TUGHE: Zitto Kabwe ashtakiwe

TUGHE: Zitto Kabwe ashtakiwe

Status
Not open for further replies.
Nimesoma comments za watu kwenye topic inayohusu TUGHE kumlalamikia Zitto Kabwe,na comments za mtu anayejiita CHABRUMA zimenichefua kweli,labda Tanzania imejazwa na watu wenye upeo Kama wa huyu bwana ambaye hajitambui kabisa,nadhani tunaweza kumsaidia ndugu yetu huyu kwa kulitumia jina CHABRUMA kumaanisha mtu aliyeenda shule akajua kusoma na kuandika ila hajui kufikiria hata kidogo na hajitambui hata kwa chembe ili ku raise concern ya namna Elimu yetu kwamba sio tu inatengeneza watu wasiojua kusoma na kuandika Bali pia kundi kubwa la wale wanaojua kusoma na kuandika hawajui kufikiria kabisa,naomba kuwasilisha hoja!
Hii ni chang'aa au kiroba?
 
Great minds discuss ideas while very small minds discuss people.
cc.
mleta mada na genge lake
 
Mnahangaika na watu wa lumumba wasiojielewa.kama chabruma ni id ya Jakaya sitashangaa sana kufanya vile kwa kujitetea kwenye hilo li kitumbua lake(japo kiukweli si vyema).ila kama ni mlalahoi kama walivyo wabongo wengi basi atakuwa amevurugwa vibaya sana.
Kamalizie usingizi ksha ukiamka unawe uso ndio urudi hapa uokote okote mia mbili mia mbili zako.
 
mkuu, hawa wanahangaika sana. yaani mtu anayejitolea kuwaelimisha na kuwaeleza ukweli wao wanamwona mbaya. hizo ndo dalili za chama kufika ukingoni
Hao ndio bar ya vichaa bana. Wameishiwa hoja wamebaki kusubiri matukio. Km imefika wakati mtu anaamka asbh anamwanzishia mwenzake thred, sio kufilisika kifikra huko? Poor you machadema
 
Kuliko Kuwa bavicha ni afadhali mara mia uwe kichaa uokote makopo jalalani
 
mkuu, hayo ni mawazo yako na wala hakuna atakayekushurutisha kuamini waaminiyo wenzako
haina haja ya kubishana na Sir E.J Buyamba, huyu ni house boy wa Dr Slaa lazima atetee chakula kama umewahi kufika kwake yeye kazi yake ni kufua na kuosha gari, na kumwendesha Josephine. kubishana na bekitatu unaweza pasuka kichwa hawa kila koment Jf wanalipwa Tsh. 35.00/= wao hawadili na mada bali kukuchanganya na wewe huonekane kiplate kama wao.
 
Wananchi ndo waliomwajiri Kikwete na wana haki ya kujua mshahara wake. Huna haja ya kumuita mtu mburula; jenga hoja usijeonekana mburula!

Kaka huyo sio mburula,ni zaidi ya mburula,huyo ni Chabruma
 
Tughe ni chama ambacho kinaongozwa na viongozi ambao ni mafisi kwani Hawana faida yoyote kwa wafanyia kazi
zaidi ya kula na kufanyia ufisadi mkubwa kwa pesa za wanachama kuna ubaya gani kutaja Mashahara wa Rais au pinda
acheni kujipendekeza. Mafisi wakubwa mnashindwa kutetea wafanyia kazi mnatetea viongozi


wewe una wazimu nini? umekurupuka ulipotoka unakuja kureply vitu ambavyo hujui hata vimeanzia wapi. soma kwanza toka mwanzo ndio uanze kupayuka.

sisi tuteteee viongozi kwa ushenzi wanaowafanyia wananchi tutakuwa na akili timamu?
 
Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya (TUGHE) kimemlaani Mh Zitto Kabwe kwa kuweka hadharani mishahara ya wabunge, mawaziri, waziri mkuu na rais.

Lengo la Zitto kutaja mishahara ya vigogo lilikuwa kuonyesha jinsi gani wanasiasa wanavyojilipa mamilioni ya pesa za walipakodi huku wafanyakazi, hasa wa kada ya nchini (walimu na wengineo) wakilipwa mishahara midogo ambayo haizidi hata posho ya mbunge kwa siku moja!

TUGHE ni chama kinachopaswa kutetea maslahi ya wafanyakazi, hasa madai ya nyongeza ya mishahara, kupandishwa vyeo, madai ya pesa za nauli, posho, nk. Kwa hiyo, TUGHE hawakupaswa kumlaumu Zitto bali wangemsifu kwa kuanika hadharani mishahara ya vigogo, ambao hutumia zaidi ya nusu ya pesa zinazotengwa kwa ajili ya mishahara ktk nchini nzima. Yaani kikundi kidogo cha watu wasiopundukia 500 wanalipwa zaidi ya nusu ya mishahara ya serikali!

Ulipaji mishahara wa ovyo kama huu, usiozingatia usawa, ndio unapelekea serikali kugoma kuwaongeza wafanyakazi mishahara kwani sehemu kubwa ya pesa ambazo zingetumika kuongezea mishahara huishia matumboni mwa kikundi kidogo cha wateule wachache--ambao ni peke yao tu waliobarikiwa kuishi maisha bora.

Kwa hali kama hii nilitegemea kwamba TUGHE wangemuunga mkono Mh Zitto kuibana serikali iboreshe mishahara ya wafanyakazi wa kada ya chini badala ya kuzidi kuwalundikia posho wabunge, mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi huku wafanyakazi ngazi ya chini wakizidi kufa njaa kila kukicha. Nina wasiwasi kama kweli TUGHE wanatetea masilahi ya wanachama wao au kama wanatetea masilahi ya serikali inayowakandamiza wafanyakazi wataalam huku ikiwabeba wanasiasa. Sina imani tena na chama hiki katika kutetea maslahi ya wanachama wake. Hiki ni chama cha kinafiki na kindumilakuwili na kamwe hakiwezi kutegemewa kuwatetea wanyonge ikiwa viongozi wake wana mawazo mgando na tabia za kifisi kama hizi. Wanachama wa TUGHE mtakuwa mmeng'amua aina ya chama mnachokitegemea kuwatetea dhidi ya ukandamizaji wa serikali. Hiki ni chama cha ovyo kabisa kuwahi kuwapo katika ardhi hii ya Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom