Tuacheni udhalilishaji, imetosha sasa

Tuacheni udhalilishaji, imetosha sasa

Sihitaji kuiona hiyo clip.

Inaonekana kulikuwa na nia ya dhati kufanya udhalilishaji huo. Inawezekana kabisa kuwa hili limeratibiwa kwa ustadi mkubwa na wapinzani wa Lowasa/CHADEMA na bila shaka hata Juliana alivyolileta hapa ni kwa ustadi fulani wa hali ya juu, ili apate kuwaangusha huku mkidhani anaumia pamoja na nyie.

Cha msingi hapa ni kupuuza upuuzi huu na kusonga mbele.
 
Kiongozi unakumbuka shuka kumeshakucha ??? Siku ya kufungua mlianza na Matusi ya malofa na wapumbavu mkapigilia msumari wanaume wabebe mimba
Kujuta kwenu sasa hivi ni sawa na kumbatiza Paka aache kula panya

Usihofu, tuko vzr, ila kuna watu ndani ya chama tunataka wazoee kukosolewa, chama ni chetu, hatuwezi kusubiri UKAWA watusaidie, tutayasemea wenyewe
 
Hizi ndiyo siasa ambazo CCM inawafundisha vijana wake!?

Ndiyo maana tumeshuhudia Nape akimtukana sana Lowassa hata kabla hajatoka CCM(kumbuka mkakati wa kuvua gamba) na pia mzee warioba alipigwa (makonda ) na kudhalilishwa kila kona!

Kwa tunaofuatilia siasa za ccm toka ilipoanza kupoteza muelekeo tunajua kuwa ni mabingwa wa siasa za kiuni!

Huyu aliyeleta huu uzi hapa bado hatujasahau yeye na wenzake walivyokuwa mabingwa wa kuwadhalilisha viongozi wa CDM. ....

Rai yangu kwa vijana wa Tanzania hasa tuliopo kwy siasa na hata wale tusiojihusisha na siasa tuhepuke sana kutumiwa kama 'Condom' maana hatutakuwa na future nzuri, tujiheshimu na wale wanaotamani kututuma kazi chafu za kudhalilisha watu wataogopa!
Tukatae kutumwa na kukubali kufanya kazi za hovyo na za kudhalilisha utu wetu!
 
Juliana Shonza nakupa 'SALUTE' Kumbe una utu! Keep it up, nimekuweka kundi tofauti na watu wengine. UTU kwanza siasa chafu NO.
Yapo mambo mengi yamekuwa yakiendelea katika kipindi hiki, ambapo mengi katika mambo hayo ni ya hovyo, machafu na yasiyofaa katika jamii lakini yanahalalishwa kwa jina SIASA. Mambo yenye kushusha heshima ya mtu, kudhalilisha utu wake na kufedhehesha jamii yake siku hizi hayakemewi tena, sio na watu wenyewe ama taasisi bali hata Serikali yenyewe imekalia kimya mambo hayo na jamii wameyapa jina jipya, hauitwi tena UDHALILISHAJI bali inaitwa SIASA CHAFU.

Kwa muda mrefu, binafsi nimekuwa nikitukanwa sana hapa jamvini, tena na watu wenye heshima zao na wengine nawajua kwa sura na majina halisi lakini hata hawashtuki, nao huingia kwenye mkumbo huu wa matusi, kunidhalilisha na kunishushia heshima..wakati mwingine tunalazimika kuvumilia kwa sababu ndivyo ilivyo jamii yetu lakini hakika ni lazima tukemee tabia hizi zinazoimarika ndani ya jamii yetu...Watanzania walikuwa ni watu wenye kutolewa mfano kwa kuheshimiana, kupendana na kuishi kijamaa lakini hali ya sasa ni ya mazungumzo ya chuki, uhasama, kudhalilishana na kuvunjiana heshima.

Nimeiona VIDEO inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimdhalilisha Mama Regina, huyu ni Mwanamke mwenzangu lakini pia ni kama Mama yangu mzazi kwa umri wake na mtu mwenye heshima ya kipekee katika jamii yetu, si jambo jema hata kidogo, Mimi nalipinga jambo hili kwa namna yeyote ile itakavyotafsiriwa.

Hii sio siasa, na nawaonya Vijana wenzangu wa CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ikiwa wao ndio wanaozisambaza video hizi, wajue wanafanya makosa kisheria na ni kukosa adabu na heshima kwa wazazi wetu. Nimewataja Vijana wenzangu wa CCM kwa sababu VIDEO hiyo nimeiona kwenye simu ya mmoja wao akidai ametumiwa na kijana anayeitwa Peter Kasera (ambaye nae ni kijana wa UVCCM) hizi sio tabia za wanachama ama Vijana wa CCM, MNATUDHALILISHA. Na nimeamua kukutaja kwa jina halisi ili uone haya kokote ulipo na ujutie kitendo chako, ikiwezekana uombe radhi kwa kitendo hicho.

Lakini pia hawa wapiga picha wanaokuwepo kwenye shughuli za CHADEMA na UKAWA hivi mnaishi nao vipi..? maana event ile ni ya "wanamabadiliko" imekuwaje VIDEO ile imevuja..? It's obviously kuwa mpigaji picha deliberately ameamua kuitoa kwa maslahi yake na ya wale anaowajua yeye.

Maoni yangu:
Watu hawa wote wachukuliwe hatua, kuanzia yule aliyefanya kitendo kile, aliyevujisha VIDEO pamoja na hawa wanaoendelea kusambaza..kwani ni hatua ya juu kabisa ya UDHALILISHAJI aliyofanyiwa Mama Regina.

NB:
Sitoiweka VIDEO hiyo hapa, na siitaji mtu yeyote katika uzi huu ama mwingine aweke VIDEO hiyo ama yenye mfano wa hiyo, hata kama ni SIASA jamani kuna maisha baadae..TUACHE UDHALILISHAJI, imetosha sasa.
 
Vipi na matusi na dhihaka za Abdallah Bulembo na Mwigullu Nchemba?! Nape na Musukuma je vipi na wao?! Wewe Juliana ulikuwa kinara wa matusi dhidi ya Slaa ila kama kweli unaanza kuingia kwenye u-motherhood na kutambua ushenzi wenu ni wa hovyo na kipumbavu basi nakusamehe!!

Hakuna Mkutano wa CCM uwe wa mbunge au ******** unafanyika bila matusi,tena CCM mmefikia hatua ya kuandaa matusi na kuwalipa watu waje wayanene huku mkiwalipa na kulipia TV ionyeshe mattusi!!

Wewe kenge kweli.
 
Usihofu, tuko vzr, ila kuna watu ndani ya chama tunataka wazoee kukosolewa, chama ni chetu, hatuwezi kusubiri UKAWA watusaidie, tutayasemea wenyewe

Sina tatizo na dhamira yako ya kuwakosoa viongozi Wa chama ,tatizo wenye chama wenyewe kina Mkapa ndio wanaotoa Matusi na chama sio Mali ya wanachama Tena ni Mali ya watu wachache unategemea watakuelewa Mkuu
 
Udhalilishaji umeuasisi wewe ulipotua rasmi CCM! Umesahau? Tumeshavumilia tumechoka sasa tutapambana!

Natoa onyo kali kwa FaizaFoxy na wahuni wenzake waache kuchezea utu na dini za watu! Tunawaangalia kwa umakini mkubwa sana na hilo walielewe! Hatutothubutu kuwaacha waendelee kudhalilisha utu wa mtu eti kwa sababu ya imani tofauti na itikadi tofauti! Tusije kulaumiana!!

Nnaona una kiherehere kijana.

Mwenye imani anaabudu sanamu la mzungu lililovishwa nepi? Fikiri.
 
Sihitaji kuiona hiyo clip.

Inaonekana kulikuwa na nia ya dhati kufanya udhalilishaji huo. Inawezekana kabisa kuwa hili limeratibiwa kwa ustadi mkubwa na wapinzani wa Lowasa/CHADEMA na bila shaka hata Juliana alivyolileta hapa ni kwa ustadi fulani wa hali ya juu, ili apate kuwaangusha huku mkidhani anaumia pamoja na nyie.

Cha msingi hapa ni kupuuza upuuzi huu na kusonga mbele.

Exactly

Juliana ni mnafiki tu kama mafisadi wenzake
 
Inaonyesha Mama yetu akinyosolewa tena Jamaa Anamnyoso kwa Mapozi. Kimtindo mtindo nahisi wanajuana coz kwa tendo alilolitenda yule jamaa na heshima ya yule mama either angepewa kipigo cha mwizi au polisi. Ila naona mama akaamua kumgusa na mic. Kama kweli kaamua kusamehe basi huyu mama ana roho ya huruma sana.

Nimeshtuka nimetaka mabadiliko. MAGUFULI 4 change. Kura kwa Magufuli Rais Mtarajiwa

Kawadanganye mabwana zako hapa ni Lowasa tu hata iweje,na ID zenu za kila siku
LOWASA atosha
 
Juliana umekuja na mbinu ya kitoto sana kwa sisi watu Wa kupima na Pima maji,wenye vichwa visivyojua kuchanganua na kuchanganya umewapata mama,
Lakini sisi tunaokujua wewe uliyekuwa unashinda na Mwigulu kwenye majukwaa umenoa,katu hatutakuja kuthubutu kukuamini na style yako ya kung'ata na kupuliza
LOWASA ndio mtu tunayemtaka kuwa Rais wetu baaaaasi
 
Mimi huwa kuna vitu napatashida sana kuelewa.. ukiangalia ile video utaona yule kijana kazungusha mkono kwa nyuma wakati wote mama regina anaongea, sasa najiuliza kwanini hakumzuia tangu mwanzoni? alafu kwanini watu wa ukawa wavujishe hii video? nini lengo laa haya yote? ina maana hawamtaki lowasa katika chama hicho, ina maana wamemchoka mwanamama huyo katika chama? mimi sijui ila onyo langu la kwanza ni kwa hao vijana waliovujisha hiyo video... hili halikuwa wazo zuri hata kidogo jwa sababu sisi tuna wazazi na hakuna ambae angependa kuona mzazi wake anafanyiwa hivyo.;Ni hayo tu kwa leo

Inawezekana Mama Regina alikuwa anafurahia huo mchezo, teh teh teh siasa hizi!
 
Tukumbuke tu kuna maisha baada ya uchaguzi. Hizi chuki ni za muda tu, kila mtu anatumia kila aina ya mbinu ili aonekane ametoa mchango wake hasa katika nchi zetu ambazo ukiwa kiongozi unaona umeula. Haya yanaweza kubadilika siku tukibaini kuwa kuwa kiongozi siyo ulaji bali ni mjukumu mazito
 
Back
Top Bottom