Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Huyu jamaa naye kaanza kuiga mambo ya watu weusi mtoto wake ndiye alitengeneza cabinet..

Sasa mkwe ni mshauri mkuu wa mipango yote ya uchumi na mambo ya mashariki ya kati .

Wacha tuone mwisho wake itakuwaje.

======

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

Chanzo: BBC
Mkuu kwa sheria ya huko kwao katiba yao kuna kifungu cha sheria kinamruhusu rais kumteua myu amtakae bila kupingwa!! Ila kitakacho sumbua hapo huyo alieteuliwa inasekana sio mtu wa siasa yaani ndo baado hajakomaa kiitikadi!!
 
Kwa tunaomfahamu Jared Kushner hatuwezi kushangaa wala kuponda! Kijana yuko njema kichwani na ni good strategist.. Ana mchango mkubwa sana mpaka Trump kuingia Ikulu na ni moja ya watu wachache Trump anaowaamini 100%
Umesababisha hadi nikasurf online nione weledi wa Kushner.

Nanukuu:

Hana akili aliingia Havard baada ya baba yake kulipa 2.5 milion $.
Mikakati yake mingi imebase kwenye kumwaga hela kwa wanasiasa (mpaka wa Democrats) na kua karibu na watu wenye influence.
Amekua na msaada mkubwa kwenye kampeni za Trump lakini ana roho ya kisasi kwa kuhakikisha Christie hawi na nafasi yoyote kwenye crew ya Trump baada ya kumfunga baba yake miaka ya nyuma.

Naona upepo unavuma tu kwa upande wake, kila anachotaka kinakua.
 
Mbona sijaelewa umecoment nin....kateuliwa mke wew unasifia kijana...sasa tukuelewe vip
Sio mkewe, ni mkwe.! Mume wa mtoto wake Ivanka..
Na kabla hujaponda sana nenda kafanye tafiti ufahamu Jared Kushner ni nani na amepigana kiasi gani kusaidia ndoto ya urais wa Trump kutimia!!
 
Fisi anaposubiri mkono wa binadamu udondoke. Anapoona anatembea kushotokulia anasema " huo huo unadondoka" mara binadamu anaweka mikono mfukoni; fisi anaguna ayaaaaa!! Jamaa akianza
tena kutembea na fisi anaanza tena " huo huo unadondoka.

Kwahiyo mtasubiri saaaana hilo anguko la Marekani.
Mwambie kk
 
Huyu jamaa naye kaanza kuiga mambo ya watu weusi mtoto wake ndiye alitengeneza cabinet..
...
Tatizo kwa Afrika hizi teuzi za undugu huwa ni namna ya kulifisidi taifa na kulindana. Nadhani, umeona tofauti ya Trump na Afrika - hatachukua mshahara wa Serikali; kwa Afrika thubutu! Hao "ndugu" ndani ya muda mfupi wanageuka mabilionea na miungu watu wasiohojiwa na chombo chochote. Yule wa Marekani sio tu ni bilionea bali ni kichwa balaa - pita CV yake ujionee.
 
Kwa tunaomfahamu Jared Kushner hatuwezi kushangaa wala kuponda! Kijana yuko njema kichwani na ni good strategist.. Ana mchango mkubwa sana mpaka Trump kuingia Ikulu na ni moja ya watu wachache Trump anaowaamini 100%
Kaka kumvua chu.p.i Ivanka binti mkubwa wa Trump sio mchezo mazee; lazima uwe umekamilika kila idara. Hivi ile familia kwanza unaanza kuingiaje pale? Eti unaenda TRUMP TOWER "kumtongoza" Ivanka; dah ha ha ha! sio mchezo.
 
trump_family.png
 
Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Jared Kushner na mke wake

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

Source,:
MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago
 
Back
Top Bottom