Tuelimishane hapa kuhusu hii bahati na sibu ya BIKO

Mimi ni mshiriki wa hiyo wanayo iita bahati nasibu hakuna chochote, walitoa namba rafikiyangu Fulani kashinda, nikampigia ananiambia hata hakushiriki na hajui, kuna siku nilicheza nikakatwa pesa kwenye mpesa yangu lakini sms comfimation ya biko sijaipata, hua wanatuma namba zao za huduma kwa wateja, nikapiga wee mchana kutwa hawapatikani namba zote 3 jioni najaribu tena ndo wakapokea nawaambia nimekatwa pesa na kwenye mashindano sijashirikishwa, hakunisaidia lolote, wezi tu, tena wasaka tonge wakubwa
Mimi pia nimecheza kwa line 3 voda Tigo na Air almost nimepoteza 65000 pasipo kupata hata ya papo kwa papo hawa ni wezi tu lini mikoa ya Iringa njombe mbeya singida manyara nk wakatoa mshindi
Aseeh

Sent from my SM-G950FD using JamiiForums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ni hela zenu wenyewe mnazowapa mfano WANALIWA WATU MILIONI 5 anashinda mmoja hivyo akitoa hiyo mil 20 yeye anabakiwa na kama mil 100 kila wiki. Kila anayecheza na akiangalia walioshinda wanakabidhiwa hela anadhani na yeye atashinda kumbe chance ya kushinda ni ndogo sana. Ona Tanzania nzima anapatikana mmoja tuu, usifikiri ukiwa nyumbani kwako uko mwenyewe unaye cheza, kila mtu anadhani anacheza na yuko peke yake naatachinda,, mwisho wa siku anaishia kupata vi sms vya kukuvutia uliwe zaidi .....unaambiwa bado kidogooo.....una point nyingi...lakini kushinda mzee?????
 
izo mill. ni uongo wapuuzi hao waliishia nipa vi buku 5 mara 2 navyo vilirudi kwao maana nilivicheza kufukuzia mill. kadhaa

naishi kucheza naambiwa bado nafasi 3 uwe mshindi wa mill. nimesha acha wamebaki ntumia msg zao kunihamasisha
 
Wakuu naomba kuhoji hili kwa wajuao, karibu kila siku au few days za wiki hawa Biko wanatoa Tsh 20M na wanaitangaza kwa mbwembwe....

Napata muda wa kuangalia TV za Tz naona inatangazwa na ITV tu, je ina ukweli?

Kuna mshindi humu atudhihirishie kama buku aliyopanda ndo imemzalia 20M?

Au ndo yale yale ya kula pesa za walala hoi, then hiyo 20M ni kiini macho tu?

Wish to hear!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Bahati nasibu ni kama kamali zinginezo tu hakuna udanganyifu .
Ukweli upo ambao ni kwamba mtaliwa wengi atakula mmoja baasi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa nimekaa mahali Fulani niliona wasichana wawili wakiwa wamekaa. Muda kidogo alikuja jamaa mmoja na kukaa nao. Nikawa nasikia mmoja akimuomba jamaa amkopeshe elfu hamsini ili aongezee spate laki ili ampe jamaa mmoja anayefanya kazi biko katika kuchezesha droo ili aweze kushinda million moja. Baada ya kusikia hivyo nikakaa makini kusikiliza. Jamaa akasema hana. Yule Dada akaendelea kusema kuwa mamba ya jamaa hiyo aliipata kwa MTU Fulani ambaye naye alinufaika na mchongo huo. Lakini jamaa alisema hana hiyo hela. Baadaye akaja msichana mwingine tena na kuungana nao, ambapo pia msichana yule aliyewasilisha ombi kwa mshikaji aliwasilisha kwa msichana hiyo aliyefika. Msichana yule akaridhika na kusema kuwa waende wakachukue kadi ya ATM wakachukue mkwanja ili wakafanilishe dili. Wakaondoka na kumwacha msichana mmoja na jamaa...kilichoendelea....sijui
 
Kwa hali ya sasa mtu unatakiwa uwe makini sana na kutoa pesa.

Kutapeliwa nje nje.
 
Biko wez wanawaibia watanzania kisha wakmalza watakuja wengne na jina jipya me nawasih watanzania wakae mbali na hizi kampun za wizi
 
Mende, mi nadhani hao walitaka kukuibia.

Ungeingilia maongezi, ungeenda na maji.

Mjini vijana wanatumia akili sana kuiba.
 
Habari zenu wakuu,
Nimeskia promo mbalimbali kwenye vyombo vya habari kuhusu mchezo wa bahati nasibu maarufu kama BIKO...,ningependa kufahamu kama kuna mtu yeyote aliyeshinda ili nami nijaribu bahati yangu
Biko ni mradi km mradi mwingine,
Kinachohitajika ni mtaji wa kutosha tu....
We fikilia Biko mnacheza watu wangapi? Na anakula mmoja tu au wawili ndani ya wiki, piga hesabu watu laki 100000 wakicheza zaidi ya Mara tano (5) kwa buku 1000 au zaidi wenye mradi wataingiza bei gani? Ndani ya muda huo

iPhone 6s
 
Umeona eeh... Ukibeti unajua kabisa hapa nimepata au nimepatwa ila hizi nyingine ndio huwa hata siwaelewi.

Hahahahaaa Mimi Habari Za Bahati Nasibu Tu Zimenipita Kushoto Hata Kubeti Sielewi Nasikia Mikeka Imechanika Aaah Kuna Jamaa Kutwa Na Madaftari Utafikiri Wanafunzi Ukiuliza eti Wanabeti...
 
Back
Top Bottom