Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akilimtindi, Apr 24, 2012.

 1. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa haya yote yaliyotokea tangu jana sidhani kama kuna mwenye furaha ya kweli moyoni mwake leo, labda watu kama Maige, Nundu, Maige, Ngeleja na wengineo ambao waliponea tundu la simba siku ya jana. Kwa wengine wote wenye uchungu na Taifa hili naamini leo hawana raha kabisa na kwa vyovyote watataka kujua nini cha kufanya ili sasa tuone mabadiliko ambayo tumekuwa tukiyasubiri kwa siku zote.

  Nashauri tukubaliane kwa nia njema kabisa kugoma kwa kukaa majumbani mwetu siku ya Ijumaa tarehe 28/04/2012 ili kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko ya kweli. Hii haitotupa shida kubwa maana hatutakuwa na wasiwasi wa kupata virungu vya polisi ambavyo najua wengi wetu tunaviogopa ingawa kweli hasira tunazo za kiwangi fulani. Tununue vyakula na mahitaji mengine ya muhimu kuanzia leo na hii tutaitumia kama akiba wakati tunaishinikiza serikali kufanya tunachotaka. Wiki ijayo nadhani wataanza mchakato wa kukusanya maoni kuhusu katiba na hii wataipa publicity kubwa kujaribu kufunika hii hali iliyopo, let's igore the Katiba thing kwa sasa maana haina maana kwetu kwa hali.

  Mwisho nimeshauri tugome au tuandamane kwa maana ya kwamba kama Hasira zinatosha basi tuandamane, tuna uwezo huo na tunaweza kabisa kuandamana. Lengo liko pale pale kwamba tunataka serikali ifanye mabadiliko ya kweli sio kuipindua serikali. Hiyo ni kazi ndogo sana kama tukiamua na ukweli ni kwamba serikali yetu ni dhaifu sana kuanzia juu hadi chini, hata hao polisi wanaoringa nao hawapo wa kutosha kabisa kwahiyo tuache woga kabisa kama tupo tayari tuandamane. Tukiona ngumu tugome kwa kunyamaza kimya maana hata sisi tunaweza kunyamaza kwa kuacha kila kitu kwa kusema huu ni upepo tu...!
   
 2. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nahisi hadi ifike siku hiyo Vyama vya upinzani, Maaskofu, Masheikh na taasisi zingine zitakuwa zimetoa tamko pia
   
 3. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Uandamane ili iweje, yaani unataka wananchi waache shughuli zao za kulijenga Taifa ili washiriki huo upuuzi. Jaribuni muone. Kama manataka kutikisa kiberiti muone kama kina njiti, siku hiyo kitawaunguza.
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 4. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  maandamano haya yangetakiwa yasambae nchi nzima na ni vizuri yawe na kiongozi katika kila mkoa na kila wila ya na agenda.Usisahau kuwa serikali itayapinga kwa nguvu zote maana wana uzoefu wa MISRI,Libya,ALGERIA na kilichomkuta fisadi mmoja NICOLAI CAESESCUS huko Romania miaka ya 1989!Peoples power ni hatari kuliko tsunami
   
 5. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa hapa wana historia tu lakini hawana nguvu wala uzoefu wowote zaidi ya hayo mabomu ya machozi wanayotengeneza hapo Morogoro ndiyo maana kila wakiitwa mahala wanayatwanga tu kwa kujua wanayo mengi ya kuchezea na kuona watanzania wanavyotoa machozi huku wakijua wazi wanawaliza kwa kuwakabia haki zao. Nguvu yetu ni kubwa sana kulingana na nguvu ya kataifa haka kadhaifu ka Afrika Mashariki, tukijiweka sawa wala haichukui muda ni kitendo cha siku chache sana.
   
 6. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siku zenu zinahesabika, mbinu za kuwatimua hazitugharimu akili zetu hata chembe. Ni suala la muda na kupanga tu..!
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mawazo butu!
  Uvivu tu wa kazi na ukosefu wa hoja ndio huwafanya watu wakimbilie kugoma.
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  nakushauri uondoe avatar maana maelezo yako hayafanani na huyo mwenye sura yake
   
 9. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uvivu wa kufikiri, vyakula vya bure, kusubiria ahadi za uongo ni kati ya mambo yanayofanya watu kama wewe kuendelea kuwepo na kuwa na nguvu za kuandika ujinga, siku zako si nyingi na nakushauri kuukana ujinga wako usijeigharimu familia yako baadaye maana hawataweza kukimbia wakati itakapokubidi wewe kukimbia.
   
 10. k

  kicheche999 Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wewe 100% tufuate wito wa Tahrir square tuwasihi viongozi kama Lema au Zitto mwenyewe kuwa tanataka maandamano mama viwanja vya mnazi mmoja kila Ijumaa kuanzia 27/4/12 hadi serikali au "viongozi" wawajibishwe. Watu 50,000 tu wakijitokeza mnazi mmoja JK atajinyea ikulu. Spread the word my brother this is very possible and its worth a try
   
 11. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nonesense. Shame on you stupid bastard.
   
 12. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja na hii ndio action tunayotaka ichukue nafasi kwa sasa, hao Lema na Zitto wakija wakaongeza nguvu ni sawa lakini kwa sasa ili hii issue ibaki Hot lazima tui-hit kwa kuonyesha kwamba hatujakubaliana na upumbavu wao.
   
 13. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Jamani maandamano yatafaa sana but ingekuwa vyema tungepata viongozi wenye influence like prophet lema au kabwe zitto ili watuongoze na sisi tupo tayari sema tu tunataka mtu wa ku2mobilize.
   
 14. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunakubaliana sana na ushauri wako lakini wao naamini lazima wakae kikao ili kuamua jambo la pamoja, na huenda inaweza kuchukua muda kidogo kupanga mikakati. Letu sisi kama wananchi ni kugomea kila kitu kuanzia Ijumaa 28/04/2012 kuelekea wikiendi kisha Katiba nayo tunaigomea jumla maana haitusaidii kwa mwendo huu. Kama serikali haiwezi kuwajibika kwa hili ni dhahiri hata katiba hawatafanya zuri hata moja na dalili tulishaziona tangu huu mchakato ulipoanza.
   
 15. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna mwenye mawazo tofauti kuhusu tarehe niliyoshauri kugomea? nimeshauri tarehe 28/04/2012 lakini nakaribisha maoni tofauti iwapo hoja itaonyesha umuhimu wa kufanya hivyo. La msingi hapa ni kutoa uamuzi wa pamoja kwamba ni lini na tufanyeje siku hiyo kama kuna kuambatanisha na mgomo huo wa kukaa tu nyumbani.
   
 16. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,811
  Likes Received: 2,753
  Trophy Points: 280
  Natamani ningekuwa Dar, Mnazi Mmoja, siku ya kusanyiko hilo. JK lazima aione nguvu ya umma!
   
 17. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dar kuna watu wengi sana wenye uchungu na nchi hii, ni kitendo cha kuamua tuu na kujipanga. Wangapi wako tayari tuwe pale kiwanjani siku hiyo?
   
 18. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Zitto Kabwe yupo Jahazi la Clouds FM sasa hivi, tuwasikie nao wanasema nini kuhusu ujinga wa serikali hii
   
 19. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Najaribu kusikiliza hili Jahazi la Clouds FM na kauli za viongozi walioshiriki sana kuwasha huu moto bungeni (Zitto na Filikunjombe) wakiulizana kwamba nini haswa kifanyike au nini haswa kitaendelea sasa. Najua ni ngumu wao kusema kitafanyika nini sasa lakini sisi tunasema halijaisha lazima hili lifanyiwe kazi tena mapema na sisi tunashauri Ijumaa ni siku nzuri kuionyesha serikali nini inatakiwa kufanya wakati huu. Ijumaa tuonane pale Mnazi mmoja, kuna mtu alishauri 50,000 ni wengi sana na mimi naona ni wengi kabisa.

  Nape anasema wabunge wana haki ya kujadili utendaji wa serikali, ati anasema ccm inaamini serikali imekuwa sikivu na wanaamini kweli serikali itafanyia kazi. Anadai serikali inatakiwa kufanyia kazi haya mambo mapema, nadhani kuna woga unaoendelea ndani ya ccm kwa sasa maana maongezi ya Nape yanaonyesha woga mkubwa kwa hali jinsi ilivyo.
   
 20. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  haya maandamano tushayazoea ngoja tuone nini kitatokea hiyo furahiday..
   
Loading...