TUCTA washindwa kuandaa mgomo hata mmoja!

Haya mkuu, we kajitoe mhanga wenzio waje watumbue pilao kwenye msiba wako, halafu maisha yao yanaendelea kama kawa, wewe wa kwako wanabakia yatima ama wanaishia kwa baba wa kambo! Ni hivi ndugu yangu, unapopanga vita yoyote, mtazame adui unayepigana naye, msome vizuri ndipo uandae vifaa na mbinu zitakazokuwezesha kushinda vita, siyo kwenda kufa vitani. Watu hupigana vita washinde, sio wafe, lile suala la kufa vitani huwa ni ajali, lakini mpiganishaji mzuri wa vita akipima akaona vita hii jeshi langu litaangamia, huwa anarudi nyuma, anajipanga vema katika mazingira ya kushinda, siyo kujitoa mhanga, uko hapo? Sasa hawa jamaa wa sijui TUICO na nani vile huko NMB hawajajiandaa hivyo, wamewapelekesha wenzao mzobemzobe, ile inaitwa kwenda "kichwakichwa", sasa subiria kitakachofuata utakumbuka maneno yangu.


Ndio huo woga ninaosema! kila mtu anajifikiria yeye na watoto wake and to hell with wajukuu wa miaka ishirini na tano ijayo!
Mkuu, hata huko vitani naamini kuna wakati majemadari wanaweza kuamua kukitoa muhanga kikosi cha askari 100 iwapo wanaamini kuwa katika kufanya hivyo wataokoa maisha ya askari wengine 1,000?
Tukumbuke pia kuwa kiapo cha askari ni kuapa kuwa tayari kuifia nchi yake na sio kupona kwa ajili ya nchi yake.
Mimi naamini kuwa mgomo utafanyika na wafanyakazi hawa ambao ni ndugu zetu watafanikiwa katika kudai haki yao. lakini pia hata kama hawatafanikiwa kwa asilimia mia moja, watakuwa wamefikisha salamu kwa hawa tunaowaita wawekezaji waanze kusoma maandishi ukutani!!
 
Haya mkuu, we kajitoe mhanga wenzio waje watumbue pilao kwenye msiba wako, halafu maisha yao yanaendelea kama kawa, wewe wa kwako wanabakia yatima ama wanaishia kwa baba wa kambo! Ni hivi ndugu yangu, unapopanga vita yoyote, mtazame adui unayepigana naye, msome vizuri ndipo uandae vifaa na mbinu zitakazokuwezesha kushinda vita, siyo kwenda kufa vitani. Watu hupigana vita washinde, sio wafe, lile suala la kufa vitani huwa ni ajali, lakini mpiganishaji mzuri wa vita akipima akaona vita hii jeshi langu litaangamia, huwa anarudi nyuma, anajipanga vema katika mazingira ya kushinda, siyo kujitoa mhanga, uko hapo? Sasa hawa jamaa wa sijui TUICO na nani vile huko NMB hawajajiandaa hivyo, wamewapelekesha wenzao mzobemzobe, ile inaitwa kwenda "kichwakichwa", sasa subiria kitakachofuata utakumbuka maneno yangu.

Acha woga wewe Kithuku. Hakuna mtu anayekwenda vitani ili afe. Ila wanaokwenda huko, wanajua kuna kufa. Mawazo ya woga kama hayo ndiyo yanawafanya viongozi wetu wa kidola kusema kwamba wanawagwaya mafisadi.

Hizo ni mbegu mbaya unazipandikiza.
 
Acha woga wewe Kithuku. Hakuna mtu anayekwenda vitani ili afe. Ila wanaokwenda huko, wanajua kuna kufa. Mawazo ya woga kama hayo ndiyo yanawafanya viongozi wetu wa kidola kusema kwamba wanawagwaya mafisadi.

Hizo ni mbegu mbaya unazipandikiza.

Kwa hiyo tujitoe mhanga tufe wabaki mafisadi wakitumbua nchi au?
 
Kwa hiyo tujitoe mhanga tufe wabaki mafisadi wakitumbua nchi au?

Duh! Sasa hii ndio nini? Mimi nilikuwa nakuaminia sana mwanzoni kama mjenga hoja mzuri; na mwenye uelewa mpana. Hiyo ilikuwa mwaka au zaidi uliopita. Ukapotea. Uliporudi ukawa si hasa yule yule Kithuku mjenga hoja mahiri.
 
Duh! Sasa hii ndio nini? Mimi nilikuwa nakuaminia sana mwanzoni kama mjenga hoja mzuri; na mwenye uelewa mpana. Hiyo ilikuwa mwaka au zaidi uliopita. Ukapotea. Uliporudi ukawa si hasa yule yule Kithuku mjenga hoja mahiri.

Ndiye yuleyule mkuu, wala usitie shaka. Kama unavyoelewa hakuna mawazo yaliyo static unless mtu ameacha kufikiri. Kama katika hili tumetofautiana yapo tutakayokuwa na misimamo inayofanana, ni fikra tu mkuu. Lakini ninachosema ni kuwa tunapopanga mikakati ya mapambano (kudai haki ni aina moja ya mapambano), lazima tuwalinde wapambanaji pia, si kuingia tu kichwakichwa. Kila mpambanaji angependa kuwa miongoni mwa watakaofaidi matunda ya mpambano huo, sasa watu wanapopanga mkakati ambao watu ati "wanajitoa mhanga" sijui wanamaanisha nani afaidi baada ya wapiganaji kuangamizwa? Hii mikakati ambayo iko destructive ndiyo ninayopinga, tena hasa inayomwangamiza mpiganaji badala ya kumwangamiza adui.
 
Nimechunguza kwa makini sana sakata hili la NMB.Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba, serikali haiwezi kukwepa lawama katika mgomo huu unaoendelea hivi sasa.Ni kweli kwamba serikali ilipashwa kuwalipa mafao yao wafanyakazi wa NMB baada ya kuuza hisa zake,hili halipingiki,hasa baada ya mazungumzo ya Dodoma, ambapo pande zote mbili,yaani serikali na wafanyakazi WA NMB kupitia viongozi wao wa TUICO, zilikubaliana kusaini mkataba ili kufanikisha hilo.Kwanini serikali baadae ilikacha kusaini mkataba huo, bado ni kitendawili.La msingi zaidi hata hivyo ni kwamba,wananchi,wakiwemo wafanyikazi bado wanauguza majeraha yasiyopona ya ugumu wa maisha yanayotokana na utendaji mbovu wa serikali ya awamu ya nne.Sasa linalonishangaza mimi ni kwamba, hivi serikali haioni kwamba inazidi kutonesha makovu hayo ambayo bado hayajapona?Wananchi tayari wanaishi katika maisha magumu,yasiyotabirika,halafu hata hicho kidogo walichojiwekea au wanachopata, serikali inajenga mazingira ya kufanya wananchi wasikipate.Jamani kama hii sio mikakati ile ya kishetani ya kuleta 'maximum chaos' ni nini.Katika hali ya kawaida,serikali ingechukua kila tahadhari kuzuia jambo kama hili lisitokee kwa vile linaumiza wananchi wengi wa kipato cha chini.Kuna maswali mengi ya kujiuliza kutokana na jambo hili ambalo kwa mtu wa kawaida hayana majibu,'one can only speculate'.Kwa nini serikali iliamua wafanyakazi walipiwe mishahara yao NMB,na tatizo hili linatokea NMB.Kwa nini tatizo hili litokee mwisho wa mwezi na kwa nini TUICO,uongozi wa NMB na serikali wameshindwa kuzuia mgomo huu usitokee.Hivi tuamini kwamba katika taasisi hizo hakuna vichwa kabisa.Haya ni maswali nyeti ambayo majibu yake ukiyatafakari yanatia uchungu sana.Nikiangalia kwa makini tukio hili na matukio mengi ya ajabu na kushangaza yanayoendelea kutokea hivi sasa nchini mwetu, nashindwa kujizuia ila kuamini kwamba yanaletwa kwa makusudi fulani mapana,yaani 'wider goal' ambayo mwananchi wa kawaida si rahisi kuelewa.Matizo haya tunayoyaona sisi 'kwao' si tatizo kwa vile 'the end justifies the means.' Kwa sasa ninaishauri serikali ifanye kila linalowezekana ili wananchi wasiendelee kuteseka.Mungu ibariki Tanzania.
 
Serikali yetu ina viongozi wanaofanya kazi kwa mazoea,waliposikia Nmb wanataka kugoma wakajua yale yale.Tutawachimbia mkwara wataufyata.Jamani alama za nyakati hizo. Nmb jitahidini,mwekezaji akishachukua kampuni,kufukuzana(hasa wenye miaka mingi) bila sababu kunaanza.Chukueni chenu kabisaaaaa.Baada ya hapo mtashangaa.
 
Hili swala la NMB lina impact kwenye Uchumi wa nchi vile vile. Maana NMB kwa siku mbili sasa hivi haipo kwenye Market ambapo Bank nyingi huwa zinafanya biashara na NMB haziwezi kufanya hivyo, ikimaanisha kwamba kutakuwa na uhaba wa pesa kwenye soko. Pia NMB wanakula hasara kubwa kwasababu kwa kutokuwa kwenye business ina maana kwamba wanakuwa wanapigwa penalty na BoT kila siku kwa kushindwa kushiriki kwenye Clearing House na mambo mengine. Kwa upande wa wateja, NMB inapoteza wateja wengi wakubwa wasipokuwa makini maana wateja hao wanashindwa kufanya biashara zao vizuri kutokana na mgomo huo (kama vile kuwalipa suppliers wao, kulipa kodi na kadhalika).

Ukiachilia mbali hayo, NMB wameshaanza kufunguliwa kesi na baadhi ya wateja wao, wakidai fidia kwa kukwamisha biashara zao nyingi na kuwaingizia hasara ambayo wanataka NMB wawalipe.

Mambo yako mengi tuu ya kuangalia, na impact ya huu mgomo ni kubwa sana kushinda watu wengi wanavyoifikiria na inaipotezea nchi mapato mengi tuu na pia inashusha uchumi wa nchi, ukiachilia mbali hasara kubwa ambayo Bank imeshapata mpaka sasa na ambayo pia inaendelea kuipata kwa jinsi mgomo unavyoendelea. Wananchi kama wafanya biashara wakubwa na wadogo, walimu, Polisi n.k. nao pia wanaumia kwa kiasi kikubwa kwa kukosa hela ya kujikimu ambayo ipo Bank.

Mimi nashauri hatua za haraka zichukuliwe na serikali, ama sivyo tunapoelekea ni kubaya sana.
 
Vilio mgomo NMB

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAFANYAKAZI wa Benki ya Makabwela (NMB) wa nchi nzima jana walianza kufanya mgomo wao uliosababisha kusitishwa kwa huduma zote za kibenki.

Hatua hiyo ya wafanyakazi wa benki hiyo kubwa kimtaji na kimtandao kuliko benki nyingine zote, ikiwa na jumla ya matawi 121 nchi nzima, ilisababisha mtikisiko mkubwa ndani ya uongozi wa taasisi hiyo.

Mgomo huo wa kwanza wa kihistoria nchini, ulisababisha matatizo makubwa miongoni mwa wateja wa benki hiyo ambao wengi wao ni wafanyakazi wa kada ya chini na ya kati katika taasisi za umma na sekta binafsi.

Aidha, hatua hiyo ya wafanyakazi hao kugoma ambayo inaweza ikawa imesababisha hasara ya mamilioni ya shilingi kwa benki hiyo, imewasababishia matatizo makubwa ya kifedha wafanyabiashara wa maeneo mbalimbali nchini.

Katika maeneo mbalimbali nchini, makundi ya wateja yalionekana kuwapo kwenye foleni kuanzia mapema asubuhi, huku baadhi yao wakiwa hawana taarifa za kuwapo kwa mgomo huo.

Wakati huo wote wateja hao walishikwa na butwaa wakati wakiwaona wafanyakazi wachache walikuwamo ndani ya matawi hayo, wakiwa wamekaa pasipo kutoa huduma, huku wengine wakisoma magazeti.

Hata mashine maalumu za kutolea pesa (ATM) kwenye matawi mengi nchini, hazikufanya kazi, wakati katika matawi mawili ya Bank House na Mtaa wa Samora ya jijini Dar es Salaam, mashine hizo zilianza kufanya kazi kuanzia saa 10:58 asubuhi.

Tangu asubuhi mashine hizo zilionekana zikiwa na maandishi yaliyosomeka: "Samahani, mashine hii haitumiki kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadaye."

Wakizungumza na Tanzania Daima, kwa nyakati tofauti, wateja waliofika katika matawi hayo walieleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na serikali kutomaliza tatizo hilo mapema.

Miongoni mwa wateja walioeleza wasiwasi wao kuhusu hali hiyo ni wafanyakazi wa serikali na taasisi za umma ambao wanachukua mishahara yao kupitia katika benki hiyo.

Mmoja wa wateja wa benki hiyo wa jijini Dar es Salaam alisema tukio hilo linapaswa kuwa fundisho kwa serikali ambayo inapaswa kuanza kugawa mishahara ya wafanyakazi kupitia katika benki nyingine mbali ya NMB.

Mteja mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Mama Rose, akiwa nje ya makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, aliiambia Tanzania Daima kuwa yeye ameathirika kwa mgomo huo, kwani alikuwa na shida muhimu iliyohitaji fedha alizotarajia kuzitoa katika tawi hilo.

Katika Tawi la Barabara ya Morogoro jijini, watu kadhaa walionekana kuchanganyikiwa, wasijue la kufanya walipoona milango ya benki hiyo ikiwa imefungwa.

Bakari Msele, mmoja wa wateja wa benki hiyo, aliitaka serikali iharakishe kutatua mgogoro huo, kabla hali haijabadilika na kuwa mbaya zaidi.

Kizaazaa cha mgomo huo, hakikuishia jijini Dar es Salaam pekee, kwani huko Arusha, wateja wengi walishinda kwenye matawi ya NMB wakisubiri huduma bila mafanikio.

Katika tawi la NMB la Clock Tower, milango ilikuwa imefungwa huku kukiwa na bango lenye maandishi yasemayo:

"Tunasikitika kuwaarifu wateja wetu kwamba tawi letu limefungwa leo, tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza, asanteni."

Kutokana na hali hiyo, wateja wengi walijikuta wakirejea majumbani mwao bila kupata huduma huku ATM zikiwa haina fedha.

Mteja John Simon, baada ya kuona hali hiyo, aliangua kilio huku akisema ana matatizo makubwa kutokana na mtoto wake kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha na alikuwa anahitaji fedha kwa ajili ya matibabu yake.

Huko Babati inaripotiwa kuwa, Jeshi la Polisi liliweka ulinzi mkali katika maeneo yanayolizunguka jengo la Benki ya NMB ili kuzuia vurugu kutoka kwa wananchi waliokuwa na hasira baada ya kushindwa kupata huduma za kibenki katika tawi hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Luther Mbuttu, alisema jeshi hilo limelazimika kuimarisha ulinzi kutokana na wananchi wengi kuwa na hasira na kuamua kulizunguka jengo la benki hiyo.

"Ni kweli polisi imethibitisha kuwepo kwa mgomo ila tumeimarisha ulinzi ili kuhakikisha hakuna vurugu yoyote itakayotokea," alisema Mbuttu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TUICO, Boniface Nkakatisi, alisema chama hicho kiko tayari kuwalipa mishahara wafanyakazi wote wa NMB kama serikali itashindwa kufanya hivyo.

Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya serikali kushindwa kukubaliana na masharti waliyowekeana na wafanyakazi kabla ya benki hiyo kuuzwa.

"Sisi tunasema kwamba, hatushindwi kuwalipa mishahara kama serikali ikishindwa kusaini mkataba wetu. Haya tulikubaliana lazima tuone haki inatendeka," alisema Nkakatisi.

Alisema wakati wote wa majadiliano, serikali iliwakilishwa na wanasheria wake ambao waliafikiana na kila kipengele kilichokuwa kwenye mkataba huo.

"Napenda kuwaambia hapa serikali imejaribu kuvuta kamba, sasa hatuachi mpaka kieleweke… lazima tuhakikishe kwamba tunapata haki zetu za msingi kama tulivyokubaliana kwenye mkataba wetu,"alisema Nkakatisi.

Alisema jambo kubwa linalozusha hofu kwa wafanyakazi ni kitendo cha kuuzwa kwa benki hiyo kwa mwekezaji mpya ambaye wanaamini kama hawatalipwa mafao yao sasa, wanaweza kuyakosa baada ya kuingia.

"Hatuwezi kukubali huyo mwekezaji aingie kabla hatujalipwa mafao yetu, tunaweza kuyakosa kwa sababu kila mwekezaji anakuja na sera zake. Hapa kuna hatari wafanyakazi wenzetu wakapoteza kazi," alisema Nkakatisi.

Alisema mgomo wa wafanyakazi katika benki hiyo umesababishwa na kundi fulani la watu ndani ya serikalini ambao wana ajenda ya siri juu ya wafanyakazi hao.

Hali hiyo ya mambo ilisababisha Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ben Christiaanse, kuitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari na kueleza namna hatua hiyo ya wafanyakazi ilivyosababisha, na itakavyosababisha madhara makubwa.

Christiaanse alisema mbali ya kuitia hasara kubwa benki hiyo ambayo hakuitaja, mgomo huo unaweza kusababisha matatizo makubwa kwa wafanyakazi wanaopokea mishahara yao kupitia NMB.

"Tumepata hasara kubwa kifedha, lakini hasara kubwa zaidi ni ya kupoteza imani kwa wateja wetu.

'‘Maelfu ya Watanzania leo wanahangaika kupata huduma zetu kwa sababu ya mgomo huo. Hiyo ni hasara kubwa zaidi," alisema.

Hata hivyo mkurugenzi huyo alisema hatua hiyo ya wafanyakazi imesababisha hali ya ulinzi na usalama katika benki hiyo kwa matawi yake yote nchini kuimarishwa.

Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa uongozi wa benki hiyo umeshtushwa na mgomo huo kwa madai kuwa, njia waliyotumia wafanyakazi hao kushinikiza madai yao ni kubwa na athari zake ni mzigo kwa NMB.

"Sijui mgomo huo utaisha lini, lakini binafsi napenda uishe hata sasa ila inategemea jinsi serikali itakavyoharakisha kumaliza malalamiko yao," alisema.

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, wafanyakazi hao hawajagoma kutokana na mishahara midogo, bali mafao yao waliyoahidiwa na serikali kwa mujibu wa mikataba yao.

Alisema kwa nyakati tofauti, kwa siku nzima ya jana alikuwa na mazungumzo na uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), pamoja na serikali kwa nyakati tofauti na kwamba wafanyakazi wameonyesha msimamo wa kutorejea kazini.

Katika hatua nyingine, uongozi wa NMB umekwenda mahakamani kutaka viongozi wa TUICO waliochochea mgomo huo, wachukuliwe hatua kwa madai ya kukiuka amri halali ya mahakama.

Uongozi huo kupitia wakili wao, Rosan Mbwambo, uliwasilisha ombi hilo katika Mahakama Kuu jana la kutaka viongozi wa TUICO wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa madai kuwa kuna ombi la mahakama lililozuia kufanyika kwa mgomo huo hadi hapo litakapotolewa uamuzi.

Mwanasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ombi hilo lipo mahakamani hapo kuanzia Januari mwaka huu na hadi sasa halijatolewa uamuzi, hivyo kitendo cha TUICO kutaka wafanyakazi wa NMB wagome ni cha kuvunja amri ya mahakama.

Aliwataja viongozi wa TUICO ambao leo wanatakiwa mahakamani kutoa utetezi wao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kuwa ni Katibu Mkuu, Boniface Nkakatisi, Naibu Katibu Mkuu, Alquine Senga, Mwenyekiti wa NMB tawi la TUICO, Kamati ya Majadiliano na Abdallah Kinenekejo.

Kwa mujibu wa amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji Mwipopo, ilisema amri hiyo inawataka wahusika wafike mahakamani na kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua.

Samansi ya amri hiyo, ilitolewa kidharura na kwa faragha bila upande wowote kuwapo mahakamani hapo na wahusika pia walipewa kidharura.

Habari hii imeandaliwa na Daniel Misheto, Kulwa Karedia, Happy Katabazi, Hamida Khalid, Richard Mwangulube na Deogratius Temba.
 
Haki ya mnyonge inapopigwa dana-dana.... Mshikamano tu, mpaka kieleweke!



.
 
Na mahakama mbona imekurupuka baada ya MGOMO?

Yaani siku hizi UBANGAIZAJI MPAKA KWENYE MAHAKAMA!!!!!. Wangewapa hawa jamaa "haki" yao mapema wala kusingetokea haya yote.

Justice delayed is Justice.................... (jaza)
 
Wanajua kila kitu ,wanapewa tahadhari muda mrefu sana...wamapuuza...wao wanajua kusafiri na kutalii si kusikiliza matakwa ya walio wengi....sijui hata kama wanajali....sijui nafikiria nini jamani ila..naona kama atokee mtu mmoja shujaa kama Okello...aseme alietoka haruhusiwi kurudi tafuta kibanda huko huko jumba jeupe upumzike...tuachie nchi yetu na uzalendo wetu...wapi uzalendo na uanamapinduzi??nchi haiendeshwi kwa mastory jamani ni strategies.......si longo longo na bora liende...tumechoka
 
Kithuku nakuunga mkono. Na wengi watalia baada ya mgomo. Tanzania bado hatuna machinery nzuri za mgomo na pia kwa sababu ya bribery haki haitendeki. Period. Njaa nyingi jamani.

Mwenzio hata mimi ningekuwa huko NMB nisingegoma!!!!!! kwa sasa. Nasema Tz bado solidarity haipo, ni wimbo and not practical. Na wawekezaji wengi walishasoma nyakati and that in Tanzania unaweza kumfanya empoyee namna upendavyo kwa sababu pia sheria hazimlindi mfanyakazi na si strict kwa employers. Tumeshakuwa watumwa ndani ya nchi yetu.

We need to overhaul the whole system politically, economically and socially ili mambo yaanze kwa upya. Ni kwa namna gani tutafanikisha hilo?? kazi kwako na kwangu.

Hapo mkuu umekosea sana, Tanzania sasa iko katka wakati wa mpito, paradigm shift, toka katika ujinga kwenda katika werevu. Ni kweli hatukuzoea isipokuwa huo ndio mwanzo na tunaendelea kukomaa, na ni kweli katika mapambano ni lazima pawe na watu wa kutolewa kafara. Hongereni NMB kwa kuonyesha njia, sasa tunangoja CWT, TAHLISO, mfanye kweli ili Tanzania ikomae kwa ajili ya ukombozi wa nchi.
 
Mahakama imezidi kuwabana wafanyakazi wa NMB, leo imetoa amri wasitishe mgomo, pia watoe matangazo kwenye magazeti kuwafahamisha wafanyakazi wao wote kuwa mgomo umesitishwa
 
Mahakama imezidi kuwabana wafanyakazi wa NMB, leo imetoa amri wasitishe mgomo, pia watoe matangazo kwenye magazeti kuwafahamisha wafanyakazi wao wote kuwa mgomo umesitishwa


Naambiwa wafanyakazi wametoa kauli kwamba hawajagoma, bali wanaunga mkono mgomo wa serikali.



.
 
Date::9/23/2008
Mahakama Kuu yaamru wafanyakazi NMB kurudi kazini mara moja
Na Kizitto Noya
Mwananchi

JAJI wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Jaji Mfawidhi Ernest Mwipopo, jana alibatilisha mgomo wa wafanyakazi wa Benki ya NMB na kuwataka warejee kazini ndani ya muda wa saa tatu, uamuzi ambao umeridhiwa na wafanyakazi.

Wafanyakazi hao kutoka karibu matawi yote zaidi ya 120 nchini kote, waliamua kugoma kwa muda usiojulikana wakiishinikiza serikali kusaini makubaliano ya malipo ya mkupuo wa fedha ambazo walistahili kulipwa wakati benki hiyo ikichukuliwa na mwekezaji mpya, kutengewa asilimia tano ya hisa na pia fedha za mfuko wa kujikopesha.

Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Mwipopo alizitaka pande mbili zinazopingana kutoa matangazo kwenye vyombo vyote vya habari kuwajulisha wafanyakazi hao kuwa wanatakiwa kurejea kazini kuanzia saa 11:25 jioni jana hadi leo 2:00 asubuhi.

Katika hukumu hiyo iliyodumu kwa muda wa saa mbili kuandaliwa na kusomwa, Jaji Mwipopo alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kuona upungufu katika hoja tatu za wafanyakazi hao walizozitoa kutetea mgomo wao.

Akichambua hoja moja baada ya nyingine, Jaji Mwipopo alisema aya ya kwanza na ya pili za notisi ya mgomo huo, zimeiingiza serikali katika mgogoro huo kwa kueleza kuwa imechangia kwa kugoma kusaini makubaliano yaliyofikiwa kati ya wafanyakazi wa NMB na uongozi wa benki hiyo.

"Aya hizo zinagongana na nafasi ya serikali kwenye madai ambayo ni msingi wa ugomvi," alisema. "Aya ya kwanza imeitaja serikali kuwa ndio iliyogoma kusaini makubaliano. Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano kuwa mgogoro huo umeelekezwa kwa NMB kwa sababu ndio taasisi pekee mnayoweza kuigomea."

Alisema hoja ya pili inayofanya mahakama isiutambue mgomo huo na kuuita haramu na batili, ni muda wa kutolewa kwa nositi ya kuanza kwake.

Alifafanua kuwa, notisi hiyo ya saa 48 iliyotolewa Ijumaa ilimaanisha kuwa mgomo huo ulitakiwa uanze saa 10:45 Jumapili, muda ambao saa hizo 48 ulikuwa unaisha. Lakini badala yake wafanyakazi walianza mgomo huo saa 2:00 asubuhi Jumatatu.

Hali kadhalika jaji huyo alifahamisha kuwa mgomo huo ulipaswa kuanza jana na sio juzi endapo notisi yake ingetolewa kwa kutumia siku za kazi badala ya saa kwani sheria ya kazi, haitambui siku za Jumamosi na Jumapili kuwa ni siku za kazi.

"Hoja ya pili ni timing (muda), kama notisi hiyo ni ya saa 48 na ilipokewa Ijumaa saa 10:45 jioni, muda wake ungeisha saa 10:45 Jumapili. Kwa nini hamkugoma siku hiyo na mkaamua kusubiri hadi Jumatatu?" alihoji Jaji Mwipopo na kuongeza:

"Lakini ikumbukwe kwamba, sura ya kwanza ya Sheria ya Kazi... haitambui Jumamosi na Jumapili kuwa ni siku za kazi, hivyo kuhesabu siku hizo kuwa siku za kazi sio sahihi."

Kwa mujibu wa Jaji Mwipopo ni jukumu la mahakama kutafsiri notisi ya saa 48 inaisha lini, kwa kuwa sheria haikutoa tafsiri kuhusu notisi ya masaa hasa endapo notisi hiyo inatolewa mwishoni mwa juma.

Alisema hoja ya tatu iliyotumika kuwaamuru wafanyakazi hao warejee kazini ni udhaifu uliopo katika notisi ya mgomo huo iliyoeleza kuwa mgomo utaendelea kwa muda usiojulikana mpaka mwajiri atakaposaini makubaliano.

Alisema maelezo hayo sio sahihi kwani hayatoi fursa kwa mwajiri kujadili suala hilo na ingekuwa vema mgomo ungeeleza muda maalumu ili kumpa fursa hiyo mwajiri.

"Kutokana na mambo hayo, mahakama imetengua mgomo huo na kuutangaza kuwa ni haramu na batili hivyo hautakiwi kufuatwa. Kwa mujibu wa kifungu 84 cha sheria za ajira, naamuru ndani ya masaa matatu, kuanzia sasa, wafanyakazi wote warejee kazini," alisema Jaji Mwipopo na kuongeza:

"Nimeangalia kwa makini na kugundua udhaifu wa mambo matatu ambayo yanafanya mgomo huo uonekane batili na haramu, hivyo ninatoa amri na maagizo kuhusu suala hilo.

"Naamuru mfanyakazi ambaye hakuweza kuripoti kazini leo (jana) awe ameripoti kazini kwake kesho (leo) saa 2:00 asubuhi na naagiza uongozi wa NMB uwapokee wafanyakazi hao wote bila masharti na usiwape adhabu kwa kushiriki mgomo huo."

Saa chache baadaye, wafanyakazi waliokuwa wamekutana kwenye Ukumbi wa Msimbazi Centre, walitaarifiwa kuhusu uamuzi huo na baadaye kukubaliana kuwa wataripoti kazini leo kama ilivyoamriwa na mahakama hiyo, anaripoti Jackson Odoyo.

Baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani na Taasisi za Benki (Tuico), Boniphace Nkakatisi kuwaeleza uamuzi huo, waliweka msimamo kuwa wasingerejea kazini na kumpa kiongozi huyo wakati mgumu wa kuwaelewesha.

"Nina waomba mrudi kazini kwa moyo mkunjufu tena kwa kujituma kama awali na kutii amri ya mahakama wakati sisi tunarudi mezani kwa majadiliano zaidi," alisema Nkakatisi.

Hata hivyo, baada ya majadiliano ya muda mrefu wafanyakazi hao waliamua kukubaliana na uamuzi huo, lakini wakawaagiza viongozi wao wa Tuico kuhakikisha suala hilo linatatuliwa haraka iwezekanavyo ndani ya wiki moja vinginevyo watagoma tena.

Hukumu ya Jaji Mwipopo ilitolewa baada ya saa mbili na nusu ya mvutano mkali wa hoja za kupinga na kutetea mgomo huo baina ya mawakili wa NMB na wafanyakazi, huku Jaji Mwipopo akilazimika kuingilia kati kwa kuwahoji maswali mawakili hao kwa nyakati tofauti.

Hoja iliyoibua hisia kali kwa pande zote mbili ni ile iliyoanzishwa na upande wa mlalamikaji (NMB) kupitia wakili wake, Rason Mbwambo kwamba mgomo huo umeandaliwa kwa hila ili kumkomesha mwajiri.

Mbwambo aliieleza Mahakama kuwa, hila imejitokeza kutokana na notisi ya kuanza kwake kutolewa Ijumaa jioni na anaamini imefanywa hivyo ili kutompa fursa mwajiri kuuzuia.

Hata hivyo, wakili wa wafanyakazi hao, Amour Khamis alisema mwenye hila ni mwajiri (NMB) kwa kutaka viongozi wa wafanyakazi hao wapelekwe gerezani kama wafungwa wa madai ya kuandaa mgomo badala ya kutaka kuwe na mazungumzo ya kufikia mwafaka.

"Mwajiri ndiye mwenye hila kwani anaweza kueleza sababu gani hapa (mahakamani) ya kuomba viongozi hao wakamatwe, wafilisiwe mali zao na kufungwa kama wafungwa wa madai badala ya kutaka mazungumzo," alihoji wakili huyo.

Kabla ya mahojiano hayo, Wakili Mbwambo aliiomba mahakama itoe amri na maelekezo mwafaka kwa wafanyakazi hao ili kukabiliana na mgomo huo ambao sasa umefikia katika hatua mbaya.

Mbwambo alitaka wafanyakazi hao warejee kazini huku utaratibu mwingine wa kimahakama ukiendelea ili kunusuru hasara itakayopatikana kutokana na mgomo huo unaofanyika nchi nzima.

Hata hivyo, hoja ya Wakili Mbwambo ilipingwa na wakili wa wafanyakazi, Khamis aliyesema: "Mheshimiwa jaji, Mbwambo hakuwa mkweli na hataki kuwa muwazi. Kutaka wafanyakazi hao warejee kazini ni kuendeleza mgogoro. Njia mwafaka ni watu kukutana na kufikia mwafaka."

Kabla ya majibizano hayo, Jaji Mwipopo alitumia muda mwingi kuwauliza maswali mawakili hao na ifuatayo ni sehemu ya mahojiano yao:

Jaji: Kwa nini, msomi Khamis, mahakama isiamini kuwa mgomvi wa Tuico ni serikali iliyokataa kusaini mabaliano yenu na sio NMB?

Wakili Khamis: Ndio maana nilisema kuna haja ya sisi kupata muda wa kuwasilisha nyaraka zetu kwa maandishi kwani makubaliano yalihusu pande tatu, wafanyakazi, NMB na serikali. Kabla ya serikali, NMB ilitakiwa iwe imesaini kwanza.

Jaji: Baada ya kutoa notisi ya saa 48 Ijumaa saa 10:45 jioni, kwa nini msingegoma Jumapili siku ambayo notisi yenu iliisha badala yake mkachagua Jumatatu?

Wakili Khamis: Sheria inataka watu wagome baada ya notisi, na kwa mujibu wa sheria hiyo hakuna ubaya watu kugoma muda wowote baada ya muda wa notisi hiyo kumalizika.

Jaji: Kwa nini masaa hayo 48 hayakuwa ya siku za kazi na hivyo kuishia Jumatatu na mgomo mkaanza leo (jana)?

Wakili Khamis: Siku za kazi sio za tarehe za mwezi, ni siku ambazo wafanyakazi wa taasisi wanatakiwa kufanya kazi na kwa NMB ni siku zote kwani ATM zinafanya kazi masaa 24, hivyo ni sahihi kuhesabu Jumamosi na Jumapili kuwa ni siku za kazi kwa NMB.

Baada ya mahojiano na wakili wa wafanyakazi, Jaji Mwipopo alimgeukia wakili wa NMB na sehemu ya mahojiano yao ni kama ifuatavyo:

Jaji: Kwa nini nyie (NMB) msionekane pia kuwa mna hila na mnashirikiana na wafanyakazi hao kuishinikiza serikali isaini makubaliano kwa kutotoa taarifa mapema kwamba Jumatatu mgomo unaanza?

Wakili Mbwambo: Tunashukuru kwamba unatukumbusha uwezekano wa kuwasiliana na ofisi yako hata siku za mwisho wa juma, lakini katika hali ya kawaida isingeweza kuwaza kwamba tungeweza kukupata siku hiyo.

Jaji: Kwa nini mnaomba viongozi hawa wakamatwe, wafilisiwe na wafungwe kama wafungwa wa madai badala ya kuomba mahakama izuie mgomo?

Wakili Mbwambo: Hili ni ombi moja tu, kumbuka pia tumeiomba mahakama ichukue hatua nyingine yoyote inayoona inafaa kunusuru hali hiyo.

Baada ya maswali na majibu hayo yaliyodumu kwa takriban saa 1:30 Jaji Mwipopo alisema: "Kuhusu maombi ya NMB kwamba viongozi wakuu wanne wasikilizwe leo na amri itolewe ya kukamatwa, kufilisiwa na kufungwa kama wafungwa wa madai, natoa amri kwamba mahakama imewapa muda ili waweze kujitetea kwa maandishi na vielelezo na kuwasilisha pingamizi la kiapo kesho, (leo) kesho kutwa wampe nakala ya hati hiyo wakili wa mwajiri na Septemba 26 tukutane hapo saa 4:00 asubuhi kuendelea na shauri hili."

Naye Boniface Meena anaripoti kuwa, menejimenti ya Benki ya NMB, imewataka wafanyakazi wote wa benki hiyo waliogoma kurejea kazini leo kama amri ya mahakama ilivyowataka.

Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ben Christiaanse alisema anategemea wafanyakazi hao watafika ofisini kwani serikali inayafanyia kazi madai yao.

Alisema si vizuri kwa wafanyakazi kugomea menejimenti ya benki kwa kuwa wafanyakazi hawaidai benki, bali serikali.

"Ninaamini kuwa, watafika ofisini kama kawaida na sidhani kama nitachukua hatua zozote za kisheria dhidi yao kutokana na mgomo uliotokea," alisema Christiaanse
 
Hapa ndipo ninapoijilaumu kwa kutotimiza ndoto yangu ya kusoma sheria kama ziada katika taaluma yangu. Ila nitajitahidi. Sheria ni fani inayofurahisha sana!
 
Niliwahi kuchangia kwamba huu mgomo ulikuwa wa Kipuuzi na hoja yangu ilikuwa kuwa kwamba Wao hawana mkataba wowote na Serikali zaidi ya kuwa wana mkataba na NMB.

Mambo ya kufikiria Kijima.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom