Tuendako sio kuzuri!

Aug 13, 2015
94
164
Waungwana wa JF nimeona niandike haya baada ya kutafakari sana juu ya ninachokiona sijui na wenzangu kama mnaliona hili, Kwa uelewa wangu siasa si chuki, ugomvi, hila, visasi ila siasa ni hoja, mwenye hoja humshinda asiye na hoja au mwenye hoja hafifu. Ikubukwe sote ni watanzania ingawaje tunatofautiana tu itikadi za vyama.

Sasa naona kama kuna kachuki kanajengeka kati ya chama tawala na upinzani.

Imekuwa kama ni uadui, wa upinzani anaanza kumchukia wa chama tawala wa chama tawala anamchukia mpinzani.

Mimi nimeliona hili hata humu JF. Kwa mwenendo huu Nchi yetu hatutafika kabisa tunakoelekea sio kuzuri utofauti wa vyama usituletee utengano na chuki baina yetu.

Sisi ni watoto wa Baba na mama mmoja nao ni TANZANIA. tuishi kwa kupendana.
 
Waungwana wa JF nimeona niandike haya baada ya kutafakari sana juu ya ninachokiona sijui na wenzangu kama mnaliona hili, Kwa uelewa wangu siasa si chuki, ugomvi, hila, visasi ila siasa ni hoja, mwenye hoja humshinda asiye na hoja au mwenye hoja hafifu. Ikubukwe sote ni watanzania ingawaje tunatofautiana tu itikadi za vyama. Sasa naona kama kuna kachuki kanajengeka kati ya chama tawala na upinzani. Imekuwa kama ni uadui, wa upinzani anaanza kumchukia wa chama tawala wa chama tawala anamchukia mpinzani. Mimi nimeliona hili hata humu JF. Kwa mwenendo huu Nchi yetu hatutafika kabisa tunakoelekea sio kuzuri utofauti wa vyama usituletee utengano na chuki baina yetu. Sisi ni watoto wa Baba na mama mmoja nao ni TANZANIA. tuishi kwa kupendana.
Wanachokichochea watakipata tu
 
Kwangu adui wa kwanza ni mwanaccm , sijashiriki misiba yao mtaani kwangu huu ni mwaka wa 3 sasa , halafu wao pia wanafahamu kwamba sishirikiani nao kwa lolote , na namuomba Mungu aendelee kunipa ujasiri wa kuwatenga zaidi
Ni hoja vikirishi,kuna haja ya Watanzania kukaa pamoja na kuondoa tofauti zetu za kiitikadi,Nakumbuka J K aliwahi kusema ni vema tukakaa na kumaliza tofauti tukiwa wamoja
 
Chuki hiyo si njema sana. Ukiwa CCM kuna ndugu yako yuko ulinzani na Ukiwa upinzani kuna ndugu yako yuko CCM. siasa isitutenganishe, siasa za Chuki hazina tofauti na udini, ukabila au ubaguzi wa rangi. Tusifike huko.
Kwangu adui wa kwanza ni mwanaccm , sijashiriki misiba yao mtaani kwangu huu ni mwaka wa 3 sasa , halafu wao pia wanafahamu kwamba sishirikiani nao kwa lolote , na namuomba Mungu aendelee kunipa ujasiri wa kuwatenga zaidi
 
Kuna meseji juzi imetumwa na JK akiwa mgeni kwenye mkutano wa Yanga..Narudia hivi ukisha kuwa kiongozi ata kama unataka A na kuna watu wa B lazma wote uwachukulie sawa maana sote ni watanzania. Mwenzenu anasema iweje umtangaze mpinzani,iweje upeleke maendeleo kwa mpinzani,iweje nishirikiane na wapinzani. Apo hua napata mashaka na kuuliza hivi kweli huyu ni damu ya Tanzania?
 
Waungwana wa JF nimeona niandike haya baada ya kutafakari sana juu ya ninachokiona sijui na wenzangu kama mnaliona hili, Kwa uelewa wangu siasa si chuki, ugomvi, hila, visasi ila siasa ni hoja, mwenye hoja humshinda asiye na hoja au mwenye hoja hafifu. Ikubukwe sote ni watanzania ingawaje tunatofautiana tu itikadi za vyama. Sasa naona kama kuna kachuki kanajengeka kati ya chama tawala na upinzani. Imekuwa kama ni uadui, wa upinzani anaanza kumchukia wa chama tawala wa chama tawala anamchukia mpinzani. Mimi nimeliona hili hata humu JF. Kwa mwenendo huu Nchi yetu hatutafika kabisa tunakoelekea sio kuzuri utofauti wa vyama usituletee utengano na chuki baina yetu. Sisi ni watoto wa Baba na mama mmoja nao ni TANZANIA. tuishi kwa kupendana.
Haya yote yataisha tu kama tutaelewa katiba inasema nini na tukaamua kuitii
 
Chuki hiyo si njema sana. Ukiwa CCM kuna ndugu yako yuko ulinzani na Ukiwa upinzani kuna ndugu yako yuko CCM. siasa isitutenganishe, siasa za Chuki hazina tofauti na udini, ukabila au ubaguzi wa rangi. Tusifike huko.
Utawala wa awamu hii ndiyo uliopandikiza chuki. Chuki kati ya wapinzani na ccm. Angalia hata mikutano ya kisiasa,ccm wanafanya wapendavyo,wapinzani wanazuiliwa kwa kigezo eti watavunja amani. Hivi hao ccm wenyewe hawawezi kuvunja amani? Hao wapinzani wenyewe hawapendi amani? Kuna mtu anasema etcdm walipata kura elfu 6,kwahiyo ni vizuri wakizuiliwa kufanya mikutano,Kama amani inavunjika kwa kigezo cha wingi wa kura,na hao ccm waliopata nyingi zaidi je?
Vikundi binafsi vya vyama vya ulinzi wamezuia,lakini ccm wanavyo,tena vinafanya mazoezi ya karete kabisa. Je hayo ni maandalizi ya nini kama siyo ya kuvunja amani? Wasiojulikana wanateka wapinzani tu! Sijasikia au kuona mccm ametekwa au kuuwawa.
Wapinzani wakimkosoa bwana mkubwa,yanaitwa ni matusi,lakini wapinzani wakitukanwa ni sawa tu hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Nawaambia ccm,kila jambo lina mwisho wake. Msiangalie ya leo tu,angalieni na huko tuendako. Ipo siku watu watachoka.
 
Back
Top Bottom