TUCTA washindwa kuandaa mgomo hata mmoja!


Mgoyangi

Mgoyangi

Senior Member
Joined
Feb 6, 2008
Messages
184
Likes
3
Points
35
Mgoyangi

Mgoyangi

Senior Member
Joined Feb 6, 2008
184 3 35
Je Migomo ya wafanyakazi - Tumesikia TUCTA - wametangaza kuwa na mgomo baada ya wiki mbili ikiwa hawatalipwa ile nyongeza ya mishahara waliyokopwa tangu Januari, - Walimu nao wametoa tangazo la kugoma ikiwa hawatalipwa madai yapio mbali mbali - Madaktari nao wamefyata mkia baada ya kuendesha kamgomo fulani pale Muhimbili.

Lakini Je hizi ni harakati za mpambano wa ukombozi kati ya walionacho na wasio nacho, kama ilivyojitokeza katika dola za kibebari, lakini je mgongano huu wa kitabaka unaweza siku moja kuzaa Tanzania yenye neema.

Lakini nani ana nyonya nguvu za wafanyakazi wa Tanzania hawa walio katika kundi hili la Mgomo, lakini pia migomo hii ipo kwa mslahi ya nani? Je mwananchi wa kawaida atanufaika nayo!
 
Novatus

Novatus

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2007
Messages
331
Likes
2
Points
0
Novatus

Novatus

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2007
331 2 0
Mgomo ni silaha ya mwisho ya binadamu ya kushinikiza apewe haki yake.
Mantiki hii inatakiwa izingatie maadili pia busara inatakiwa kutumika.
kabla sijatoa mifano naomba wahusika watafakari kabla ya kunielewa vibaya halafu wakanishambulia.

Mifano:-
1. Daktari anapogoma anatafuta haki yake lakini anayeumia ni mgonjwa ambaye kwa namna yoyote hausiki kumnyima haki hiyo. mgomo wa namna hii unapoteza maisha ya watu wasio na hatia. Lakini Serikali iliyokalia haki ya daktari huyu inakaa kimya kwani wanaoathirika hawawagusi hao waliokalia haki za watu

2. Mwanafunzi anapoandamana kupinga nauli ya daladala kupanda ni sawa na kugoma. lakini iangaliwe huyu mwanafunzi ametumwa na nani? Kwani fedha sio zake bali ni za mzazi. Je mwanafunzi anataka kutupa mzigo wa gharama za kusomesha kwa mwenye daladala? Ieleweke kuwa mzigo wa kusomesha mwanafunzi ni wajibu wa mzazi wala si vinginevyo.

Mapambano haya ya kitabaka hayatakwisha ikiwa UKWELI NA UWAZI havitatumika kwa pande zote mbili.
 
T

Tikerra

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Messages
1,704
Likes
11
Points
0
Age
65
T

Tikerra

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2008
1,704 11 0
Kuishi kwingi ni kuona mengi,mengi pamoja na haya ya TUCTA.Sina shaka yeyote kwamba, hawa jamaa ni wababaishaji kabisa,na kwa mawazo yangu,wana harufu ya rushwa.Labda utaniuliza rushwa wanapewa na nani?Jibu lake ni rahisi na wala sio siri,wanapewa na serikali.Utendaji wao kwa ujumla una mengi ya kujiuliza.Mara nyingi wametangaza migomo isiyotekelezeka kwa vile hawafuati sheria za kuweza kufanya migomo kabisa.Juzi tu katika hali ya kushangaza,walitangaza mgomo wa wafanyakazi nchi nzima bila kuzingatia sheria kabisa.Wenzao CWT,wakatangaza mgomo, lakini wakajitahidi kufuata sheria.Katika hali pia ya kushangaza wakasema sasa kwa vile wafanyakati wamelipwa malimbikizo yao, waendelee kuchapa kazi kwa bidii.Wamesahau madai ya msingi ya wafanyakazi ya ujira mdogo,ukiukwaji wa sheria za kazi za makusudi na mwajiri wao,mazingira mabovu ya kazi,ukosefu wa vitendea kazi nk.Dai la malimbikizo halikuwa la msingi.Jamani,hivi tuamini kwamba TUCTA hawajui sheria?Sidhani,naamini wanafanya hivyo kwa maslahi ya mabwana zao.Kwa ujumla ni kwamba, TUCTA hawaonekani kuwepo kwa ajili ya wafanyakazi ila kwa maslahi yao na serikali.Bado kwa maoni yangu hawajahalalisha uwepo wao.Wauhalalishe,vinginevyo hawana sababu ya kuwepo.
 
M

mgirima

Member
Joined
May 24, 2008
Messages
82
Likes
0
Points
0
M

mgirima

Member
Joined May 24, 2008
82 0 0
Hivi vyama vya wafanyakazi - if TUCTA, TUICO, RAAWU, TUGHE etc. vilianzishwa na serikali na havina mizizi yeyote kwa wavuja-jasho. Vipo pale kwa kuitetea serikali.

Ndio maana chama cha waalimu CWT kwa vile ni kilibuniwa na waalimu wenyewe, kina nguvu na kinasikilizwa. Kujitenga kwake ilileta bifu kubwa.
 
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
10,945
Likes
232
Points
160
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2008
10,945 232 160
Katika kuishinikiza Serikali ikubali kuwalipa mafao baada ya Serikali kuamua kuuza hisa za NMB hivyo kwa asilimia kubwa kujitoa katika umiliki wa NMB Bank,
Wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi yote nchini chini ya Chama cha wafanyakazi TUICO imetoa notisi ya masaa 48( kuanzia tarehe 20, september, 2008) kwa menejimenti ya NMB ya kugoma endapo Serikali itaendelea na msimamo wake wa kukataa kusaini makubaliano ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kulipwa mafao yao ambayo kisheria wanatakiwa walipwe.


Waraka wa Kugoma ulitolewa jana kutoka TUICO kwenda kwa menejimenti ya NMB na wafanyakazi wote.

Hata hivyo mara baada ya waraka huo kuwafikia walengwa, menejimenti ya NMB ilitoa taarifa ya vitisho kwa wafanyakazi wake wote.

Sehemu ya taarifa hiyo ilisema "kwa mfanyakazi yeyote atakaegoma hatolipwa mshahara wake kwa siku atakazokua kwenye mgomo na hata kusitishwa kwa ajira yake"

Hata hivyo vitisho hivyo viliwafikia viongozi wa TUICO na ndipo ujumbe mfupi wa simu za mkononi ufuatao ukasambazwa kwa kila mfanyakazi wa NMB,

"Puuzieni kejeli za mgt(menejimenti) ya NMB. Taratibu za kisheria kuhusu mgomo zimefuatwa na TUICO na itamjibu kisheria. kusanyikeni maeneo mtakayopangiwa. mgomo ni Jm3 saa 2 asubuhi. Mtasaini maeneo mtakayokusanyika. Atakaye baki kwenye tawi ni meneja peke yake huyo ndiye mkuu wa tawi. Mtando tumefutwa kuutumia. Muda wote pigeni simu. Upeleke ujumbe huu kwa mwenzio. MASSANA"

Massana ni mwenyekiti wa TUICO NMB.

Inasemekana Wafanyakazi wote wa NMB siku hiyo ya mgomo watakusanyika kwenye maeneo tulivu kana kwamba wanafanya sherehe fulani.

Hata hivyo baadhi ya wafanyakazi hasa wale wageni wameanza kuonyesha uwoga na kuweka wazi dhamira yao ya kutotaka kushiriki mgomo huo pengine kutokana na vitisho vilivyotolewa na menejimenti ya NMB.

Tayari wafanyakazi wa NMB matawi ya Dar es Salaam wamekubaliana kukusanyika maeneo ya Msimbazi Centre ambapo wataleta bendi ya muziki wa dansi kuwaburudisha wakati wa mgomo.

Ingawa baadhi ya wafanyakazi wa NMB wanakosa ujasiri kwa asilimia mia moja lakini bado ile kauli ya 'SOLIDALITY FOREVER' inawapa nguvu kwa kiasi fulani.
 
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,842
Likes
96
Points
145
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,842 96 145
Management ni ya wazungu wale wa Dutch ama ni waswahili ? Mbona kugoma ni haki yao na hata hao wazungu wanajua hili leo wanaweka mkwara wa kazi gani ?Ama kweli TZ unaweza kushangaa KOVA anamwaga FFU pale kuzima jaribio la kumuumiza mwekezaji.
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Likes
101
Points
145
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 101 145
Upuuzi mwingine;

Kufikiria kijamaa na kijima wakati tuko kwenye ubepari!!! Aliyewaajiri hao wafanyakazi ni NMB, whether hiyo benki shareholder mkubwa ni Serikali au shetani still mwajiri ni NMB...

Watanzania bwana... yaani jamaa wanashindwa kujua kwamba wafanyakazi kama wafanyakazi sio wanahisa wa kampuni?

Haya haya yalitokea TTCL, ati wanamwambia mwajiri wao asiuze hisa zake... au asiweke management anayotaka!!!

This is wrong... ukiwa kama mfanyakazi unaangalia entity iliyokuajiri... ambayo kwa case hii ni NMB... na NMB ipo whether serikali ina hisa 1% au ina hisa 0%.

Mungu wabariki watu waamke.
 
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,842
Likes
96
Points
145
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,842 96 145
Kasheshe uko kazini ?
Unasema ati ...................................
 
K

Kithuku

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2006
Messages
1,395
Likes
108
Points
145
K

Kithuku

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2006
1,395 108 145
Wapo vijana walioajiriwa benki majuzi tu baada ya kusaga lami muda mrefu kutafuta kazi, hapo wako katika sintofahamu ya kuachia "hamadi kibindoni". Na wengine nje wanasubiri hawa "wagomaji" watemwe wachangamkie tenda, "kufa kufaana". Na wale wa "mguu ndani mguu nje" wanasubiri "yakisanuka" watalia "tulilazimishwa, hatukutaka kugoma!" Watarudi kwa magoti "kumwinamia kafiri wapate mradi wao!". Hiyo "SOLIDARITY FOREVER" hapo hamna kitu, ni filimbi tu, bongo haijafikia hatua hiyo!
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,490
Likes
932
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,490 932 280
Mlioko Dar na miji mingine ya Bongo,twambieni jamaa wamegoma au ndo nyimbo zilezile tulizozizoea?
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,028
Likes
1,381
Points
280
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,028 1,381 280
Wapo vijana walioajiriwa benki majuzi tu baada ya kusaga lami muda mrefu kutafuta kazi, hapo wako katika sintofahamu ya kuachia "hamadi kibindoni". Na wengine nje wanasubiri hawa "wagomaji" watemwe wachangamkie tenda, "kufa kufaana". Na wale wa "mguu ndani mguu nje" wanasubiri "yakisanuka" watalia "tulilazimishwa, hatukutaka kugoma!" Watarudi kwa magoti "kumwinamia kafiri wapate mradi wao!". Hiyo "SOLIDARITY FOREVER" hapo hamna kitu, ni filimbi tu, bongo haijafikia hatua hiyo!

Kithuku nakuunga mkono. Na wengi watalia baada ya mgomo. Tanzania bado hatuna machinery nzuri za mgomo na pia kwa sababu ya bribery haki haitendeki. Period. Njaa nyingi jamani.

Mwenzio hata mimi ningekuwa huko NMB nisingegoma!!!!!! kwa sasa. Nasema Tz bado solidarity haipo, ni wimbo and not practical. Na wawekezaji wengi walishasoma nyakati and that in Tanzania unaweza kumfanya empoyee namna upendavyo kwa sababu pia sheria hazimlindi mfanyakazi na si strict kwa employers. Tumeshakuwa watumwa ndani ya nchi yetu.

We need to overhaul the whole system politically, economically and socially ili mambo yaanze kwa upya. Ni kwa namna gani tutafanikisha hilo?? kazi kwako na kwangu.
 
D

David Nkulu

Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
53
Likes
0
Points
0
D

David Nkulu

Member
Joined Jul 25, 2008
53 0 0
Nawasikitikia wafanyakazi, kwa kweli hali ni ngumu. Kugoma sio solution ktk hali iliyopo. Ikiwa shares zinauzwa ktk soko huria, na wao wanagoma, ni wazi kuwa share za NMB zitakuwa bomu. Muajiri atafanya kila jinsi kuhakikisha kuwa analinda maslahi yake na shareholders.
Tatizo ni pale ambapo tunavamia systems ambazo hatuna uwezo wala kuzielewa kwa undani na kutaka kuiga bila kufikia kiwango kinachotakika.
Tunalala kwenye banda la udongo na dari ya makuti bila umeme wala maji na tunataka tuangalie DVD kila kukicha kama vile tunaishi N.Y.!!
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,490
Likes
932
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,490 932 280
Mkuu Kipanga asante, nawapongeza kwa kufanya kweli. matokeo ya mgomo ni swala lingine.Wasaliti/waoga wapo,watakuwepo na walikuwepo. Tukumbuke shujaa hufa mara moja ila waoga hufa vifo vingi kabla ya kifo halisi.
 
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
7,011
Likes
38
Points
145
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
7,011 38 145
Mwanasheria wa NMB kaenda mahakamani na mahakama imetoa amri ya kuitwa mahakani kesho viongozi wa TUICO na NMB ambao wameitisha mgomo. Inadaiwa kuwa walilofanya ni kosa la jinai (kudharau amri ya mahakama) kwa sababu suala hilo lipo mahakamani kusubiri uamuzi na walishazuiwa kugoma mpaka uamuzi utakapotolewa
 
T

Tikerra

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Messages
1,704
Likes
11
Points
0
Age
65
T

Tikerra

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2008
1,704 11 0
Labda mafisadi hawa migomo ndiyo lugha wanayoielewa.Endeleeni NMB,kila la heri.
 
LazyDog

LazyDog

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
2,478
Likes
17
Points
135
LazyDog

LazyDog

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
2,478 17 135
Katika kuishinikiza Serikali ikubali kuwalipa mafao baada ya Serikali kuamua kuuza hisa za NMB hivyo kwa asilimia kubwa kujitoa katika umiliki wa NMB Bank,
Wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi yote nchini chini ya Chama cha wafanyakazi TUICO imetoa notisi ya masaa 48( kuanzia tarehe 20, september, 2008) kwa menejimenti ya NMB ya kugoma endapo Serikali itaendelea na msimamo wake wa kukataa kusaini makubaliano ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kulipwa mafao yao ambayo kisheria wanatakiwa walipwe.


Waraka wa Kugoma ulitolewa jana kutoka TUICO kwenda kwa menejimenti ya NMB na wafanyakazi wote.Kuna tetesi kwamba ile sheria inayotaka NOTICE ya mgomo kutolewa siku 60 kabla imerekebishwa. Kuna mwenye ufahamu kuhusu hili?.
 
BabaDesi

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Messages
2,846
Likes
89
Points
145
BabaDesi

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2007
2,846 89 145
Kithuku nakuunga mkono. Na wengi watalia baada ya mgomo. Tanzania bado hatuna machinery nzuri za mgomo na pia kwa sababu ya bribery haki haitendeki. Period. Njaa nyingi jamani.

Mwenzio hata mimi ningekuwa huko NMB nisingegoma!!!!!! kwa sasa. Nasema Tz bado solidarity haipo, ni wimbo and not practical. Na wawekezaji wengi walishasoma nyakati and that in Tanzania unaweza kumfanya empoyee namna upendavyo kwa sababu pia sheria hazimlindi mfanyakazi na si strict kwa employers. Tumeshakuwa watumwa ndani ya nchi yetu.

We need to overhaul the whole system politically, economically and socially ili mambo yaanze kwa upya. Ni kwa namna gani tutafanikisha hilo?? kazi kwako na kwangu.

...mmmm, naweza kukubaliana nawe kwa namna moja lakini kuna swali. Kama tumeishakiri kuwa tumeishakuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe halafu kila mmoja anakuwa kama Maane na kuogopa kugoma ili kutetea haki yake, maana yake ni kuwa hata wajukuu zetu nao watakuja kuwa watumwa ndani ya nchi yao kwa vile tu babu na bibi zao (sisi!) kila moja alikuwa anatetea kamkate kake na watoto wake mwenyewe, Ubinafsi kwa kwenda mbele! Ni nchi gani jamani ilijikomboa bila baadhi ya watu kujitoa mhanga????
 
K

Kithuku

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2006
Messages
1,395
Likes
108
Points
145
K

Kithuku

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2006
1,395 108 145
...mmmm, naweza kukubaliana nawe kwa namna moja lakini kuna swali. Kama tumeishakiri kuwa tumeishakuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe halafu kila mmoja anakuwa kama Maane na kuogopa kugoma ili kutetea haki yake, maana yake ni kuwa hata wajukuu zetu nao watakuja kuwa watumwa ndani ya nchi yao kwa vile tu babu na bibi zao (sisi!) kila moja alikuwa anateta kamkate kake na kawatoto wake mwenyewe, Ubinafsi kwa kwenda mbele! Ni nchi gali jamani ilijikomboa bila baadhi ya watu kujitoa mhanga????
Haya mkuu, we kajitoe mhanga wenzio waje watumbue pilao kwenye msiba wako, halafu maisha yao yanaendelea kama kawa, wewe wa kwako wanabakia yatima ama wanaishia kwa baba wa kambo! Ni hivi ndugu yangu, unapopanga vita yoyote, mtazame adui unayepigana naye, msome vizuri ndipo uandae vifaa na mbinu zitakazokuwezesha kushinda vita, siyo kwenda kufa vitani. Watu hupigana vita washinde, sio wafe, lile suala la kufa vitani huwa ni ajali, lakini mpiganishaji mzuri wa vita akipima akaona vita hii jeshi langu litaangamia, huwa anarudi nyuma, anajipanga vema katika mazingira ya kushinda, siyo kujitoa mhanga, uko hapo? Sasa hawa jamaa wa sijui TUICO na nani vile huko NMB hawajajiandaa hivyo, wamewapelekesha wenzao mzobemzobe, ile inaitwa kwenda "kichwakichwa", sasa subiria kitakachofuata utakumbuka maneno yangu.
 

Forum statistics

Threads 1,238,390
Members 475,954
Posts 29,318,999