Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

I second with you, mi naamini ulobby wake hasa na team yake ya jews inamsaidia katika harakati zake

Baba yake aliwahi kutumikia kifungo na prosecuting attorney alikuwa ni Gov. Chris Christie enzi hizo akiwa US attorney.

Na ndo maana kwenye transition team Gov. Christie na huyo dogo wali butt heads hadi kupelekea Christie kuondoka.

Hii nafasi kapewa kwa sababu ya loyalty alonayo kwa Trump by way of marriage.

Ila ni kichwa? Nah...not to my standards.
 
Huyu jamaa naye kaanza kuiga mambo ya watu weusi mtoto wake ndiye alitengeneza cabinet..

Sasa mkwe ni mshauri mkuu wa mipango yote ya uchumi na mambo ya mashariki ya kati .

Wacha tuone mwisho wake itakuwaje.

======

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

Chanzo: BBC
Kaka hiyo kawaida sana .kwani ni lazima mtu ateue mtu ambaye anaamini atamsaidia na kiwa royal kwake.but huwa nashangaa sana kwa hapa kwetu pale vyama vya upinzani hulalamika kuwa CCM wanapeana wenyewe kwa wenyewe
 
Ikumbukwe kwamba huyo mteuliwa hatapokea mshahara wowote wa serikali kwa kazi hiyo aliyopewa
 
Baba yake aliwahi kutumikia kifungo na prosecuting attorney alikuwa ni Gov. Chris Christie enzi hizo akiwa US attorney.

Na ndo maana kwenye transition team Gov. Christie na huyo dogo wali butt heads hadi kupelekea Christie kuondoka.

Hii nafasi kapewa kwa sababu ya loyalty alonayo kwa Trump by way of marriage.

Ila ni kichwa? Nah...not to my standards.

Nimeona hii makala washington post ikimchambua huyu kijana
For Trump son-in-law and confidant Jared Kushner, a long history of fierce loyalty

Back
Top Bottom