TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

VIFURUSHI VYA INTERNET
Spidi ni ndogo sana hapa kibaigwa Dodoma, na havimvutii mteja kiujazo kutumia lain ya ttcl ukilinganisha na mitandao mingine.

VIFURUSHI YA DAKIKA
bado havimshawishi mteja kutumia lain ya ttcl kulinganisha na mitandao mingine.

USHAURI
Mtufanyie vizur kweny spid ya internet na vifurushi vya internet mfano weka kwa buku jero mteja apate 1GB na dak100 mitandao yote kwa wiki...lazima tuzitafute lain zetu za ttcl kweny mabegi na kuanz kuzitumia.
 
Mnajitahidi sana katika vifurushi vyenu🤝!!
 
Buhigwe Kumenoga!
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua mnara wa Mawasiliano wa 4G Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.
Buhigwe Garuka Imuhila Halanoze!











 
Sasa sehemu hakuna maji wala barabara za kutosha Ww unawapelekea 4G iwasaidie nn

Hamna mkoa maskini kama kigoma ndani ya Tanzania hii

Hata huko kwa makamu wa raisi pamechoka hatar

Nafurah sana kuzaliwa uchagani

Karibuni tunywe mbege wandugu
 
TTCL kadiri siku zinavyosonga mnazidi kuwa watu wa hovyo tuu, Leo ni karibu siku ya 5 sasa SMS hazitoki, yaani kero tupu!
 
Mnara wa simu unazinduliwa na Makamu wa Rais !! Mkuu wa wilaya atazindua nini sasa!!
Tanzania tutafika uchumi wa kati wa juu tukiwa tumechoka sana.
 
Ufipa tulieni dawa iwaingie
 
Naomba mnirudishie Dakika Zangu na SMS zangu...


Mbona mnakuwa WEZIIIIIIII??

nilijunga kifurushi cha jiachie... Dk 8000+ Sms 7000+ MB ziliisha..

Leo nakuta mmebeba vilivyobaki vyoteee na nature ya kifurushi changu hakina EXPIRE DATE... Nahitaji ufafanuzii nimewatumia EMAIL na nimewapigia customer care wenu naona hawajielewi
 
@Kanungila Karim
 
Mbeya ofisi napata wapi?
 
Turudishieni bando letu la Bandika Bandua
 
TTCL Customer Care kunani leo tarehe 4.1.2022 Dar es salaam?,mbona leo network ni shida sana?,tangu asubuhi hakuna kitu kabisa!!.

Shida ni nini?,Je kuna tatizo?.

Nimejaribu kutumia line za mitandao mingine naona network ni nzuri,tatizo nikitumia line ya TTCL kwenye network yaani haipo kabisa!.

Hii hali inakera na kuudhi sana ukizingatia mimi mtandao wangu pendwa kwenye masuala ya internet ni TTCL,nina bando la wiki nzima lakini ninavyopata taabu asikwambieni mtu.

Sijawahi kushuhudia hili tatizo,ni leo tu!,na ndiyo maana ninaomba kufahamishwa hili tatizo limesababishwa na nini?

TTCL Customer Care
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…