Unanikumbusha mbali kweli, miaka 19 iliyopita nilipokuwa S/msingi Kiloleni Tabora darasa la tano.<br />
Mwalimu alikuwa anafundisha hesabu za VIPEO na VIPEUO, akatoa mfano 10 kipeo cha pili ni sawa na 10x10 = 100 siyo 10X2; mbili kipeo cha tatu ni sawa na 2x2x2 = 8 siyo 2x3. Akasema: "Sasa nataka mtu aniambie 10 kipeo cha 3 ni sawa na ngapi, usikurupuke tu na kuropoka, ukikosea tu utaniona!!!" Nikaona mbona swali simple, na vile nilikuwa kipanga, nikanyoosha mkono faster huku nikijua 'lkn hapa sitakiwi kufanya 10x3=30', ghafla akani-point nijibu, lol NIKAROPOKA na kusema 30! Alinilamba kofi hilo! Kumbe akilini mwangu 30 lilikuwa ni jibu ambalo SIKUTAKIWA KULITAJA!<br />
Lkn kwa kuwa nilikuwa naamini najua (hayo makofi kwangu sana yalipunguza heshima kwake) na S/msingi nilifaulu, hesabu nilipata 48/50, Lugha 47/50, Maarifa 45/50. O-level nikapata B-Maths B+, Physics B+, Chem A, Bios A. A-level nikasoma PCB - hapa nilianza kutokusoma kwa pressure, nikaona niwe nasoma vitu ambavyo nitavitumia katika maisha yangu, nikawa nasoma Bios na Chem (Physics nilisoma topic 4 tu), nikapata division I (point 9), nikaenda Muhimbili - I AM NOW A MEDICAL OFFICER - DOCTOR (MD).<br />
<br />
Siku akija ninapofanyia kazi akiwa anaumwa au ndugu/ jamaa yake anaumwa nitamtibu, nikishamtibu nitamkumbusha: "Mwalimu unakumbuka mwaka 1992 ........?!" Atalia! Akishamaliza kulia nitamtoa out kwenda kupata moja moto moja baridi na kula kuku kwa mrija, thereafter nitampeleka home akapajue anapoishi mwanaye, then nitampatia bussiness card yangu - "In case of anything related to health don't hesitate to contact me AT ANY TIME, I am ready to help you 24/7!"