Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 11,523
- 18,233
Tatizo uliloleta jukwani linachangiwa na changamoto kuu mbili ambazo ni (i) Mitaji na (ii) Soko la mazao ya kilimo.
Tutafanikiwa kutatua au kupunguza changamoto ya kwanza (i) Mitaji kwa kushughulikia na kulimaliza tatizo la pili (ii) Masoko kama ifuatavyo:
Mashariti ya mikopo ya miradi ya kilimo kama ya TADB siyo rafiki kwa wajasiriamali vijana ambao wana ndoto lakini hawana mitaji, changamoto hii inaenda mbali zaidi kwani vijana wenzao hawazielewi ndoto zao ili kuweza kuungana nao kama kikundi waweze kukopesheka kwa mashariti ya vikundi.
Changamoto ya masoko ya ndani
Mpaka sasa sijawahi kuelewa ule utaratibu wa madalali wa mazao wanao nyonya wakulima masokoni Tanzania kote. Kwanini mkulima asifike sokoni na mzigo wake kisha kuoneshwa eneo na kushusha mzigo wake bila kulazimishwa akabidhi mzigo wake kwa dalali?
Suala la ulinzi, ushushaji mzigo n.k. liratibiwe na uongozi wa soko.
Hawa viongozi wa soko wapo sokoni kufanya kazi gani?
Madalali wanatengeneza curtail masokoni na kulalia wakulima na walaji. Hawa madalali wanafanya bishara flani kama muundo wa mafia mobs wa kudhibiti eneo la soko.
Ufumbuzi tatizo la madalali wa sokoni
Ufumbuzi zaidi kuhusu elimu ya Masoko ya Nje na ndani kwa pamoja
Elimu ya kutafuta masoko ya nje na ndani ya bidhaa za kilimo hayaja wekewa mkazo huko mashuleni na vyuoni, na kwenye media zetu chini ya ufadhili wa wizara ya kilimo au viwanda na biashara. Kwa sasa wahitimu wa vyuo vikuu vya kilimo waliounda kampuni au vikundi wamewekeza kwenye kutuoa elimu kwa wakulima jinsi ya kulima kwa lengo la wao kuja kuwauzia wakulima pembejeo, mbegu, na huduma za consultation tu. Hawa wadau muhimu hawasaidii kutafutia wakulima masoko ya uhakika kwa muundo wa mikataba.
Kinachotokea wakimuuzia huduma hizo mkulima anaweza kupata mavuno bora lakini msimu unaofuata hawezi kuendelea na kilimo sababu amekosa masoko na kupata hasara. Hapo utaona hata hawa wahitimu wanampoteza mteja na biashara yao inayumba, hakuna muendelezo wa miradi(no sustainability).
Serikali kupitia wizara husika haisaiidii kuwajulisha wakulima wengi uwepo wa fursa ya soko la zao flani nje ya nchi na kuwaunganisha wakulima na wateja wa huko nje.
Ukisikia tangazo ukienda wizarani haupati msaada unazungushwa tu badala ya kuunganishwa na mteja na kusaidiwa kutafsiri mashariti ya mteja, akienda mwanasiasa mkubwa kama mbunge au waziri ndiyo anasaidiwa lakini hawa wengi hawana wito wa hiyo biashara, biashara zao nyingi zinakufa kwa kukosa ufuatiliaji. Huyu mwanasiasa kwake kilimo siyo shughuli kuu ya kumuingizia kipato bali ni shughuli(kazi) ya ziada hivyo hawekezi muda wake mwingi kwenye shughuli hiyo unakuta anahujumiwa na wafanyakazi wake kisha anafilisika huku akiwa amezuia fursa kwa vijana ambao wangetumia vizuri fursa hiyo ya soko na mtaji na kufanya kilimo kama ajira yao pekee.
Elimu ya usindikaji mazao ya shamba pia haijapewa nguvu kubwa kwa watu wa kawaida ndiyo maana nyanya zina ozea sokoni au shambani. Kwa waliopata hiyo elimu hawajapewa mitaji kwa mfumo wa ruzuku au mikopo, kisha wafuatiliwe na wasimamizi maalum kuangalia wapi wanakwama.
Uingizaji toka nje au ujengaji wa viwanda vya malighafi kama kemikali zinazotumika kwenye usindikaji bado ni changamoto, wakati wenzetu kama Kenya naona kuna Taasisi inatoa mafunzo kwa nguvu na upatikanaji wa kemikali za usindikaji ni rahisi sana. Jamaa wanasambaza vitini hadi mitandaoni. Serikali itafute wafadhili kwenye sekta ya vifaa na kemikali za usindikaji.
SIDO, TIRDO na taasisi zingine zina jitahidi kutoa mafunzo lakini hakuna muendelezo au ufuatiliaji kwa wale waliopata mafunzo ikiwezakana wawezeshwe mitaji n.k. Angalia hapa jinsi taasisi kama hiyo ya Kenya inavyofanya ufuatiliaji au mrejesho (client feedback) toka kwa wateja wao Can you spare a few moments to take my survey? .
Mrejesho unahakikisha suala la sustainability ya miradi.
Tukifanikiwa kwenye ubora na uwingi wa bidhaa zinazo sindikwa ndani tutaondoa ulazima wa kuweka mashariti mengi yasiyo rafiki ya vibali vya kupeleka bidhaa za mazao ya kilimo nje ya nchi kama ilivyo sasa. Hata tukiweka mashariti ya kusafirisha bidhaa zilizosindikwa pekee bado haitaleta hathari kwa mkulima sababu tayari tutakuwa tuna wasindikaji wengi wa ndani.
KAMA yakitekelezwa mengi ya niliyo shauri hapo juu na kuboreshwa zaidi naamini changamoto ya masoko itapungua au kuisha, nina imani hapo suala la vijana kupata mitaji litakuwa rahisi kwa maana hata watu binafsi au ndugu watakopesha vijana mitaji kwa vile wanaona kilimo ni biashara ambayo inaweza kurudisha mitaji na kuleta faida.
NB: Rebecca 83 na wasomaji mtanisamehe kwa maelezo marefu lakini nilikosa maneno machache na rahisi kueleweka, labda mods au mleta uzi mnaweza kuninukuu na ku-edit mkafupisha.

- Madalali wa biashara za mazao wawe na ofisi zao wasajiriwe rasmi kama kampuni na wao wahusike kutafuta bidhaa inayotakiwa kwa jumla na wateja wakubwa wa ndani au wa nje.
- Wahusike kupokea wakulima wanaotafuta mteja wa bidhaa kwa muundo wa mikataba ya masoko ya muda mrefu, Nasisitiza lazima wafanye kazi kwa muundo wa mikataba tu.
- Kusiruhusiwe ule uhuni kama wa sokoni ambao mkulima anaokotewa viazi vibovu baada ya siku tatu anapokuja kuchukua pesa yake anaaambiwa hivi vimeoza hatujauza.
- Mkulima akisaini mkataba apewe mashariti ya ubora, akikidhi mashariti anapokabidhi mzigo wake basi hasara inayofuata baada ya hapo haimhusu mkulima.