ya sh. 100! PUMBAVU! Bado tu tuwakenulie meno kwenye mikutano ya injili, mihadhara na ile ya siasa? Tule kiapo! Tusukumwe na Mantiki ya UTU iliyopo nafsini mwetu, na siku moja mifupa yetu aridhini, italoweshwa kwa mito ya machozi ya furaha kutoka katika macho ya watoto wetu" Sisi ni dhahabu, tusiogope kupita katika moto, huo ndio upendo wa juu kabisa kwa watoto wetu! Damu yangu i radhi, na ndiyo furaha yangu. Sijawahi kuwa na furaha hata siku moja, hata yako haina msingi, tuitafute ya kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom