TTCL hatarini kunyang’anywa soko

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Tanzania imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) liko katika hatari kubwa zaidi ya kunyang’anywa soko na makampuni mengine ya simu kutokana na upungufu wa mtaji.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Februari 16, 2022 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Silaa wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli zilizofanywa katika kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Mbali na TTCL kamati hiyo imebaini upungufu wa mitaji katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Amesema TTCL lipo katika hatari kubwa zaidi ya kunyang’anywa soko kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na kampuni nyingine za simu hapa nchini hasa Vodacom, Airtel, Tigo na Halotel.

Silaa amesema ili TTCl iweze kufanya uwekezaji mkubwa linatakiwa kuwa na mtaji wa Dola za Kimarekani milioni 752 lakini hadi sasa shirika hilo lina mtaji wa Sh370.465 bilioni tu.

“Serikali iangalie namna bora zaidi ya kuongeza mtaji wa Shirika hili kwa kuwapatia kiasi cha Sh360.09 bilioni kilichoombwa na Shirika kwa sasa ili Shirika liweze kufanya uwekezaji wenye tija,”amesema.

Kwa upande wa TPDC umeendelea kuwa hasi ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/20, mtaji huo uliongezeka kutoka mtaji hasi wa Sh 354.8 bilioni mwaka 2018/19 hadi mtaji hasi wa Sh331.2 bilioni mwaka wa fedha 2019/20 ambapo ni ongezeko la asilimia 6.7.

Amesema licha ya ukweli kwamba, mtaji wa TPDC umeendelea kuwa hasi kutokana na hasara iliyopatikana katika mwaka wa fedha 2014/15 ambayo ilisababishwa na mkopo wa Dola za Kimarekani bilioni 1.194 zilizotolewa kwa ajii ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. “Mkopo huo uliingizwa kwenye hesabu za Shirika na hivyo kusababisha Shirika kupata hasara ya Sh257.2 bilioni iliyotokana na matumizi ya gharama za riba na mikopo na hasara ya kubadilisha fedha (exchange loss) kutokana na mkopo husika,”amesema.

Amesema kwa kiasi kikubwa mkopo huu ndiyo umesababisha mtaji wa Shirika kuwa hasi pamoja na faida ambayo Shirika limekuwa likipata katika mwaka wa fedha 2019/20 na 2018/19.

Amesema pia katika TADB imebaini changamoto ya upungufu wa mtaji katika benki ambapo benki ilianza na mtaji wa Sh60 bilioni ingawa mtaji ulioidhinishwa (Authorized Capital) ni Sh800 bilioni.

“Ili kukamilisha mtaji ulioidhinishwa, Serikali iliahidi kutoa katika bajeti yake ya kila mwaka kiasi cha Sh100 bilioni. Kamati inatambua juhudi mbalimbali za Serikali katika kuiwezesha Benki hii kwa kuipatia kiasi cha Sh208 bilioni, mnamo Disemba 2021,”amesema.

Amesema kamati hiyo inashauri kuwa jitihada za Serikali ziendelee ili TADB iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi

Chanzo: Mwananchi

=========

Je, unashauri nini kifanyike ili TTCL ishike soko la mawasiliano hapa Tanzania na ukandwa na Afrika ya Mashariki?
 
Silaa amesema ili TTCl iweze kufanya uwekezaji mkubwa linatakiwa kuwa na mtaji wa Dola za Kimarekani milioni 752 lakini hadi sasa shirika hilo lina mtaji wa Sh370.465 bilioni tu.
 
TTCL ni kuuzwa kwa private tu serikali ijitoe kabisa katika haya mambo yakufanya biashara waachie wawekezaji kikubwa kusanya kodi weka sera nzuri za kiushindani waacha watu washindane kikubwa kusanya kodi zako bure bila kuwekeza hata centi moja haya mashirika ni mizigo vunjilia mbali.
 
Bila kuwa na mtaji wa kutosha, shirika la simu lazima life tu.

Teknolojia inakimbia sana na kila mara makampuni ya simu huitajika kufanya modernizations.
 
Walikuwa hawatoi gawio hawa?
Tangu lini serikali ikafanya biashara yenyewe na ikafanikiwa? Haya mambo Serikali haijifunzi tuu?? Achia sekta binafsi ifanye, Serikali kusanyeni kodi, tengenezeni infrastructures nzuri za watu kufanya biashara.
 
Mkubwa Gani Anataka Kujimilikisha?

Ile Ya Airtel Ilifikia Wapi Ilitakiwa Kuchunguzwa Na Kurudishwa Kwa TTCL?
 
Internet ndio biashara sasa hivi na yenye future; waachane na voice, wakijikite kwenye kusambaza internet majumbani. Dar Es Salaam peke yake wanaweza kupiga hela nzuri sana. Sambaza fiber maeneo yote yenye watu wa middle na upper class, make sure kila nyumba ina fiber connection.

1645100240846.png


Mipango ipo mingi, ila utekelezaji ni changamoto.
 
TTCL iwapo watafanya mambo matatu in 2 years to come watakuwa number one telecom company in Tanzania.

TPDC wana uwezo wa kulipa madeni na kuwa Shirika lenye kuzalisha pesa nyingi hapa nchini iwapo wataanzisha 3 projects zinazousiana na gesi asilia hapa nchini- TPDC mpaka sasa awajielewi na awapo kibiashara hilo ndo tatizo lao kubwa . Natamani ningepata nafasi ya kuonana na wahusika wa TTCL na TPDC niwape ramani ya vita

😃
TADB hawa nao wanaendesha hii bank kama chombo cha siasa! Iwapo wangejikita zaidi kwenye kuwezesha ukulima wa mihogo, Soya, Shahiri na alizeti na kujizatiti kwenye ku add Value kwenye zao la Alizeti wangepiga hatua kubwa sana kama Benk kwenye kukuza mtaji wake! Tanzania 2021 imetumia Sh443 billion Kuagiza mafuta ya alizeti nje ya nchi (How Tanzania plans to curb cooking oil shortages) Uhitaji wa muhongo na Soya China pekee ni fursa tosha kwa TADB kujipanua na kuongeza mtaji wake.

Hizi taasisi zote tatu zina uwezo wa kuwa chachu ya maendeleo ya Kiuchumi hapa Tanzania -tatizo nnaloliona ni kukosa watu staiki wenye uelewa wa mambo na nini kifanyike kupaisha mitaji yao
 
TTCL ni kuuzwa kwa private tu serikali ijitoe kabisa katika haya mambo yakufanya biashara waachie wawekezaji kikubwa kusanya kodi weka sera nzuri za kiushindani waacha watu washindane kikubwa kusanya kodi zako bure bila kuwekeza hata centi moja haya mashirika ni mizigo vunjilia mbali.

Chamsingi uongozi TTCL ubadilishwe na shirika libadili mfumo wa umiliki. Wathaminishe mtaji wa shirika alafu wajisajiri ktk soko la hisa

Hapo watafanikiwa
 
  • Thanks
Reactions: aye
Internet ndio biashara sasa hivi na yenye future; waachane na voice, wakijikite kwenye kusambaza internet majumbani. Dar Es Salaam peke yake wanaweza kupiga hela nzuri sana... sambaza fiber maeneo yote yenye watu wa middle na upper class, make sure kila nyumba ina fiber connection.

View attachment 2122033

Mipango ipo mingi, ila utekelezaji ni changamoto.
Hata hiyo voice ni internet tu mkuu
Kinachofanyika ni kubadirisha mb kuwa dak au kuwa sms
 
Back
Top Bottom