Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..!

Nakuelewa sana kuhusiana na suala la vyama mimi mwenyewe baadhi ya viongozi Chadema siwaamini lakini hakuna alternative na kama kuna watu wenye zana na uwezo wa kukusanya watu na watu si wanachama tunazungumzia wananchi kwa ujumla ni viongozi wa vyama wenye nia ya kuleta mabadiliko. Cha muhimu ni message na message ni kwamba tunataka mabadiliko na serikali lazima iwajibishwe tumechoka mazungumzo tunataka action na matokeo
 
Baada wa Wamisri kuandamana nini kimefuata?Naona hali ya nchi hiyo imekuwa mbaya kuliko kipindi cha urahisi wa mubaraka.Sio maandamano yote yanayoleta tija.

Elewa makusudi ya hili, hatuipindui serikali bali tunataka serikali iache dharau na ifanye mabadiliko kutokana na ubadhirifu wa wazi ulioonekana. Fungua akili yako uungane na wenzako kuikomboa nchi yako kama una uchungu nayo, kama huna uchungu na yanayotokea kaa kimya sisi tutafanya kazi.
 
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda hapa nchini hivi sasa inabidi kwa kweli wananchi tuchukue hatua.

Tunachohitaji hapa sasa ni kuunganisha nguvu tu na inawezekana sana kwenda pale Mnazi mmoja Ijumaa, bila kufanya hivi JK anatuona sisi wote ni wapumbavu sana na yeye atazidi kuona ni jinsi gani anavyoweza kufanya lolote na mkapiga kelele yeye akasema lolote kisha akaendelea kuhudhuria misiba.
 
uandamane ili iweje, yaani unataka wananchi waache shughuli zao za kulijenga taifa ili washiriki huo upuuzi. Jaribuni muone. Kama manataka kutikisa kiberiti muone kama kina njiti, siku hiyo kitawaunguza.
.
"wasiosoma ni chakula cha wasomi".

ebu elezea wananchi wanachangia nini ktk kulijenga hili taifa? Ni upeo mdogo wa uelewa, kama hakuna uwajibikaji ktk serikali iliyokithiri rushwa na kutofuata sheria basi hata ujenzi wa taifa haupo, na wala taifa haliwezi kujengeka kiuchumi, litazidi kujengeka zaidi kimasikini kama inavyokuwa sasa
 
Mie nasema Ijumaa sintokuwepo ntakuwa kwenye mihangaiko natafuta ugali wa familia yangu. Nyie wote mnao andamana mmeisha shiba

sie wenye njaa tutajitokeza,bora kufa kwa risasi nikiwa nadai haki yangu kuliko mateso ya njaa kisa wewe ushiba pekee yako.unasema unaenda kusaka ugali au unaenda kucheza dili lingine kabla hatujawafilis
 
Mafisadi wana familia kubwa kwa sasa kwasababu hata watoto wao sasa wapo kwenye system na wanapigana na sisi sana, tusipofanya bidii kurudisha uwajibikaji hatuna muda mrefu hii nchi itakuwa ya kifalme.
 
"Moyo wa Ukombozi" ni fikra ya kuwafikiria wengine,ni kujitolea leo ili kesho watu wengine wanufaike. Hebu tuamke, tuwafikirie wengine wa kizazi kijacho,tusipothubutu leo basi tunachofanya ni kuwalundikia maumivu na madeni yasiyolipika kizazi kijacho. Haya shime'', zamu hii ni yetu baada ya Mwalimu na wenzake kuthubutu na kutupa fursa tuliyonayo leo kama Watanzania huru, sasa tuinuke tuunganishe myoyo,misuli na akili timamu ili tuimarishe Ukombozi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa hili.
 
Tuko pamoja sana Zandrany maana huu ndio moyo unaotakiwa kwenye kuikomboa nchi hii, tafadhali kaa tayari tutakapopeana habari kamili kwamba mikakati yetu itakuwaje ili kufanikisha maandamano haya ya kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko yenye tija.
 
Tusipoonyesha leo kuwa hatutaki kukubalikuwa tunadhulumiwa basi tutapotezwa na wakati na kubaki historia na wanetu watakojolea makaburi yetu na kusema kumbe wazazi wetu walikuwa mazezeta. Kujilimbikizia pesa na mali kwa ubadhirifu ni sawa na dinosour waliokuwa na miili mikubwa wakidahni wangeweza kuhimili mabadiliko ya dunia na leo hawapo tean waliobaki ni wale wenye vichwa vikubwa na matumbo madodgo.Magamba chukueni hatua, pesa zetu mnazoiba hata vitukuu vyenu vya pili haviatiikuta na vitaabika tu.
 
matusi ya nini mkuu..kama una hamu na virungu si uandamane tu!!

Wenye uchungu na nchi hii lazima watakuwa na hasira na matukio maana mambo yako wazi, ni ajabu sana kwamba bado wapo wenye kuitetea serikali hii inayokingia majambazi kifua waziwazi. Siku zenu zinahesabika kama wengine wote.
 
Uandamane ili iweje, yaani unataka wananchi waache shughuli zao za kulijenga Taifa ili washiriki huo upuuzi. Jaribuni muone. Kama manataka kutikisa kiberiti muone kama kina njiti, siku hiyo kitawaunguza.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

wajenge taifa kwa kukusanya kodi ela mle tukiongea iwe kosa..craap
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom