Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,668
119,281
Wanabodi,
Nimeona mijadala mbalimbali kumlaumu rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuteua wabunge wanaume 6 na Wanawake 2, kati nafasi zake 10 za uteuzi.
Naomba kukiri nimehamasika kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana JF huyu
Mkuu Learned brother Petro Mselewa.

Kwanza with due respect, imeitendea haki LL.M yako, but ume err kwenye tafsiri, na ndio maana kunapotokea mkanganyiko wa tafsiri sahihi wa kifungu chochote cha katiba na sheria, mamlaka pekee yenye uwezo wa kutafsiri katiba na kutamka kuwa rais amevunja katiba ni mahakama pekee!

Na endapo shauri la kutaka tafsiri ya kifungu chochote cha katiba na sheria, hatua ya kwanza ya mahakama kwenye kudelibarate hilo shauri ni kwa kujiuliza jee mtunga katiba, sheria, alidhamiria nini?. (the motive behind and not the application).

Hivyo naomba kuchangia as if mimi ndiye mtunga Katiba.

Neno "angalau", yaani "at least", mtunga katiba alidhamiria wapatikane angalau wanawake watato, lakini wakikosekana pia its ok!, at least five plus or minus!. Kama mtunga katiba alidhamiria lazima wawe watano na kuendelea, angesema expressly, neno angalau lisingekuwepo, kwa sababu neno hilo ni kiashiria cha probability na sio definitive, hivyo kama wangetaka kumaanisha lazima wawe wabunge watano, katika isingetumia at least, ingetumia "shall" na "will", ambayo ni diminutives and not "at least " ambayo ni probability.

Hivyo kufuatia kukosekana wanawake 5 wenye sifa za kuteuliwa wabunge, mpaka sasa angalau wamepatikana wawili tuu, lakini wanaume wenye sifa ni 6, hata ikitokea akakosa wanawake wenye sifa kwenye hizo nafasi mbili zilizobakia, bado anaweza kuteua wabunge wanaume wengine wawili na ikawa 8/2 na bado akawa hajavunja katiba, kwa sababu kwenye katiba kuna sheria, taratibu na kanuni, atakuwa amevunja tuu taratibu na sio kuvunja katiba.

Japo ni kweli katiba ilimtaka ateue angalau wanawake watano, lakini kwa kuteua wanaume 6, then kwa nafasi zilizobaki wanawake hawawezi kufika watano. Ili Katiba ifuatwe, lazima mambo mawili haya yafanyike, 1. Lazima amtumbue mmoja kati ya wabunge Wanaume 6 aliowatea, 2. Nafasi 3 zilipoanza zobaki, lazima ateue wabunge wanawake, hata akikosa wenye sifa na vingezo, then afanye kuokoteza tuu ili kukidhi takwa la kikatiba la gender balance.

Naamini kilicho pelekea rais wetu kuteua wabunge wanaume wengi kinyume cha katiba ni kufuatia TZ Hatuna Wanawake Wengi Wa Kutosha, Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa Wabunge!, ndio maana wameteuliwa wanaume wengi zaidi ya Katiba inavyoelekeza, hivyo natoa wito Tuacheni kabisa Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume wengi kuliko wanawake, licha ya idadi ya wanawake kuwa ni wengi kuliko wanaume, Wenye sifa na vingezo ni wa kuhesabika, kwenye ubunge wa kuteuliwa ndio angalau wamepatikana hao wawili!.

Kwa hili, tusimlaumu bure Mhe. Rais na kumsingizia amevunja katiba, Mhe. Rais hajavunja katiba popote, neno angalau kwa lugha ya Kiingereza ni "at least", ikimaanisha wakiwepo wanawake wenye sifa hizo za kuteuliwa na rais, then wateuliwe angalau watano, lakini kwa bahati mbaya sana, imetokea Tanzania hatuna hao wanawake watano wenye sifa wa kutosha, ndio maana wameteuliwa wanaume wengi lakini wangekuwepo wanawake wenye sifa na vigezo, wangeteuliwa! .

Japo it's a fact kuwa, in Tanzania, idadi ya population ya wanawake ni wengi kuliko wanaume kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi, lakini licha ya uwingi wao, wanawake wenye sifa na vigezo zinazohitajika ili kuteuliwa ni wachache, ndio maana kuna wanawake wawili tuu ndio wameisha teuliwa wabunge, hivyo tusilalamikie kutoteuliwa kwa wanawake wa kutosha kwenye kila sehemu ili kukidhi tuu haja ya usawa wa kijinsia, kama hakuna wanawake wa kutosha, mtu unafanyaje?!, si unateua wanaume?, na sio katika ubunge tuu, hata katika teuzi mbalimbali za uongozi wa kuteuliwa, wanawake ni wacheche kuliko wanaume kwa sababu hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa na vigezo vya kuteuliwa, kama wangekuwepo, wanawake wa kutosha wenye sifa na vigezo, basi wangeteuliwa!.

Naomba kukiri kuwa kwa kufuata tuu vigezo vya CV, Tanzania tuna wanawake wengi tuu wenye sifa na vigezo, ambao ni wasomi wazuri, wana CV nzuri tuu za kushiba, lakini sifa na vigezo vya kuteuliwa sio hizo CV tuu, ni sifa na vigezo maalum ambazo hawana, hivyo hatuna wanawake wa kutosha wenye hizo sifa na vigezo, vinavyotakiwa ili wateuliwe wabunge, ndio maana wanateuliwa wanaume!, wanawake wangekuwepo wa kutosha wangeteuliwa!.
Sasa kwa vile wanawake hao wenye sifa na vigezo hivyo vya kuteuliwa hawako wa kutosha, then rais hawezi kujiteulia tuu wanawake just kwa vile ni wanawake hata wasio na sifa na vigezo, ili tuu kutimiza takwa la usawa wa kijinsia kwenye katiba, eti kwa sababu tuu katiba imeshauri, no way!, kwani Katiba ni nini?, hata ikibidi kuweka pembeni katiba, then Magufuli, weka tuu pembeni katiba, kama ulivyofanya kwenye mikutano ya kisiasa, endelea kupiga kazi!.

Naendelea kumshauri rais wetu mpendwa, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, angalia nchi inataka nini, fanya kile kitu nchi inataka na aendelee tuu kuchapa kazi na kuteua watu wenye sifa na vigezo kwa nafasi mbili zilizobaki, kama hakuna wanawake wenye sifa na vigezo, teua tuu wanaume, kwa sababu sote tunaishuhudia performance ya hao wanawake wawili aliosha wateua, kwa maoni yangu wanatosha sana, maana kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa, kuliko kufanya makosa tena, teua tuu wanaume hata nafasi zote za uteuzi, kwa sababu Tanzania wanawake wenye sifa na vigezo bado hawatoshi, ila wakitosha, wateue!.

Wanabodi na haswa wanawake, naombeni sana msinielewe vibaya, kwa sababu wanawake ni mama zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, shangazi zetu, shemeji zetu, watoto wetu, samahanini sana kwa kuwaambia kuwa hamna sifa na vigezo vya kutosha kuteuliwa ili kufikia lengo la 50/50 kwa sababu huu ndio ukweli wenyewe japo ni ukweli mchungu, kwa sababu kama mgekuwa na sifa na vigezo, mngeteuliwa!.

Uthibitisho kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi stahiki za uongozi sio kwenye ubunge tuu hata teuzi nyingine.

Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, kati ya wakuu wa mikoa 26 wanne tu ndio wanawake, kati ya wakuu wa wilaya 134 wanawake ni 25 tu na kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wilaya 185 wanawake ni 33 tu!.

Awamu ya JK kiukweli aliwabeba sana wanawake, ila kiukweli tumeona utendaji wenu kwenye nafasi za juu za mamlaka, hivyo msinikasirikie mimi, huo ndio ukweli wenyewe maana hao wenzenu waliobebwa na kupewa mamlaka kwa kubebwa bebwa tuu, tumeona matokeo yake kwenye performance zao na delivery zao.

Kikwete alikuwa ni mtu wa kubeba beba hadi mizigo, lakini bahati mbaya sana, Magufuli sio mtu wa kubeba beba kama JK, kwa Magufuli ni sifa tuu na vigezo, kama huna sifa na vigezo, hauteuliwi, mambo ya kubebana bebana ilikuwa ni enzi za JK, sasa ni nyakati tofauti, hapa sasa hakuna kubebwa ni kazi tuu!. Poleni!.

Declaration of interest:
Mimi natoka Kanda fulani, wengi wetu tunakabiliwa na tatizo la kisaikolojia liitwalo "male chauvinism" ambapo we don't believe in "strength of a woman",or in "girls powers".

Kwetu sisi "a woman's place is at the kitchen", ila pamoja na kuwaona wanawake stahili zao ni jikoni tuu, watu wa kabila langu ndio tunaoongoza kuthamini wanawake kwa kuwapenda watuhudumie kuliko makabila mengine yote nchini Tanzania, na tunapenda wanawake wengi hadi kujikuta tunaona sifa kuwa na wanawake wengi na watoto wengi!, tena tunaongoza kwa kuhonga, kuanzia kuhonga pesa nyingi, gari hadi nyumba na wengine wetu tumehonga hadi ghorofa!, (mfano mimi nyumba ninayoishi, nimeisha honga siku nyingi kwa kale cheupe), hivyo naishi kama mpangaji tuu, lakini linapokuja suala la kuwaamini wanawake kwenye mambo makubwa!, no way!, nafasi yao ni jikoni tuu!

Hivyo ukiniambia nitafute wanawake 5 wa kuwateua ubunge, nikajitahidi nikapata angalau wawili, ushukuru Mungu sana kwa hao wawili na kunipongeza badala ya kunilaumu, maana hapo ndio ujue kuwa nimejitahidi sana kutafuta ndio wakapatikana angalau hao wawili, nikawateua, vinginevyo...

Wasalaam

Paskali

=====
Wana JF, jifunzeni kufanya rejea:

> Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?!

> Siku ya Wanawake Duniani: Tuwakumbuke Top Ten Wanawake Wakurugenzi Wakuu Wa Taasisi Kubwa
 
Kwangu binafsi sitaki kuungana na Pascal moja kwa moja ila nataka kuwakumbusha wanawake hasa wa Tanzania kuwa tabia za kupenda SLOPE muache.

Nimesoma primary mpaka chuo kikuu hawa watu (wanawake) ni watu wa ajabu sana. Twende turudi hawajiongezi hasa inapokuja uwanja wenye ushindani sawa.

Mashuleni tumeshuhudia ktk harakati za kudai haki zetu wakiwa nyuma siku zote na huwa mpaka wasukumwe kwa mijredi.

Katika kugombea uongozi au kujifunza mambo ya kiuraia ni wapuuuuzi sana, kupiga kura kwenyewe wanatamani wakaongwe au watongozwe.

Njoo issue ya kufanya harakati za haki za kiraia wako nyuma mpaka kero! Hapa jukwaani wapiga kelele wa haki za akina mama km hii issues ni wanaume as if wao hawapo..! POOR TANZANIA WOMEN.
 
Tanzania kila mwananchi anafahamu sheria!

Nadhani unachofanya ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa!

Siasa za fuata bendera zimefanya baadhi ya watu hata waliokuwa weledi kuwa wajinga.

Nafahamu umeingiza vijembe (mockery) kwenye hoja zako lakini msingi wa ukweli Rais amefanya kazi yake kama inavyotakiwa na Katiba ya Tanzania.

Don't hate the player hate the game!
 
wenye sifa naimani wamejaa tele,shida ni mteuaji viwango vyake hawafit pia mfumo dume nahisi upo ndani yake, nilishangaa siku ile anaigiza sauti ya kubana pua ya mwanamke (mke wa waziri mmoja mwandamizi aliyeitilafiana na trafiki) ,mimi binafsi niliona kama ni dharau kwa mwanamke,kwa kiongozi mkubwa kufanya vile mbele ya hadhara

ila tumuombe sana kama yeye anayosema Kuongoza nchi ni kazi sana
"But I sense a whiff of sarcasm in the piece...." BY NYANI NGABU....:p:p:p
 
Paskal Leo umeteleza kaka

Ingawa huyu bwana paskali kuna wasaa haeleweki msimamo wake dhahiri lakini ukilisoma vema andiko lake utabaini utumizi mkubwa wa mbinu ya kisanaa ya kejeli.

Nasema hivyo kwani ukifikiria kwa umakini utagundua wapo wanawake wengi mno wenye sifa kemkem kuwazidi hata madume!Wapo kina Tibaijuka, Dr. Malecela,.....nk.

Hivyo Paskali anajaribu kufikisha ujumbe kwa njia ya kejeli. Ni sawa na akuambiae ww una ngozi nzuri, teketeke, nyeupe na isiyo na makovu wakati unajijua ww u mweusi, ngozi ngumu na yenye magamba! Yaleyale ya kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa

Ila hajapenda kuandika hivyo...hana jinsi anahofia kuitwa mchochezi!nani asiyeogopa kibano cha wale jamaa wa miwani myeusi....wakiziponda korodani zako utatia adabu.

Hata kiba Shaaban Robert kwa kuhofia kunaswa na makucha ya watawala waliamua kuandika kazi ambazo zilikuwa ba mabdhari+wahusika wa kufikirika!...

Rejea Riwaya ya Kusadikika.
 
Hahaaa ninachoona Pasco kaongea kwa upande wa pili, Kagusia katiba na kugusa kipengele, "at least 5" maana yake wawe 5 ila wasiwe chini ya 5, sasa mpaka sasa nafasi zilizobaki ni 2 tu na wale 2 walioteuliwa awali labda ndo ifikie 4 (ikiwa atawateua wanawake ambapo pia hakuna uhakika kama atafanya hivyo).

Kwa kipengele hicho tu Mkuu yupo kinyume na katiba.

Pili kusema kutegemea slope/upendeleo, japo mwandishi kakiri wanawake wenye CV zilizoshiba wapo wengi tuu ila vigezo na masharti ndo shida, sasa tujiulize Vigezo na Masharti gani ambayo hayapo kwa kanuni za katiba ili hao wenye CV wasiteuliwe?

Na mwisho mwandishi kaelezea dhana ya kule atokako jinsi wanavyowachukulia Wanawake, hawa-Value sana hasa kiuongozi kuwa wataweza, so kacompare na teuzi hizi yawezekana zimefuata mfumo huo, ikiwa mkubwa ni wa huko pia?

Kingine unachoweza dadavua ni je, hao wawili wanawake waliokwisha teuliwa hawajafanya mazuri kumuonesha mkuu kuwa wanaweza zaidi hivyo kuwa na hofu akiongeza wengine watamuangusha?

So nilivyomuelewa muandishi kuwa hajakubaliana na jinsi teuzi zinavyoenda ila kaelezea kwa lugha ya kinyumenyume.

Only Great Thinker will unlock Codes.
 
Ndiyo maana kuna katiba hata kama wewe uwe wa kabila gani lazima ufuate katiba inasaje harafu naona kama wewe una chembe ya ukabila achana na mambo hayo ya kizamani.

Pia unataka kuwaaminisha watu kuwa kuwa kila kiongozi ataongoza kulingana na kabila lake Na sio katiba harafu pia uwaheshimu wanawake kwakuwa sasa wapo wengi wasomi wanawake ambao wana sifa nzuri kushinda hata hao unaofikilia.

Kwa hiyo take note usiwe mpotoshaji raisi ni taasisi ambayo ipo kisheria kila kitu lazima kifuate sheria Na sio mawazo ya kabila lako kama ulivyo eleza
 
Back
Top Bottom