Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..!

Tugome au Tuandamane Ijumaa tarehe 28/04/2012. It's worth it..!

haya maandamano tushayazoea ngoja tuone nini kitatokea hiyo furahiday..

Safari hii hatutaki mazoea tunataka kazi na wewe unatakiwa uwe mmojawapo maana tunajua maandamano sio ya mtu mmoja, la msingi kama unaona Mnazi mmoja pagumu kaa nyumbani maana njia za kugoma zipo nyingi. Inawezekana kuwa hapo Mnazi mmoja au unaweza kuamua kukaa nyumbani ndio maana wazo langu mapema ilikuwa kukaa nyumbani kama huoni kwenda Mnazi mmoja kuna umuhimu.
 
Najaribu kusikiliza hili Jahazi la Clouds FM na kauli za viongozi walioshiriki sana kuwasha huu moto bungeni (Zitto na Filikunjombe) wakiulizana kwamba nini haswa kifanyike au nini haswa kitaendelea sasa. Najua ni ngumu wao kusema kitafanyika nini sasa lakini sisi tunasema halijaisha lazima hili lifanyiwe kazi tena mapema na sisi tunashauri Ijumaa ni siku nzuri kuionyesha serikali nini inatakiwa kufanya wakati huu. Ijumaa tuonane pale Mnazi mmoja, kuna mtu alishauri 50,000 ni wengi sana na mimi naona ni wengi kabisa.

Nape anasema wabunge wana haki ya kujadili utendaji wa serikali, ati anasema ccm inaamini serikali imekuwa sikivu na wanaamini kweli serikali itafanyia kazi. Anadai serikali inatakiwa kufanyia kazi haya mambo mapema, nadhani kuna woga unaoendelea ndani ya ccm kwa sasa maana maongezi ya Nape yanaonyesha woga mkubwa kwa hali jinsi ilivyo.

Mie nasema Ijumaa sintokuwepo ntakuwa kwenye mihangaiko natafuta ugali wa familia yangu. Nyie wote mnao andamana mmeisha shiba
 
No retreat no surrender. Aluta continua.

We have to find out an alternative to this forum understanding, members won't have collectively one mind. I know I'm not popular here because I never use to be very active at most times. I'll have to spend time in the forum now, consider me an active member from now onwards..!
 
Sikukuu ya muungano siku nzuri sana ya kufikisha ujumbe kwa mabango.
 
Wa Egypti wasinge weza kufanikiwa bila maandamano ya tahrir square. Sikubaliani na hoja ya kukaa nyumbani kwa sababu mkusanyiko wa watu ndio chanzo cha kuvua watu uoga na kuavisha empowerment. Na mimi nasema hii hoja ifikishwe Chadema au kwa Zitto mwenyewe kwani hao ndio wanauwezo wakuleta watu wakutosha mnazi mmoja. Kama kuna mtu ana email ya Chadema au viongozi wake naiomba niweze kupendekeza hii hoja
 
Kicheche999 nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa sana, cha msingi tukubaliane kwamba sasa tunahamasishana kwamba kazi ni pale mnazi mmoja hiyo ijumaa. Mawasiliano ya Chadema haya hapa Anuani za Wanachama wa CHADEMA na naamini kila mtu akiwasiliana na CDM kupitia kokote ama kupitia info@chadema.or.tz na kuwaeleza tupo tayari kwa lipi basi naamini nao wata-respond kwakuwa hata wao wanachosubiri ni sisi tuelimike na kuwa tayari kuchukua hatua.
 
Hata mkeo yuko hivi ndio maana unampenda, tupe mawazo rasmi sasa maana tumekusubiria kwa muda.
Mambo ya mke wangu yanakujaje hapa?
Unafaahmu kuwa hii sredi inatishia amani ya nchi? Sidhan kama JF inaruhusu sredi kama hizi ziendelee kuwepo. Ngoja niwashtue mods waitoe.
 
Wa Egypti wasinge weza kufanikiwa bila maandamano ya tahrir square. Sikubaliani na hoja ya kukaa nyumbani kwa sababu mkusanyiko wa watu ndio chanzo cha kuvua watu uoga na kuavisha empowerment. Na mimi nasema hii hoja ifikishwe Chadema au kwa Zitto mwenyewe kwani hao ndio wanauwezo wakuleta watu wakutosha mnazi mmoja. Kama kuna mtu ana email ya Chadema au viongozi wake naiomba niweze kupendekeza hii hoja

Mkuu natofautiana na wewe kidogo kwenye swala la Chadema kuongoza hii kitu. Ukweli ni kwamba tumeguswa wengi sana na huu upuuzi (wenye kadi za vyama vya siasa na ambao hatuna vyama) in a sense watanzania wengi wanahasira ajabu. Sasa naona ni muhimu hii kitu ikaongozwa na watu neutral ikiwezekana NGO'S kuliko watu wa vyama vya siasa, hii itaondoa dhana ya kwamba hii ajenda ni political propaganda (hili ni wazo langu). However wana CCM, CDM, TLP, NCCR wanaruhusiwa pia kuwepo kwani wao pia ni watanzania.
 
Mambo ya mke wangu yanakujaje hapa?
Unafaahmu kuwa hii sredi inatishia amani ya nchi? Sidhan kama JF inaruhusu sredi kama hizi ziendelee kuwepo. Ngoja niwashtue mods waitoe.

Tunahitaji mawazo yako maana maandamano yanakuja kwa kukosa response ya serikali, unayo maoni yeyote au unaomba tu mods waondoe hii thread kwasababu inakukera? Hatutashangaa lakini hiyo haibadilishi lolote, ukishapata cancer ukigusa kidonda haimaanishi kidonda kimeisha ila ujue kinakuja kwa nguvu zaidi. Tupe maoni kama unayo vinginevyo na wewe tunakuweka kwenye list ile iliyoleta sera za ajabu mchana, muda wako pia utahesabika.
 
Mi nakuunga mkono hili kwa asilimia mia moja!! lazima tuonyeshe msimamo km watanzania wenye uchungu na nchi yetu. Siyo lazima chadema waanzishe , hata maandamano ya tahrir yalianzishwa kwa mtu moja kujichoma moto.... saa ya ukombozi ni sasa WATANZANIA TUONDOE WOGA , TUIKOMBOE NCHI. TANZANIA SIYO WA WANACCM, WALA WANACHADEMA, TANZANIA NI YA WATU WOTE WALIORAIA WA WATANZANIA. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU TUBARIKI NA UTUPE MOYO WA UJASIRI WA KUMSHIDA ADUI WA HAKI. ULITUPA NCHI ULIYOIBARIKI KWA MIKONO YAKO NA UKATUWEKA TUISHI HUMO NA TUFAIDI MATUNDA YA NCHI HII, ILA SI KUTESEKA NA KUWA WATUMWA WA WACHACHE. MUNGU TUTIE NGUVU NA MOYO.
 
Mkuu natofautiana na wewe kidogo kwenye swala la Chadema kuongoza hii kitu. Ukweli ni kwamba tumeguswa wengi sana na huu upuuzi (wenye kadi za vyama vya siasa na ambao hatuna vyama) in a sense watanzania wengi wanahasira ajabu. Sasa naona ni muhimu hii kitu ikaongozwa na watu neutral ikiwezekana NGO'S kuliko watu wa vyama vya siasa, hii itaondoa dhana ya kwamba hii ajenda ni political propaganda (hili ni wazo langu). However wana CCM, CDM, TLP, NCCR wanaruhusiwa pia kuwepo kwani wao pia ni watanzania.

This is a lot better unstoppable, sasa tuwasukume akina nani watuongoze katika hili? Kibamba anafaa au tuwatafute akina Kijo Bisimba? tutawasiliana vipi na hao watu ili haya mambo yafanyike kwa mpango wa kueleweka? kikubwa hapa kinachohitajika nii mobilization na hiyo ikifanyika sasa nadhani utakuwa ni muda muafaka kabisa. Hatuipindui serikali lakini tunaishurutisha serikali kufanya mabadiliko ya ukweli.
 
Wa Egypti wasinge weza kufanikiwa bila maandamano ya tahrir square. Sikubaliani na hoja ya kukaa nyumbani kwa sababu mkusanyiko wa watu ndio chanzo cha kuvua watu uoga na kuavisha empowerment. Na mimi nasema hii hoja ifikishwe Chadema au kwa Zitto mwenyewe kwani hao ndio wanauwezo wakuleta watu wakutosha mnazi mmoja. Kama kuna mtu ana email ya Chadema au viongozi wake naiomba niweze kupendekeza hii hoja

Baada wa Wamisri kuandamana nini kimefuata?Naona hali ya nchi hiyo imekuwa mbaya kuliko kipindi cha urahisi wa mubaraka.Sio maandamano yote yanayoleta tija.
 
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda hapa nchini hivi sasa inabidi kwa kweli wananchi tuchukue hatua.
 
Nadhani ni wakati muafaka kwa serikali yetu kuwa sikivu....kwa jambo hili yatubidi wananchi kuchukua hatua za haraka kuionesha serikali kuwa tumechoka
 
Mi nakuunga mkono hili kwa asilimia mia moja!! lazima tuonyeshe msimamo km watanzania wenye uchungu na nchi yetu. Siyo lazima chadema waanzishe , hata maandamano ya tahrir yalianzishwa kwa mtu moja kujichoma moto.... saa ya ukombozi ni sasa WATANZANIA TUONDOE WOGA , TUIKOMBOE NCHI. TANZANIA SIYO WA WANACCM, WALA WANACHADEMA, TANZANIA NI YA WATU WOTE WALIORAIA WA WATANZANIA. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU TUBARIKI NA UTUPE MOYO WA UJASIRI WA KUMSHIDA ADUI WA HAKI. ULITUPA NCHI ULIYOIBARIKI KWA MIKONO YAKO NA UKATUWEKA TUISHI HUMO NA TUFAIDI MATUNDA YA NCHI HII, ILA SI KUTESEKA NA KUWA WATUMWA WA WACHACHE. MUNGU TUTIE NGUVU NA MOYO.

Tunashukuru sana kwa sala yako ndugu yangu Remon, kikubwa hapa kweli tunachotafuta ni namna ya kuwapata watu wa kutosha kuandamana. Kwanza mimi nilishauri tugome kwa kukaa tu kimya majumbani mwetu, kicheche999 akasissitiza hiyoo haifai itakuwa woga na mimi nimemkubalia. Sasa inatakiwa tukusanyike pale Mnazi mmoja kwa shughuli rasmi Ijumaa ya tarehe 27/04/2012. Tunachohitaji hapa ni tumpate mhamasishaji mmoja afanye hii kazi na imekadiriwa tukipata watu 50,000 wanatosha kabisa kuanza hii kazi, mimi nahisi kwa hali iliyopo tunaweza kabisa kupata watu wengi zaidi kabisa. Wengi walishazoea maneno kwenye hili kwahiyo tunataka mpango kamili kwamba tunafanyaje hili jambo lifanikiwe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom