Kasheshe uko kazini ?
Unasema ati ...................................
Wapo vijana walioajiriwa benki majuzi tu baada ya kusaga lami muda mrefu kutafuta kazi, hapo wako katika sintofahamu ya kuachia "hamadi kibindoni". Na wengine nje wanasubiri hawa "wagomaji" watemwe wachangamkie tenda, "kufa kufaana". Na wale wa "mguu ndani mguu nje" wanasubiri "yakisanuka" watalia "tulilazimishwa, hatukutaka kugoma!" Watarudi kwa magoti "kumwinamia kafiri wapate mradi wao!". Hiyo "SOLIDARITY FOREVER" hapo hamna kitu, ni filimbi tu, bongo haijafikia hatua hiyo!
..Wamegoma!!!!!!Mlioko Dar na miji mingine ya Bongo,twambieni jamaa wamegoma au ndo nyimbo zilezile tulizozizoea?
Katika kuishinikiza Serikali ikubali kuwalipa mafao baada ya Serikali kuamua kuuza hisa za NMB hivyo kwa asilimia kubwa kujitoa katika umiliki wa NMB Bank,
Wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi yote nchini chini ya Chama cha wafanyakazi TUICO imetoa notisi ya masaa 48( kuanzia tarehe 20, september, 2008) kwa menejimenti ya NMB ya kugoma endapo Serikali itaendelea na msimamo wake wa kukataa kusaini makubaliano ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kulipwa mafao yao ambayo kisheria wanatakiwa walipwe.
Waraka wa Kugoma ulitolewa jana kutoka TUICO kwenda kwa menejimenti ya NMB na wafanyakazi wote.
Kithuku nakuunga mkono. Na wengi watalia baada ya mgomo. Tanzania bado hatuna machinery nzuri za mgomo na pia kwa sababu ya bribery haki haitendeki. Period. Njaa nyingi jamani.
Mwenzio hata mimi ningekuwa huko NMB nisingegoma!!!!!! kwa sasa. Nasema Tz bado solidarity haipo, ni wimbo and not practical. Na wawekezaji wengi walishasoma nyakati and that in Tanzania unaweza kumfanya empoyee namna upendavyo kwa sababu pia sheria hazimlindi mfanyakazi na si strict kwa employers. Tumeshakuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
We need to overhaul the whole system politically, economically and socially ili mambo yaanze kwa upya. Ni kwa namna gani tutafanikisha hilo?? kazi kwako na kwangu.
...mmmm, naweza kukubaliana nawe kwa namna moja lakini kuna swali. Kama tumeishakiri kuwa tumeishakuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe halafu kila mmoja anakuwa kama Maane na kuogopa kugoma ili kutetea haki yake, maana yake ni kuwa hata wajukuu zetu nao watakuja kuwa watumwa ndani ya nchi yao kwa vile tu babu na bibi zao (sisi!) kila moja alikuwa anateta kamkate kake na kawatoto wake mwenyewe, Ubinafsi kwa kwenda mbele! Ni nchi gali jamani ilijikomboa bila baadhi ya watu kujitoa mhanga????