pansophy
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 502
- 320
Mara kadha wa kadha tumesikia serikali yetu ipo kwenye vita ya uchumi (Economic War). Kwa miaka ya hivi karibuni hii vita ya uchumi imekuwa ikihusisha mataifa makubwa mawili, Marekani na China. Walau kwa wenzetu tunaweza kuona mpambano unaendaje mathalan China anashusha thamani ya pesa yake, wanashindana kupata mikataba ya kibiashara na nchi mbalimbali (Trade agreements) na njia nyingine mbalimbali.
Tukiacha haya mataifa makubwa kuna vitu bado vinanitaza kwa upande wetu;
a)Tanzania ipo kwenye vita ya Uchumi na nani?
b)Mbinu zetu za kivita ni zipi?
c)Tutashinda vipi (vigezo vitakavyotufanya tuseme tumeshinda au tunaongoza kwenye mpambano huu.
Sitegemei majibu mepesi kama uchumi wa kati na viwanda kama yanatosha kuonyesha namna tulivyojipanga kwenye hii vita.
NB: Usilete majibu ya mepesi au kejeli na kelele za wachumia matumbo. Lengo ni kujifunza na kutaka kujua ili tusonge mbele. Sio lazima wote tujibu.
Karibuni wana jamvi