technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,485
- 50,898
Huyu jamaa naye kaanza kuiga mambo ya watu weusi mtoto wake ndiye alitengeneza cabinet..
Sasa mkwe ni mshauri mkuu wa mipango yote ya uchumi na mambo ya mashariki ya kati .
Wacha tuone mwisho wake itakuwaje.
======
Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.
Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.
Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.
Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.
Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.
Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.
Chanzo: BBC