True Story: Nimechezea Bahati

tzfanatic

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
626
382
Kila Nkisikiaga hii nyimbo Ya Man X ft Dully Sykes Najisikia Vibaya Sana Ingawa Wakati Mwingine napiga Moyo Konde najifariji, Kwa kusahau Yale Ya nyuma...

Wanazuoni wanasema kila kinachotokea kina sababu yake ya kutokea, Kinachopaswa ni Kujipanga....kuweza kusawazisha ama Kuongeza Kasi Ya mabadiliko hayo.....

BACK 2000'S

Ilikuwa Ni Jumatatu Tulivu Ya Mwezi wa Kumi na Mbili, Ya Tarehe 26 maarufu kama Boxing Day., Kama Kawaida watoto wa Uswazi wa kipindi hicho cha mwanzoni mwa miaka ya 2000, tulipiga Pamba Zetu, Za sikukuu kila moja kusubilia Hiace Kali iliyo na mziki kwa kipindi hicho Almaarufu kama Dungu....

Muda Ulizidi sogea, huku pilika pilika na maskani watu wakiwa hawakauki, kama mnavojua mitaa yetu ya Manzese,Tandale na Kigogo...Tukisubili safari ianze rasmi Kuelekea Coco Beach....Kupitia Kinondoni. Ilipofika Mid noon kama Saa nane hivi, Vuu Dungu likafika Karatasi ikachukuliwa Tukajihesabu tulochanga Safari Ikaanza...

COCO BEACH....
Baadaya Ya kama Dakika 15 tukawa ndani ya Coco Beach, Tukajichanganya na kuhaidiana na Dereva wa Hiace Ile maarufu kama Dungu, ije ituchukue saa 06:30 jioni, na tukaonyeshana sehemu ya kukutania,....tukajichanganya kwenye Maji na wengine kwenye vinywaji na michezo mbali mbali, ....nikiwa nimeongozana na rafiki zangu , mimi nikajichanganya kwenye Maji....nakupiga mbizi nikiwa pira langu mdogo mdogo, mara ghafla mapigo yangu ya moyo yanaenda kasi baadaya ya kuchomwa na kitu mgongoni, . nageuka na kukutana na binti mmoja mrembo sana mwenye mchanganyiko wa kisomali , aliyevalia vazi moja zuri sana lenye uzuri wa sura na shepu yake, niliganda ghafla kama dakika kadhaa , nikitazama sura yake na kifua chake kidogo kilichofungasha viduara viwili vizuri sana, na vyenye kuvutia haswa, Hakika Mola alijua Kuumba na sifa kedede kede kamjalia, alikuwa na Macho makubwa yenye uduara nadhifu, nyusi kiasi zilizopangwa vizuri, Ingawa kiumri nilikuwa mdogo, nisiyefika 18 but nilijikuta na fall ghafla bila kutaraji.

FIRST MOVE,
Baada ya kuganda kama muda wa dakika, takribani 5 , nikashindwa jizuia nikatoa salamu, moja ya kiingereza cha kizushi, bila kutaraji, naye akaitika nikamtajia jina langu , akataja na lake japo first time alinidanganya..., nikaomba kampani yake tuwe pamoja walau , tufarijiane na kubadili mawazo pamoja, tukiwa ndani ya maji , akagoma na kuanza kurudi na kutoka kabisa ndani ya maji....moyo wangu nikajihisi mpweke na mjinga kwa kushindwa kumzuia kwa kumshawishi, nikasema its ok nitajaribu kila niwezalo walau niweze kumtia mkononi nami nikawatamba masela kitaa .........

Itaendeleaaa​
 
SECOND MOVE
Hii ilikuwa ni final move towards mtoto yule mzuri, wakati anatoka ndani ya maji ilibidi nimpige jicho , nione anaelekea wapi, kwa mbali nikamuona , yuko na kampani ambayo baadaye nilikuja kugundua ni familia yake,. Alikuwa ni mdogo wake mmoja wa kike, pamoja na dada zake wawili, walikuwa wamekaa juu kidogo jirani na ilipo barabara kuu ya Coco Beach,..

Mara ghafla uoga ukaniingia , nikawa najiuliza peke angu ndani ya nafsi angu jinsi gani naweza sogea jirani yake, ikizingatiwa alikuwa na ndugu zake , kiukweli yule binti alikuwa amenivutia sana na kwa mara ya kwanza nilikuwa na fill love inside, ....
....Wazo Likanijia
ghafla akili yangu ikafanya kazi kama ya mtu mzima, niende kuchukua kampani ya mabraza wawili ambao tulikuja nao ili kujenga , team ya watu wa tatu, ingawa sikuwaambia nia yangu Maana nilitaka iwe siri yangu kipindi namfuatilia yule bint mpaka nihakikishe nimefanikiwa kwanza.

wakati tunajisogeza kuelekea upande ule ambao walikuwa wamekaa yule bint na nduguze, mara ghafla alinyanyuka , yule bint kuja upande tunaotokea , nami nikawa namtizama kwa jicho la wizi mpaka ,jirani kabisa na yanapouzwa madafu...nami nikaomba udhuru na kuanza kumfuata nyuma nyuma,nikamgusa bega kidogo, then niacha kitabasamu furani , naye akajibu kwa tabasamu, then akaniuluiza..." una shida gani mbona hivi " nikamuomba samahani, kwa usumbufu maana nilikua ni mgeni kwake na ndio mara ya kwanza kukutana naye , ila mara ya kwanza inaweza kuwa na manufaa sana baadaye,..Nilichompendea alikuwa msikivu then atabasamu tena na kujibu ok.. tukaanza chat kwa maneno akaniuliza unatokea wapi, nikamjibu natokea kigogo-Luhanga, naye akanijibu anatokea mbezi beach inter-chick. Nilimueleza ya kuwa nimefurahi sana kukutana naye kwa mara ya kwanza na natamani na kutaraji tutafahamiana zaid mbeleni, akanielekeza anapokaa maeneo ya interchick , na mahali ambapo naweza kumpata kiurahisi, maana alikuwa mwanafunzi ambaye amemaliza std 7 anajiandaa kuingia form one kama kwa kipindi hicho,....

Alinambia Kama nataka mpita kwa urahis basi nende Kariakoo , mtaa wa Swahili na Nyamwezi walikuwa na duka kubwa la bidhaa, mchanganiko likiwa la jumla na rejareja.. Jirani kabisa na Muhindi wa Toto Kanko.

Tukapiga story mpaka jirani kabisa na Dada Zake then akanitambulisha kwa dada zake kama rafikiye tuliosoma wote, hawakuwa na nouma, na kwa kuwa giza lilishanza ingia tukaagana , pale kwa pronmise ya kuonana jumapili ya mwaka mpya ....then wakapanda kwa gari yao na kuondoka, nasi tukajikusanya kusubiri Hiace yetu..tuanze safari....

JUMAPILI MWAKA MPYA
Sitaweza isahau siku hii Maana , nilijisahau kabisa kwanza ilikuwa weekend pili Mwishoni mwa wiki,so mara nyingi maduka ya maeneo yale huwa yanafungwa....Nikatoka mdogo mdogo mpaka Karikoo na nafuu kidogo kulikuwa na ndugu zangu wanakaa maeneo haya mitaa ya Muhoro, so haikuwa tabu sana nikazamia kariakoo, Mpaka nilipoelekezwa na yule binti, ambaye kwangu alijitambulisha kama ,Nurat mazingira nilikuta yametulia na frem zote za maeneo yale zilikuwa zimefungwa, sio siri viungo vya mwili na akili yote ilichoka, nikashindwa nifanye nini, maana nikabaki najilaumu tu why nimekuja huku na kwanini sikuenda hata maeneo ya mbezi beach kama nilivoelekezwa , ila nikasema hakuna ubaya , nitamuona tu siku nyingine kama si leo basi kesho.

Nikajitosa kwa mama zangu wadogo kuwasabahi then , nikaasizi kama masaa kadhaa mpaka ilipotimu mida ya saa kumi na mbili na robo , kaka zangu wakaniomba niwape kampani kuelekea Bakhresa kununua Ice cream , kwa kuwa nilikuwa nilikuwa bored na akili yangu ikimfikiria Nurat nikaona poa ngoja nikaoshe macho...........

------------itaendeleaaaaa..................
 
Back
Top Bottom