Tuache mijadala ya udini plz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuache mijadala ya udini plz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkerio, Dec 6, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mkerio Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2006
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa mwanachama wa JF siku nyingi kidogo. Uzuri wa JF ni kwamba wanachama wengi wamesoma angalao kufika form IV. Huwa kila siku nasoma makala na si mimi tu hata maprofesa na wasomi wengi ni wanachama. Sasa naomba ili JF iendelee kuwa blog makini tujaribu kujadili mambo makubwa ya kulijenga taifa. Tz tuna matatizo ya rushwa, umaskini, katiba, mbovu nk. Tujikite huko kuliko kujadili mambo madogo kama vile baraza la mawaziri lina wakristo na waislamu wangapi nk. Kujadili mambo madogo haya ni kuonyesha uchanga wa fikra. Ni ushauri tu lakini
   
 2. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli lakini kinacho leta tatizo ni kwamba kuna members wametumwa huku kuleta issue ya udini ili hata haya ya ufisadi, katiba mpya yasiendelee kujadiliwa.

  Mimi napendekezo moja tusichangie issue ambazo ziko tata kama za dini kwa sababu haina maslahi kwangu na kwako ila kwa walioko madarakani kuendelea kutumia ujanja wao kututawala na kuchukua rasilimali zetu bure.
  Kwa upande mwingine maana ya demacrasia ndio hii, waache watu wawe huru kujadili kila kitu ili na sisi tufahamu hata na hao wanaowatuma kuja kuleta udini humu wafahamu kwamba ukweli ukoje.

  Mfano kuna jamaa moja alikuwa na kelele kinoma baada ya issue yake kujadiliwa hapa JF akawampole maana aligunadua hata watu aliokuwa anawategemea wanamkosoa kwahiyo akaona atulie ili asiendelee kujishushia heshima.

  Maana JF imejaa watu wenye uelewa mkubwa mkubwa sana ingawaje kuna baadhi ambao wanashindwa kusimamia hata waliyoyahubiri muda uliopita.
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkerio,

  Heko mkuu kwa kuliona hili na hata mimi nimeliona hili.Ni karibuni tu niliamuwa kuwa member hapa JF, nilivutika na banner ya Great thinkers. Kabla ya hapo nilikuwa nachungulia mara moja moja na nilikuwa navutika na hoja jinsi zinavyoshushwa ila sasa hivi, hasa baada ya Uchafuzi mkuu imekuwa JF pia inachakachuliwa.

  Jana nilipata wazo kama lako la kutaka kuwatanabahisha great thinkers kuwa "gari linaacha barabara sasa" na niliandika hiyo mada, "Changamoto kwa Watumiaji wa JF" baada ya kui-post , naingia ku-peruse posts nimekutana na hii ya kwako.

  Umefanya jambo la maana kututanabahisha. Kweli kuna mambo ya msingi ya kuyashughulikia, mlalahoi wa TZ anaumia, mjasirimali mdogo anaumia, mfanyakazi anaumia. wanahitaji sauti ya kuwatetea. Tuache longolongo. wanaJF!
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Asanteni kwa kuanzisha mada hii. Ninaungana na wote waliotoa msimamo wao kuhusu mijadala ya dini ambayo haitufikishi popote zaidi ya kupoteza wakati na kututenganisha. Ni ukweli wa kikatiba kuwa Tz haina dini ingawa wa TZ wanazo dini zao. INATOSHA. Kila mtu abakie na imani yake moyoni, hadharani tujadili mambo ya kumkomboa Mtanzania.
  Tuna masuala kama katiba, umeme, maji, barabara mbovu, ajira, mishahara mibovu, pensheni, elimu duni (kuanzia chekechea hadi vyuo, uhaba wa madarasa, samani, walimu, vifaa vya maabara, nobe hata chaki hatuna sisemi sayansi na teknolojia), afya, usafiri na miundombinu, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma, mikataba mibovu, uongozi bora... Orodha haiishii hapa. Kwa nini tunayawacha haya tunajadili dini na dini ya mtu.
  Tuamkeni Watanzania. JF ni mahala muafaka pa kuanzisha mijadala ya kujenga, ya kumkomboa Mtanzania na wala sio dini. I-N-A-T-O-S-H-A.
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  huwezi kuacha kujadili dini wakati kila mtu ana dini labda kama ni mpagani ndio huna cha kusema ila sisi wenye dini lazima tujadili na kuvutia kwetu,mkristo anapenda ukristo wake na muislam nae pia anapenda uislam wake ndio maana kikwete amechagua viongozi waislam wengi ingekuwa sio kuogopa macho na maneno ya watu angachagua waislamu wote kila sekta kama alivyofanya nyerere kila mkristo msomi enzi za nyerere alikuwa kiongozi,hili halizuiliki na mimi naona ni sawa tuuu,ukristo upo,ukabila upo ,ukanda upo na yote haya hayaepukiki tuache unafki.

   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuanze na Rais wa TZ aache kujadili udini ndiye anayechochea udini tanzania
   
 7. S

  Sufian New Member

  #7
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba mijadala ya kidini haijengi bali inabomoa kwani inavyoonekana wengi hatuna elimu za dini na ninaamini huwezi ukajadili jambo usilokua na elimu nalo sanasana tutaishia kulumbana mwishowe kujengeana uhasama hatimaye tukawa hatujafikia lengo la kuelimishana maswala ya dini tuwaachie viongozi wa dini.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Mimi pia nilishakemea kuhusu hii mijadala ya udini mpaka nilifika kuwalaumu mods kuwa wanailea hali hii kwa kuruhusu mijadala hii. Ingekuwa mijadala ambayo ni elimishi sawa, lakini siku zote mijadala hii ni ya kushambulia imani za wengine na kukashifiana. Narudia tena kuwa dini ni suala la mtu binafsi na mungu wake kwa wale wanaoamini.Ila na rais wetu anahusika sana kwa hali hii kwani ameitumia wakati wa kampeni ili kuvunja umoja wa watanzania katika kukabiliana na tuhuma za ufisadi zinazokielemea chama chake, hivyo watu kuanza kujadili udini badala ya ufsadi, sasa uchaguzi umekwisha lakini mbegu aliyopanda JK inazidi kumea.
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  nakubali mia kwa mia kiongozi
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  sahihi
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...