Tuache siasa kwenye mambo nyeti. Tuwe na wanasheria wa Taifa na siyo wanasheria wa Serikali

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
1,287
1,604
Kwa ubush lawyer wangu ukifuatilia matukio ya Sabaya mahakamani na matukio ya Mbowe mahakamani unaona kabisa wanasheria wa Serikali wanahama kwenye taaluma ili kumfurahisha mwanasiasa mwenye vifaru. Wakati huyo huyo mwanasiasa ndiye aliyeagiza.

Kumfanya mwanasheria wa Taifa kutampa Uhuru wa kutoa ushauri na kupitia ushahidi kabla yakupeleka mahakamani.

Kuwa mwanasheria wa Taifa kutamlinda na ajira yake.

Chama chochote kitakachokuwa madarakani ndicho kiwe na mwanasheria wao kwenye chama.

Tutaendelea kuongoza Nchi kwa mikopo tunayoita vita ya uchumi kwa kutumia pesa nyingi kwenye kesi za maagizo ya mwanasiasa kulinda matumbo yao.
 
Ungana na Watanzania walio wengi wanaodai nchi ipate KATIBA mpya,mada yako inahitaji mabadiliko ya kisheria chini ya KATIBA mpya.
 
Back
Top Bottom