Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa!

No sio demotion, kwa sababu anampa wizara katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri atakalo lifanya hivi karibuni.

Paskali

Paskali embu litazame hili kwa pande zote mbili kwanza; First Lady's exposure aliyopata kwenye miaka 10 Ikulu leo hii unakuwa waziri badala kuwa na miradi mikubwa ya kusaidia jamii na kusimama kwenye World Stages kupaza na kutetea maslahi ya walio chini kweli leo anaenda kuombewa muongozo na Msukuma au Sugu Bungeni.

Uwaziri ni cheo cha chini sana kwa Mama Salma Kikwete achilia mbali ubunge.

Jenga picha hivi ingekuwa Mama Anna Mkapa angekubali kweli udharirishaji huu.

Bado haijaniingia akilini na wala fikra haziruhusu hilo. Huyu mama ana nafasi kubwa sana kwenye jamii na mengi bado anaweza kufanya.
 
Yasipofanyika
SubirI lisipofanyika ndipo uulize, a quick motive behind uteuzi huu wa ndivyo unavyoelekeza general common sense. Lisipofanyika ndipo tutaformulate what is the motive behind, yaani 1st Lady ameteuliwa tuu kuwa mbunge wa kawaida tuu ili iweje ? .

Paskali
 
SubirI lisipofanyika ndipo uulize, a quick motive behind uteuzi huu wa ndivyo unavyoelekeza general common sense. Lisipofanyika ndipo tutaformulate what is the motive behind, yaani 1st Lady ameteuliwa tuu kuwa mbunge wa kawaida tuu ili iweje ? .

Paskali

Hatimaye mabadiliko tayari, no Salma in the list.
 
Wanabodi,
Nimeona mijadala mbalimbali kumlaumu rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuteua wabunge wanaume 6 na Wanawake 2, kati nafasi zake 10 za uteuzi.

Sasa kwa vile wanawake hao wenye sifa na vigezo hivyo vya kuteuliwa hawako wa kutosha, then rais hawezi kujiteulia tuu wanawake just kwa vile ni wanawake hata wasio na sifa na vigezo, ili tuu kutimiza usawa wa kijinsia, eti kwa sababu tuu katiba imeshauri, no way!, hata ikibidi kuweka pembeni katiba, then Magufuli, weka pembeni katiba, endelea kupiga kazi!.

Naendelea kumshauri rais wetu mpendwa, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, aendelee tuu kuchapa kazi na kuteua watu wenye sifa na vigezo kwa nafasi mbili zilizobaki, kama hakuna wanawake wenye sifa, teua tuu wanaume, kwa sababu sote tunaishuhudia performance ya hao wanawake wawili aliosha wateua, kwa maoni yangu wanatosha, maana kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa, kuliko kufanya makosa tena, teua tuu wanaume hata nafasi zote za uteuzi, kwa sababu Tanzania wanawake wenye sifa na vigezo bado hawatoshi, ila wakitosha, wateue!.

Wanabodi na haswa wanawake, naombeni sana msinielewe vibaya, kwa sababu wanawake ni mama zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, shangazi zetu, shemeji zetu, watoto wetu, samahanini sana kwa kuwaambia kuwa hamna sifa na vigezo vya kuteuliwa kwa sababu huu ndio ukweli wenyewe japo ni ukweli mchungu, kwa sababu kama mgekuwa na sifa na vigezo, mngeteuliwa!.

Uthibitisho kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi stahiki za uongozi sio kwenye ubunge tuu hata teuzi nyingine.

Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, kati ya wakuu wa mikoa 26 wanne tu ndio wanawake, kati ya wakuu wa wilaya 134 wanawake ni 25 tu na kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wilaya 185 wanawake ni 33 tu!.

Awamu ya JK kiukweli aliwabeba sana, ila kiukweli tumeona utendaji wenu kwenye nafasi za juu za mamlaka, hivyo msinikasirikie mimi, huo ndio ukweli wenyewe maana hao wenzenu waliobebwa na kupewa mamlaka kwa kubebwa bebwa tuu, tumeona matokeo yake!, Magufuli sio mtu wa kubeba beba kama JK, kwa Magufuli ni sifa na vigezo tuu, kama huna sifa na vigezo, hauteuliwi, mambo ya kubebana bebana ilikuwa ni enzi za JK, sasa ni nyakati tofauti, hapa sasa hakuna kubebwa ni kazi tuu!. Poleni!.

Declaration of interest:
Mimi natoka Kanda fulani, wengi wetu tunakabiliwa na tatizo la kisosholojia na kisaikolojia liitwalo "male chauvinism" ambapo we don't believe in "strength of a woman",or in "girls powers".

Kwetu sisi "a woman's place is at the kitchen", ila pamoja na kuwaona wanawake stahili zao ni jikoni tuu, watu wa kabila langu ndio tunaoongoza kuthamini wanawake kwa kupenda nchini Tanzania, na tunapenda wanawake wengi hadi kujikuta tunaona sifa!, tena tunaongoza kwa kuhonga, kuanzia kuhonga pesa nyingi, gari hadi nyumba na wengine wetu tumehonga hadi ghorofa!, (mfano nyumba, ninayoishi, nimehonga kale cheupe), hivyo naishi kama mpangaji tuu, lakini linapokuja suala la kuwaamini wanawake kwenye mambo makubwa!, no way!, nafasi yao ni jikoni tuu!

Hivyo ukiniambia nitafute wanawake 5 wa kuwateua ubunge, nikajitahidi nikapata angalau wawili, ushukuru sana na kunipongeza badala ya kunilaumu, maana hapo ndio ujue kuwa nimejitahidi sana kuwateua hao niliowateua, vinginevyo...


Wasalaam

Paskali

=====
Wana JF, jifunzeni kufanya rejea:

> Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?!

> Siku ya Wanawake Duniani: Tuwakumbuke Top Ten Wanawake Wakurugenzi Wakuu Wa Taasisi Kubwa
Vipi waislam nao hawana watu wenye vigezo
 
Ingawa huyu bwana paskali kuna wasaa haeleweki msimamo wake dhahiri lakini ukilisoma vema andiko lake utabaini utumizi mkubwa wa mbinu ya kisanaa ya kejeli.

Nasema hivyo kwani ukifikiria kwa umakini utagundua wapo wanawake wengi mno wenye sifa kemkem kuwazidi hata madume!Wapo kina Tibaijuka, Dr. Malecela,.....nk.

Hivyo Paskali anajaribu kufikisha ujumbe kwa njia ya kejeli. Ni sawa na akuambiae ww una ngozi nzuri, teketeke, nyeupe na isiyo na makovu wakati unajijua ww u mweusi, ngozi ngumu na yenye magamba! Yaleyale ya kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa

Ila hajapenda kuandika hivyo...hana jinsi anahofia kuitwa mchochezi!nani asiyeogopa kibano cha wale jamaa wa miwani myeusi....wakiziponda korodani zako utatia adabu.

Hata kiba Shaaban Robert kwa kuhofia kunaswa na makucha ya watawala waliamua kuandika kazi ambazo zilikuwa ba mabdhari+wahusika wa kufikirika!...

Rejea Riwaya ya Kusadikika.


wengi huwa hawamuelewi kbs Pascal Mayalla !huu ndo uandishi wake anaandika kikebehi na kwakupaka mgongo mafuta !ni njia nzuri sana kwa era hizi !
 
Wakuu,

Ni miaka 22 sasa toka ufanyike mkutano wa Being china. Na moja ya madhumuni ilikuwa kupungua vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya wanawake katika sekta mbali mbali ikiwemo uongozi.

Pamoja na jitihada zoote zinazofanywa na serikali na taasisi mbali mbali, kuinua wanawake katika sekta mbali mbali. Mfumo dume umendelea kukwamisha juhudi hizi.

Kitendo cha kuwaita wateule wa rais... Angella, Ummy na Juliana "Side Chick", "Washusha sketi", "Wahonga miili", "Wanajipendekeza" etc Na mbaya zaidi wanao sema hivi wengine ni wanawake wenzao.

Kiukweli ni aibu,... Hata kama ni tofauti za kichama. Wale ni dada , Mama au shangazi zetu pia. Tueshimiane.
 
Chadema wanahasira sana na Shonza, maana jiwe walilolikataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu.

Kuna vijana aliwaacha Bavicha mpaka leo wanachoma mahindi mbaya zaidi wanazidi kupotea kisiasa.

Kazi yao kumsifia na kumtetea Mbowe JF...hata akosee hawataki kumwambia ukweli.
 
Wanabodi,

Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu katika taasisi mbalimbali kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na mfumo dume, hivyo kushikwa na wanaume!.

Swali ni jee, nafasi hizo zimeshikwa na wanaume kwa sababu hatuna wanawake wenye sifa, au zimeenelea kushikwa na wanaume kwa sababu ya mfumo dume tuu, nikimaanisha wanawake wenye sifa wapo, lakini hawajateuliwa kushika nafasi hizo.

Sasa hapa naomba tuwataje the Top Ten "Boss Ladies" wa ukweli, ambao ni wanawake kwenye nafasi za Wakurugenzi Wakuu wa Tasisi za Umma ambao teuzi zao zimefanywa na Rais.

  1. Jacline Mnenei Maleko-Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade
  2. Irene Isaka-Mkurugenzi Mkuu wa SSRA
  3. Dr Marina Njelekela-Mkurugenzi Mkuu, Muhimbili
  4. Dr. Mwele Malechela-Mkurugenzi Mkuu wa Nimri
  5. Dr Akwilina Kayumba - CEO wa OSHA.
  6. Dr. Agnes Kijazi- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA)
  7. Dr. Albina Chuwa-Mkurugenzi Mkuu-Takwimu.
  8. Eng.Marcelin Magessa- CEO- TEMESA
  9. Juliet Kairuki-Mkurugenzi Mkuu-TIC
  10. Magret Chacha, Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake, TWB.
    endelea kuwataja wanawake ambao ni wakurugenzi wakuu wa taasisi kubwa kubwa!.

Hongera sana kwa wanawake hawa!.
Leo ni Siku ya Wanawake Dunia, tuangazie kidogo uteuzi wa wanawake kwenye the driver's seat za public corporations kwa Awamu hii ya 5.

Rais Magufuli alipoingia madarakani, aliwakuta hao ma CEOs zaidi ya 10 ambao ni Wanawake na Waliteuliwa na Kikwete, leo miaka 3 baadae, kati ya 10 hawa, wamebakia wawili tuu!,
Dr. Agnes Kijazi- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) na
Dr. Albina Chuwa-Mkurugenzi Mkuu-Takwimu.

Jee mpaka sasa katika nafasi za Wakurungenzi Wakuu wa Mashirika ya Umma, wameteuliwa wanawake wangapi?.

Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka, naona kama graph imeshuka, swali ni jee inawezekana JK aliwateua wanawake wengi zaidi as deserving kwa sifa na vingezo, lakini sasa wanawake hao wenye sifa na vingezo vya kuteuliwa kwenye executive positions wamepungua ndio maana hakuna wakuteuliwa, au tangu enzi za JK, Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa na vingezo, bali JK alifanya kuwabeba tuu kwa kuwateua wengi ili tuu kuibeba agenda ya usawa wa kijinsia, gender equality?.

Hivyo inawezekana kabisa hoja yangu hii inaukweli?.Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! - JamiiForums

Hongereni Wanawake Wote, Leo ni Siku yenu.

Paskali.
 
Wanabodi,
Nimeona mijadala mbalimbali kumlaumu rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuteua wabunge wanaume 6 na Wanawake 2, kati nafasi zake 10 za uteuzi.

Sasa kwa vile wanawake hao wenye sifa na vigezo hivyo vya kuteuliwa hawako wa kutosha, then rais hawezi kujiteulia tuu wanawake just kwa vile ni wanawake hata wasio na sifa na vigezo, ili tuu kutimiza takwa la usawa wa kijinsia kwenye katiba, eti kwa sababu tuu katiba imeshauri, no way!, kwani Katiba ni nini?, hata ikibidi kuweka pembeni katiba, then Magufuli, weka tuu pembeni katiba, kama ulivyofanya kwenye mikutano ya kisiasa, endelea kupiga kazi!.

Naendelea kumshauri rais wetu mpendwa, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, angalia nchi inataka nini, fanya kile kitu nchi inataka na aendelee tuu kuchapa kazi na kuteua watu wenye sifa na vigezo kwa nafasi mbili zilizobaki, kama hakuna wanawake wenye sifa na vigezo, teua tuu wanaume, kwa sababu sote tunaishuhudia performance ya hao wanawake wawili aliosha wateua, kwa maoni yangu wanatosha sana, maana kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa, kuliko kufanya makosa tena, teua tuu wanaume hata nafasi zote za uteuzi, kwa sababu Tanzania wanawake wenye sifa na vigezo bado hawatoshi, ila wakitosha, wateue!.

Wanabodi na haswa wanawake, naombeni sana msinielewe vibaya, kwa sababu wanawake ni mama zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, shangazi zetu, shemeji zetu, watoto wetu, samahanini sana kwa kuwaambia kuwa hamna sifa na vigezo vya kutosha kuteuliwa ili kufikia lengo la 50/50 kwa sababu huu ndio ukweli wenyewe japo ni ukweli mchungu, kwa sababu kama mgekuwa na sifa na vigezo, mngeteuliwa!.

Uthibitisho kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi stahiki za uongozi sio kwenye ubunge tuu hata teuzi nyingine.

Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, kati ya wakuu wa mikoa 26 wanne tu ndio wanawake, kati ya wakuu wa wilaya 134 wanawake ni 25 tu na kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wilaya 185 wanawake ni 33 tu!.

Awamu ya JK kiukweli aliwabeba sana wanawake, ila kiukweli tumeona utendaji wenu kwenye nafasi za juu za mamlaka, hivyo msinikasirikie mimi, huo ndio ukweli wenyewe maana hao wenzenu waliobebwa na kupewa mamlaka kwa kubebwa bebwa tuu, tumeona matokeo yake kwenye performance zao na delivery zao.

Kikwete alikuwa ni mtu wa kubeba beba hadi mizigo, lakini bahati mbaya sana, Magufuli sio mtu wa kubeba beba kama JK, kwa Magufuli ni sifa tuu na vigezo, kama huna sifa na vigezo, hauteuliwi, mambo ya kubebana bebana ilikuwa ni enzi za JK, sasa ni nyakati tofauti, hapa sasa hakuna kubebwa ni kazi tuu!. Poleni!.

Declaration of interest:
Mimi natoka Kanda fulani, wengi wetu tunakabiliwa na tatizo la kisaikolojia liitwalo "male chauvinism" ambapo we don't believe in "strength of a woman",or in "girls powers".

Kwetu sisi "a woman's place is at the kitchen", ila pamoja na kuwaona wanawake stahili zao ni jikoni tuu, watu wa kabila langu ndio tunaoongoza kuthamini wanawake kwa kuwapenda watuhudumie kuliko makabila mengine yote nchini Tanzania, na tunapenda wanawake wengi hadi kujikuta tunaona sifa kuwa na wanawake wengi na watoto wengi!, tena tunaongoza kwa kuhonga, kuanzia kuhonga pesa nyingi, gari hadi nyumba na wengine wetu tumehonga hadi ghorofa!, (mfano mimi nyumba ninayoishi, nimeisha honga siku nyingi kwa kale cheupe), hivyo naishi kama mpangaji tuu, lakini linapokuja suala la kuwaamini wanawake kwenye mambo makubwa!, no way!, nafasi yao ni jikoni tuu!

Hivyo ukiniambia nitafute wanawake 5 wa kuwateua ubunge, nikajitahidi nikapata angalau wawili, ushukuru Mungu sana kwa hao wawili na kunipongeza badala ya kunilaumu, maana hapo ndio ujue kuwa nimejitahidi sana kutafuta ndio wakapatikana angalau hao wawili, nikawateua, vinginevyo...

Wasalaam

Paskali

=====
Wana JF, jifunzeni kufanya rejea:

> Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?!

> Siku ya Wanawake Duniani: Tuwakumbuke Top Ten Wanawake Wakurugenzi Wakuu Wa Taasisi Kubwa
Asante Paskali, Kweli cheupe dawa kwa huko kwenu.Asante kwa kuwa mkweli, hili andiko lake nimelipenda sana
 
Back
Top Bottom