Tugawane nchi katikati

Ukiambiwa utaje madhara ya kupigwa tone tone, basi kuchanganyikiwa kiakili kama mleta mada na waungaji mikono wake usiache kuitaja katika madhara Yako.
 
Ni vyema. Jee muungano bado uwepo? Sio tatizo tena?
 
Naona pwani yetu , Zanzibar , Tanga , Mtwara , Dar , lindi tukiwa na kila kitu yaani ..Bahari zote kwetu , gas na kilimo cha kutosha , hakuna riba kwenye bank zetu .

Tunaondoa kabisa mfumo wa kidemokrasia , tunatafuta mzawa.. Hatutokuwa na stress kabisa ..
 
Katiba haimalizi matatizo ya utamaduni, huelewi wapi?

Pia, Katiba imempa kiongozi gani madaraka bila ukomo?

Unaweza kuweka kifungu hicho hapa tukijadili?
Vipo vifungu,
1. Rais anateua kila mtu katika mihimili yote, hadi mtendaji mkuu wa bunge!
2. Matokeo ya uchaguzi ya Rais hayahojiwi popote
3. Bajeti ya Ikulu haidhibitwi
4. Rais anaweza kuunda idadi yoyote ya mikoa, wilaya na wizara.
5. Rais hashitakiwi mahakamani kwa kosa lolote.
6.Rais ana mamlaka yasiyodhibitwa katika kusaini watu wanyongwe.
7.Rais anaweza kupanga bajeti yoyote nje ya bunge.
 
Hata sasa Pwani ni yenu ila mmeishia kuuza bandari tu.
 
Somalia wanakila kitu na demokrasia hawaitaki lakini hawajatoboa
 
Mkishajitenga kama mlivyosema. Tayari mtakuwa na ile ingridient muhimu ya fujo
Chanzo cha fujo ni hao tunajitenga nao, sisi katiba mpya itatuongoza vyema
 
🤣🤣🤣🤣 Hata mimi hapo kwa Maconder kuwa rais bora nihamie Haiti
 
Muweke maneno vizuri, ukisema madaraka bila ukomo unaweza kusomeka kuwa katiba inampa rais urais usio na ukomo.

Madaraka ya rais yana ukomo term ya urais inapoisha.

Tanzania kuna term limits.

Ila kwa muktadha wako, rais ana madaraka makubwa sana, si madaraka yasiyo na ukomo.

Kwa sababu katiba hiyo hiyo in principle imetoa hata impeachment procedure ya kumuondoa rais.

Enough with the hyperbokes. Yiu don't need them to make a point and it only makws you look disingenuous.
 
Kwenye muungano watajuana CCM na wazanzibar, kipande chetu hatutaki muungano
Huenda unazungumza ukiwa huna kumbukumbu au Tanzania huijui au umeisahau. Kwenye huu muungano, au kwenye makubaliano ya huu muungano hakuna swala la Chama. Liliopo ni Tanganyika na Zanzibar. Ukitaja Chama ni kama umejisau. Swala hapa ni muungano na wala sio chama. Jee muungano uwepo, kwamba leo umekuwa mwema, au usiwepo?
 
Muungano usiwepo, hauna manufaa kwetu,unawanufaisha zaidi wazanzibar,sioni faida yoyote yamuungano Tanganyika
 
Muungano usiwepo, hauna manufaa kwetu,unawanufaisha zaidi wazanzibar,sioni faida yoyote yamuungano Tanganyika
Nakubaliana nawe kwamba muungano usiwepo. Sikubaliani nawe kwamba muungano unawanufaisha zaidi Wazanzibari. Jee hili la kuwanufaisha zaidi Wazanzibari limeanza 2021 au kabla? Ikiwa ni kabla ulikuwa wapi wakati huo hujasema, unasema leo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…