TUGHE: Zitto Kabwe ashtakiwe

TUGHE: Zitto Kabwe ashtakiwe

Status
Not open for further replies.
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Nchini (TUGHE) kimetaka Zitto ashtakiwe kwa kutamka mshahara wa Rais na Waziri Mkuu hadharani.

Kwani wao hawaruhusiwi kwenda mahakamani ? Si waende wao !
 
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.
Kumbe Rais kawekwa madarakani na nani kama si wananchi? kajiweka madarakani? kwani Urais ni Ufalme? Acha ushabiki na mihemko ya kipumbavu, yaani unaweka hapa mawazo ya kumtukuza rais kama Mungu? Mwajili wa serikali yeyote halali madalakani, ni umma. na ndio maana umma (hadhara) inaweza kuiondoa madarakani serikali au kiongozi. jifunze kinachoendelea nchi nyingi. rais na serikali yake, wanalipwa KODI za wannanchi, kama ingekua wananchi hawajawaajiri basi tusingewalipa kodi zetu! Elewa, usikurupuke.
 
{Kura zenu laki 4 tuu sizihitaji}JK aliwaambia wazee wa dar wakati wa mgomo wa walimu akiwa diamond jubilee.TUGHE ACHENI KUJIPENDEKEZA
 
kwani wananchi wote ndo wamemwajiri Rais? Ni wale tu waliopiga kura na kumchagua JK ndo wanapaswa kujua mshahara wake na si wananchi wote. yaani hata machadema nanyi mnajiita ni mwajiri wa JK?
kwani pesa anazolipwa rais na mawaziri ni KODI za wale waliompigia kura tuu?? Fikiri kwa uziada, ushabiki na mihemko ya kukurupuka, mara nyingine hudharirisha utu wako. kua na mwono huru.
 
kazi kweli.... mtu anauliza mpigakura amemuajiri vip RAIS.........!
 
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.

kwa hiyo kaajiriwa na babaako? hujui kuwa vyeo vyote vya kisiasa waajiri wake ni wananchi kupitia kura zao?
 
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.
Kumbe CCM ndo mnavyotuchukulia wananchi!
 
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Nchini (TUGHE) kimetaka Zitto ashtakiwe kwa kutamka mshahara wa Rais na Waziri Mkuu hadharani.
Wanajipendekeza tu kwani kujua mishahara ya hao watu kuna tatizo gani zaidi ya kuwajuza kiasi ambacho wanachi wananyonywa kodi zao
 
Mungu wangu TUGHE hawatoi jasho wanakula tu michango ya wanachama wake, keeping relaxing and chewing others money - wakati wanachama wake wanasaga rumba, wamekazania urasimu tu, I hate TUGHE na aina yote ya Trade Unions za kitanzania, ni vijiwe tu, angalia Trade unions za Kenya,Africa Kusini wakikohoa tu govt inasikiliza!
Hivi TUGHE ni chama cha Wafanyakazi/wana-taaluma gani?

Serious hata angekuwa RAIS wa CHODAWU (no disrespect) asingeweza kutoa kauli hii ya STONE AGE.

Huyu RAIS wa TUGHE is an OBTUSE PERSON LIVING IN A DIFFERENT PLANET!
 
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.


Huyu chabruma amesoma kweli hata darasa la saba? hajui kuwa sisi ndo waajiri wa Rais? da!! kweli ule utafiti wa juzi kuwa asilimia....ni.....kumbe ni kweli aiseeee!!
 
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Nchini (TUGHE) kimetaka Zitto ashtakiwe kwa kutamka mshahara wa Rais na Waziri Mkuu hadharani.

Poor tughe, wachumia matumbo wakubwa. Mnaacha kutetea maslahi ya wanachama wenu wanaolipwa mishahara duni na kukatwa kodi kubwa badala yake mko busy kujipendekeza kwa mafisadi papa, wanaojipangia mishahara mikibwa tena bila kukatwa kodi hata senti. Shame on youuuuuuu tughe.
 
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.

Wewe hujitambui kabisa, hivi unajua serikali makini zinavyowajibika kwa wananchi ambao ndio waajiri wao? We mburula squared
 
HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.

Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.

Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.

Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.

“Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.

Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.

“Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.

Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.

“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.

Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.

Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.
 
Dah nina kila sababu ya kutojiunga TUGHE, hawa jamaa ni wajinga kupindukia. Mi Nilitegemea wao wangeanzia hapo kulianzisha, yaani wao wanaona tofauti hii ya mishahara Kati ya viongozi wa juu na wa chini ni kawaida kabisa. Mshahara wa mwl kuingia mara 50 kwa mshahara wa waziri mkuu wao wanaona sawa tu. Kuna watu hata hawajui wapo hapo walipo kwa sababu gani. TUGHE ni janga pia.
 
kwani wananchi wote ndo wamemwajiri Rais? Ni wale tu waliopiga kura na kumchagua JK ndo wanapaswa kujua mshahara wake na si wananchi wote. yaani hata machadema nanyi mnajiita ni mwajiri wa JK?

Wakati wa kulipa kodi hakuna MACHADEMA wala MA CCM Rais ni mwajiri wa walipa kodi so ni lazima tujue mshahara wake na hao kenge wanao lalamika wakae pembeni kama wanaona noma mishahara yao kujulikana wajiuzulu watu kibao wanazihijaji hizo ajira.
 
As long as upo kwenye system ya Malipo mshahara wa mtu si siri,
 
"mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa"
Naona anasahau kama sisi ndiye waajiri wenyewe.
 
Em tufumbuane macho hasara za kutaja mshahara wa rais njenje ni ipi?
Ma rais wengi tu mshahara wao unajulikana hata Obama mshahara wake kaweka hadharani $400,000 kwa mwaka.
Sasa inakua vipi hapa??
 
Kwa maoni yangu kiini hasa cha kutaka mishahara ya viongozi wa juu iwe siri ni kwamba wamejipangia mishahara mikubwa mno ikilinganishwa na hali halisi ya nchi yetu kiasi kwamba hata wao wenyewe wanahofia wananchi uenda wakawajia juu wakibaini uporaji huo. Katika hali hiyo kauli ya TUGHE haina mshiko wowote. Kiini chake ni uroho wa viongozi wa chama hicho wanaojaribu kujipendekeza ili kuganga njaa yao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom