True story kumhusu ndg yangu kipande cha mwisho

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,780
NOTE : KABLA HUJASOMA HAPA ANZA NA SEHEMU YA KWANZA KUNA THREAD ILIOITANGULIA HII. Bebiy alifika ktk mji aishipo Dadaake Riza.
Wakati wa mapokezi (namnukuu Riza)
Hee mwenzetu na mtoto tena ! Hiyo harusi lini ? Hadi mimba ! Hadi mtoto ?
Bebiy : "Dada tulizana kwanza"
Baada ya mapumziko mafupi. Ndy ufahamanishaji ukaanza, na ghafla kikazuka kilio, Bebiy alipojulishwa kufa kwa Karama.
Mazungumzo baina ya ndg hao yakahitimishwa na azma ya Bebiy kusema pale Yemen hatomaliza wiki, ni lazima aondoke kurudi Jeddah.
Riza alimwambia utaondoka vipi wkt wewe ni Mtanzania, hapa Yemen uko illegally na huko unapotaka kwenda nako ni hivyohivyo.
Bebiy alimwambia nitamuomba Mungu hatua kwa hatua mie na mwanangu mengineyo mbele kw mbele.
Wiki 1 mbele Bebiy akaondoka kule kijijini hadi Sanaa (capital city). Hapo aliuza vipuri kadhaa na alikwishapewa na Riza roadmap situated kua kutoka boder ya Yemen hadi kuingia Saudia kuna Checking Point ngapi.
So alipofika boder akashuka na mwanae kisha aka'cross by foot, hakupanda tena bus alilokuja nalo.
Hapa kwa kuokoa mda wenu ningependa nifupishe namna alivyovuka viunzi vya ma'polisi ila ieleweke kw kutumia vijipesa alivyokua ameuza vipuri alihonga kila palipotokea ulazima.
Ambapo check point ya mwisho alihonga mkufu wa mama J.
Hatimae Bebiy akafika kwao Jeddah, hoihoi , nderemo, vikatawala, na kisha vilio.
Baada ya siku mbili Bebiy akawa ameshawapa muhtasari wote kumhusu yeye na J. Kikafata cha kumtafuta Babaake J, MrTiba lakini haikua bahati kumpata kwani simu ya Tiba haikua hewani.
Masiku, miezi, miaka inakwenda mawasiliano na Mr Tiba hakuna, Bebiy ameshapata kazi na J amefika umri wa kuanza Shule na akaanzishwa Nusary, pia hadi wakati huo familia hii yote ikawa imeshadadavua kupata uraia, tatizo hilo halikuwepo tena.
Mtaani na pale nyumbani Bebiy alifahamika kama mama J.
Takriban miaka 6 imepita tangu Bebiy atoke jela.
Hiyo siku amekaa kazini ikamjia kama hamu kuijaribu No ya Tiba, my God ! Simu ikaita na kupokelewa, baada ya intro ikafatia ufahamishano wakutaneje, na hilo likafanyika na Tiba kupewa direction itakayomfikisha kwao Bebiy.
Wakati huo Tiba tayari alikwisha kua akijua mkewe alifia jela na kuzikwa na serikali, na hakua ameoa tena.
Siku ya kihistoria ikawadia Baba J original kufika kw Mama J, Photocopy !
Izingatiwe kwmb hadi muda huo Bebiy moyoni alikua na hamu ya kuolewa bt hapakua na mwanaume yeyote aliekwishampa proposal.
Tiba alipokelewa kwa hoihoi (haipishani na alivyopokewa Bebiy na J siku walipofika Jeddah)
Baada ya kupeana milolongo ya habari kuwahusu ikafata familia nzima kuondoka sitingroom na wakabaki Bebiy na Tiba.
Unadhani ni fadhila gani Mr. Tiba amlipe Bebiy kwa kumtunza J hadi J kufikia umri wa kwenda shule?
Jibu liko wazi ! Hivi niandikavyo Tiba na Bebiy ni mke na mume na wamepata watoto watatu na J ni wa4 Bebiy jina la kuitwa mama J halikuanguka chini hadi leo anaitwa hivyo.
Wapendwa wangu Jf membars habari hizi ananihadithia dada yangu wa tumbo moja ambae alikwenda Jeddah kimatembezi na akakaa hapo kwao Bebiy kw mwezi mzima (nasikitika dada yng huyu ni marehemu alifariki mwaka jana) namnukuu marehemu dada wkt anamaliza kunipa story hii alisema "unaliona hili gauni nililovaa ? Kanipa Bebiy kama kumbukumbu, ndy gauni alilokua anavaa akiwa jela.
 
Hii ni movie ya kibongo?kama ni muvi nakushauri msiipeleke sokoni,mtakula hasara.
 
Dah so tired at last nimemaliza.

Mh. Kabana pole sana! Hata hivyo ni muda mrefu story hii nimekaa nayo moyoni, nikichelea kufunguka nayo kutokana na urefu wake hatimae leo nikasema potelea mbali iwe iwavyo, nafunguka nayo.
 
Mh. Kabana pole sana! Hata hivyo ni muda mrefu story hii nimekaa nayo moyoni, nikichelea kufunguka nayo kutokana na urefu wake hatimae leo nikasema potelea mbali iwe iwavyo, nafunguka nayo.

at last umeitoa moyoni,
 
Kama hii story ni ya kubuni, una kipaji hivyo mtembelee Shigongo akupe tenda ya kusaply hadithi kwenye magazeti yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom